Hongera sana Sakapal, kwani ni bahati iliyoje kupitia the whole process hadi ukaitwa mama. Niliwahi sema hapa jamvini kuwa adabu ya mtoto wa kike hata kama anamuheshimu mama yake katu haiwezi fikia kama pale akijaaliwa kuzaa na yeye pia. Hili huwafanya wale wenye mama zao kuongeza mapenzi maradufu na kumuonesha mama namna gani wamthamini hata kama ni kwa vizawadi... Na pia huwa wakati mgumu sana kwa yule ambae kisha mpoteza mamake; wengi huona kama vile bado hakuweza kumuonesha mamake ni namna gani alimpenda na namna gani alivyo mtu wa thamani....
Wewe ulipata bahati, ukawa na mamako... Hongera saana. Kila la kheri katika maisha yako na mwanao pamoja na familia yote. Hongera...