NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,023
- 2,492
Asante, nitaufanyia kazi ushauri wako.
ila swala bado lipo pale pale, baada ya hayo yote then what shall I do? should I sacrifice my happiness so that my children are happy? or should I keep on searching till god say yes? totally confused.
Pole kaka. Msamehe mke wako ila usimrudie. Watoto wanaolelewa chini ya dari la wazinzi na wagomvi wanatoka wabaya kuliko wanaoishi kwa upweke, tena wa muda. Huwa napenda kusisitiza quality ya wazazi/walezi kuliko idadi ya wazazi au walezi. Umeshaulizwa mke angekufa ingekuwaje? Wapo wanaume wenzio wamefiwa au kuachwa na wake zao wakaachiwa watoto wadogo na hawajaoa wala kupeleka watoto boarding. Wengine nawafahamu ni wanachama hapa wanaweza kukupa uzoefu. Unachotakiwa ni kubadilisha maisha tu na kuvaa kofia mbili za ubaba na umama kama wanavyofanya single parents wengine. Manake ni kuwa kama ulikuwa ukitoka kazini unapitia kwa mama kamche kupata bia na ktm unaacha, unaenda moja kwa moja nuumbani kwanza.
That you should sacrifice your happiness for your children's happiness is out of question. It is an OBLIGATION. Maadam umeamua kuzaa basi lengo lako la kwanza, la pili na la tatu ni kuhakikisha ustawi wa watoto wako. Manake ni kuwa utalala njaa wewe wao wale, utatembea kwa mguu wao wasome, utaomba ruhusa kazini ukakae nao dada akiondoka......yaani watoto wako wanatakiwa kuwa kila kitu kwako ikiwa ni pamoja na kujikana mwenyewe ili wafurahi. Ila kujikana huko kusihusishe kuhatarisha uhai wako. Ukitaka utaweza tu. Ondoa kichwani kwako kuwa malezi ni taaluma ya wanawake tu. Maadam we si mnyama, hili unaliweza.
Sikushauri kupeleka watoto boarding, na ukilazimika basi liwe ni suluhisho la muda wakati we unajipanga. Omba ndugu yako, pia tafuta yaya mzuri, mpe mshahara mzuri watoto wako watakuwa vizuri bila shida. Cha msingi upatikane, usiwe baba wa wikiendi, au baba mtoa hela tu.
Hilo la kuoa kaka tuliza boli. Subiri maji yapoe. Sasa hivi tunaongelea watoto. Au unamaanisha unataka uoe ili upate mlezi wa watoto? Kama ndivyo hii si sababu nzuri ya kuoa kwa sasa. Utaishia kupata garasa bure. Mke anayeweza kukulelea watoto hata watano yupo, ila atapatikana ukiwa umetulia. Kama unahofia ukipata mwenye m/watoto mzigo utakuwa mkubwa basi utatafuta mke anayeingiza kipato, au wewe utafute hela zaidi. Kwani huyo dadako na housegirl nani alikuwa anawagharamia? Hofu tu. Sasa utampata wapi binti ambaye hajazaa umuoe halafu asizae. Labda umpate ambae anajijua ni mgumba. Sasa hivi ume-panick kila kuti unataka kushika. Kwa jinsi mambo yalivyo sasa hivi bado huna uwezo wa kutafuta mke bora. Yaani unataka kufanya kata mti panda mti kwenye jambo sensitiv namna hii? Hapo bado jeraha linauma unarukaruka. Settle issue ya watoto kwanza, ukimaliza sasa ndo uanze kuskilizia maumivu yako. Ukishapona utatafakari njia ya kuchukua kuelekea kwenye mahusiano na wanawake. Sijui we ni mtu wa aina gani kimtazamo kwa hiyo ni vigumu kukushauri. Kama unaamini sana katika dini basi utataka uoe haraka ili usizini. Hii inaweza kukudidimiza shimoni endapo utakosea kuchagua. Kama unaweza kukaa bila ngono muda mrefu jaribu kwa muda tu au jifunze. Kama huwezi tafuta mwanamke ila mambo yenu yaishie huko nje ya geti watoto wasione wala kusikia. Nitarudi baadae.