sakapal
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,804
- 1,425
Habari zenu wanajukwaa wa MMU, leo ni siku ambayo ni ya historia katika maisha yangu.
Ni miaka kadhaa iliyopita yapata 14 sasa nimeamua kuishea pamoja na nyie ili mshereheke pamoja nami. Nilikuwa binti mmdogo kwani niliwahi kuolewa na baada ya harusi mume wangu alisafiri kwenda masomomi kwa miaka 4 kwa kipindi hicho ilibidi aache kazi kwani alipata sponsor ya serikali. Na mimi nilikuwa sijaanza kazi hivyo boom alilopata ndio alikuwa ananitumia kwa matumizi, alipoondoka aliniacha mjamzito na kwa kuwa wazazi wake walikuwa mkoani ilibidi nikae nyumbani kwa wazazi wangu ili kupata support ya ujauzito wangu na ilikuwa ndo mimba yangu ya kwanza.
Ilipofika siku ya kujifungua tulienda hospitali ya serikali, mama alinipeleka na tulifika hospitali mida ya saa moja asubuhi. Uchungu ulikuwa mkali na ulikuwa ukiongezeka kadri muda unavoongezeka, baada ya kunikabidhi kwa manesi walimwambia mama aondoke na amefika mikono salama, namumbuka mama aliniambia fanya vile utakachoambiwa na manesi ili usipate shida nikachukua begi langu nililoenda nalo na nikawekwa kwenye benchi. Baada ya mama kuondoka manesi walinisahau pale kwenye benchi nami nilikuwa najiskia vibaya na nafuu yangu ilikuwa nipate kitanda, alipita nesi mmoja nikamwambia sista naomba nisaidie najiskia vibaya yule nesi akanichukua na kuniepeleka kwenye kitanda kimoja na kuniambia panda hapa nikupime kupanda kwenyewe kwa shida vitanda virefu baada ya kupanda akashangaa hee hujavua c**pi utazaaje? daaah ikabidi nishuke tena baada ya kunipima ndo akanipeleka wodini.
Lahaula nilikuwa namuomba mungu nisaidie nimalize hiikazi salama kwani napata shida mmo, wodini kumejaa wamama wengine wana uchungu wengine hawana vitanda wamekaa wawili wawili nesi akaniambia haya tafuta kitanda ukae kuangalia sioni hata pa kujiegemeza nikisimama nazidi kujiskia vibaya, nikamwambia mmama mmoja naomba nisaidie sogea kidogo nijilaze walau nipate nafuu ya dakika kumi tuu akanipisha nikawa nazidiwa na uchungu bahati nzuri nesi akapita tena akaniambia wewe binti njoo huku tukupime tena maana unaonekana unakaribia kuiva. Kufika kitanda cha kupimia kirefu lazima upande ngazi baada ya kupanda anakwambia lala chali jamani huko kujigeuza nachukua dakika 3 basi baada ya kunipima akamuita daktari wa zamu, '' daktari njoo umpime na wewe huyu ni prime'' huku mie napata shida na maumivu ya uchungu baada ya kunipima yule daktari akasema nipelekwe leba tayari kujifungua kushuka hapo kitandani napo shida basi nikajizoazoa hdi leba kufika naesi akaniambia mimba yako ya ngapi nikamwambia ya kwanza akasema haya lete khanga au kitenge nikampa kitenge akanitandikia nasubiria mwana ashuke huku nasali kimoyomoyo.
Kufika saa sita mchana uchungu ukakomaa hauachi mara gafla wingu zito likafunga ikanyesha mvua kubwaa wakati huohuo nikajifungua mtoto wa kiume daaah nikashukuru mungu nesi akanionesha mtoto wangu na akaenda kumshuhulikia kwanza ile katoto kutoka tuu kakalia kwa nguvu basi baada ya mtoto kupata huduma zote nesi akanirudia mimi na alipomaliza akaniingiza wodi ya wazazi na hapo nilipata kitanda cha peke yangu n a mwanangu, kwa mara ya kwanza ndo nikawa mama na nikaanza kumnyonyesha mtoto wangu kalikuwa na kilo 3.4. Yule nesi aliyenihudumia akarudi kuniambia binti nimekuhudumia vizuri hata unipe hela ya maji nikamwambia haya mama maana alikuwa mtu mzima na aliomba kistaarabi kwenye kapichi kangu nilikuwa na elfu nne wakati huo nikampa elfu mbili basi akashukuru na kuondoka.
Jioni saa kumi mama akaja na shangazi kuja kunichukua kwenda nyumbani kwani niliruhusiwa kwa kuwa mimi na mtoto hatukuwa na matatizo yoyote. Basi maisha mapya yakaanza na nilipofika home nikamuita mtoto wangu Rainer maana alizaliwa wakato mvua inanyesha na ilinyesha gafla na baada ya kujifungua mvua ilikatika, nikanza kumuombea mwanangu maana niliitafsiri ile mvua kama baraka na nikamwambia mungu baraka hii mungu aliyomshusha nayo duniani basi iambatane nae hadi mwisho wa maisha yangu.
Nilijifunza kuwa mama ni wa kuheshimiwa sana na nilielewa kwa nini watu walikuwa wanaenda kanisani kutoa shukurani baada ya kujifunguakwani ile shuhuli asikwambie mtu ile ni karibu nusu kifo, nilienda kanisani nami kumshukuru mungu kutoka leba salama. Miaka yote hii nikagundua kuwa kuzaa sio kazi kazi ni kulea mtoto jamani inahitaji nguvu na hekima ya mungu, mungu azidi kunitia nguvu.
Hii ni habari ya kweli na leo ndio birthday ya kifungua mimba wangu Rainer, karibuni tushereheke pamoja, je wewe unakitu gani ambacho hutakaa ukisahau maishani mwako? Karibuni nawakilisha.