Siku akijibu mapigo msilie

Siku akijibu mapigo msilie

Status
Not open for further replies.
Kama nilivyokuwa natarajia baada ya kupata habari za jaribio la kuchukua uhai wa Tundu Lisu, akili za watu wengi ziliwatuma kumhisi rais Magufuli kuwa ndiye anahusika na jaribio hilo.

Mpaka sasa huyo bwana mkubwa hajalizungumzia tena hadharani hilo jambo zaidi ya yale maneno yake machache ya kulaani hilo shambulio kwenye mtandao wa Twitter.

Maneno mengi sana yanasemwa na nadharia kadha wa kadha zimebuniwa kuhusu uhusika wake.

Na kwa kadri nijuavyo yeye hajasema lolote juu ya hayo yanayosemwa. Naamini hajasema hivyo kwa makusudi tu na si kwa sababu hajui kuwa anasemwa semwa na kuhisiwa kuwa yeye ndiye mhusika.

Naamini huwa anapita sana humu na kusoma yanayosemwa na watu anaowaongoza.

Lakini naamini pia ya kwamba ipo siku atalizungumzia tu hili suala.

Na hiyo siku ikifika, maneno atakayoyasema, yasije tu kuwaliza. Yule bwana siyo mtu wa PC [political correctness].

Mdomo wake hauna chujio. Yatokayo huwa yanatoka hivyo hivyo yalivyo. Hayapitii chujio wala uhariri.

Siku ya yeye kulizungumzia hilo suala, naamini atakwaruza na kujeruhi hisia za watu wengi.

Hivyo kaeni mkao wa kupokea maneno ambayo hamkuyataraji.. msije tu mkasema Ngabu hakuwatonya!

Ni mimi wenu mtiifu katika ujenzi wa taifa,

Alhaji Ngabu.
Unaamini vipi kuwa anapita humu? Na je umejuaje kuwa mdomo wake hauna chujio we ni mkewe?
 
Mwaka jana ulikuwa unaleta thread zenye akili sana..mpaka mapema mwaka huu.baada ya hapo umekuwa ukileta thread zisizo na akili kabisa...tangu hili sakata la lissu kujeruhiwa umekuwa ukiandika sana na kutaka kumtetea bwana mkubwa kuwa hausiki..kwa kifupi watu wanajua kuwa anahusika..kwaaneno na matendo yake leo unamtenga vipi na tuhuma hizi..Binafsi nafaham gufuli anahusika..
 
Mwaka jana ulikuwa unaleta thread zenye akili sana..mpaka mapema mwaka huu.baada ya hapo umekuwa ukileta thread zisizo na akili kabisa...tangu hili sakata la lissu kujeruhiwa umekuwa ukiandika sana na kutaka kumtetea bwana mkubwa kuwa hausiki..kwa kifupi watu wanajua kuwa anahusika..kwaaneno na matendo yake leo unamtenga vipi na tuhuma hizi..Binafsi nafaham gufuli anahusika..

Una ushahidi kuwa Magufuli anahusika?
 
Kiukweli mpaka hapa tumesha zoea mambo yake ya kuona Nchi hii ni mail yake.2020 atatujua watanzania kuwa haturudii Makosa.
Unadhani kila mtu anawaza kama wewe? Sikupanga kupiga kura 2020 lakini nikiwepo duniani na tz nitampigia tena, for the second time.

Watz wengi ni watu hovyo sana.
 
2020 mnadhani atashindwa?

Ukweli wa mambo ni kwamba Magu ana grassroots support kubwa sana kuliko ambavyo inavyodaiwa humu JF.

Mtashangaa 2020 anashinda kwa asilimia 80 na hapo ndo mtapolia na kusaga meno.

Upinzani bado sana kuweza kuchukua dola kupitia sanduku la kura.

..jaribio la kumuua TL nadhani limebadilisha hayo mahesabu yako.

..MUNGU akimjalia TL akarudi mzima na akagombea kuna uwezekano mkubwa akapigiwa kura za HURUMA.

..WINGU JEUSI litakuwa likimfuata " mcha mungu" kila anapokwenda. Wananchi watasita kumpa kura kwasababu ataonekana ni mtu mshari na anayevuruga amani ya waTz.
 
Ila uliandika nini kuhusu weusi wenzio??? Wewe ndio unawehuka. Hujui real wala drama,fact wala opinion.
In short tia maji tia maji tu.[emoji57]
Ukishiba chukua na hela , nakutafutia usafiri wa kukurudisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom