Sijui nianzie wapi?

Sijui nianzie wapi?

Watoto watatu ni wengi sana na ni vigumu kumpata mwanamke anayeweza kuwalea hao watoto wako watatu.
Hasa ukiangalia mioyo ya wanawake wetu hawa.

Kwani ni wanawake tu? Mwanaume anaweza kuoa mwanamke wa watoto watatu na kulea?
Hili sio la upande mmoja, wote linatuhusu
 
never never,
worse enough hajawahi hata siku moja kunieleza kua simridhishi haja zake, Kazi nilipiga vizuri hilo hata yeye alikiri.

What goes around comes around. Nahisi kuna siri au chimbuko la hili.

Pole sana
 
Fanya hivi...watt wakubwa peleka boarding Huyomdogo mpelekee mama ako kama yupo au kama ikishindikana mpmkeo amlee akfkifkia umr wa miaka minne chukua mtt wako....kuusu kurud yana nae ucthibut ata kuongezea mactrec Bure mwishoe akuue uache wtt wako kwan amekupunguzia aclmia za uaminf huwez kumu amin kama zaman tract me or not kwan nkwel Huyo mwanamke cmwaminf mwache na wakat watt hawapo utapata wakat mzur wa kutafuta mwanamke mwingine na kucpend nae...kuusu kuzaa nae ucogope unaweza kuzaa nae hata watt wawil ucogope watt nmubaraka kutoka kwamungu ivyo mungu mwenyewe atafungua njia mtalea2 na mkwapanga vizur mbona mtafurai wenyewe.....niiite Mrs engeneer...
 
Mbaya zaidi kiongozi, wakati wa purukushani hii, huyu wife alishawahi kuwakimbia hawa watoto sio chini ya mara tatu. alidiriki kuondoka nyumbani zaidi ya siku sita, hiki hasa ndo kilichonifanya nisiwaze hata mara moja kumwambia aondoke kwangu. haikua rahisi na ni mengi sana nimeyaona sijayaweka hapa. najuta kumfahamu huyu mwanamke

achana na huyo mwanamke mwisho wa siku atakuuwa kwa presha au ukimwi. kaa lea watoto peke yako, mungu akikujaalia upate mwanamke mwenye mtoto/watoto ambaye anajielewa, usiogope mzigo wa kulea maana malezi sana ni chakula, nguo, matibabu na vitu vingine vidogovidogo, kama baba yao anawasilisha matumizi na mama yao anafanya kazi wala haitakusumbua. Lakini huyo mwanamke wako ingekuwa mimi nasonga mbele siangalii nyuma.
 
hili la DNA mnataka jamaa afe haraka aisee

Imagine akienda akikuta sio wake anaweza kukutana na muumba siku si zake na inaonekana anawapenda watoto sana. Anaweza pia akaendelea kuwalea kama wake lakini mama yao akigundua amejua sio wake n analea tu, akaanza kuleta fujo na kuchukua watoto ili tu kumuumiza zaidi.
 
Mbaya zaidi kiongozi, wakati wa purukushani hii, huyu wife alishawahi kuwakimbia hawa watoto sio chini ya mara tatu. alidiriki kuondoka nyumbani zaidi ya siku sita, hiki hasa ndo kilichonifanya nisiwaze hata mara moja kumwambia aondoke kwangu. haikua rahisi na ni mengi sana nimeyaona sijayaweka hapa. najuta kumfahamu huyu mwanamke

Mmmh! Hilo jambo gumu lakini daktari wa mtu ni yeye mwenyewe.
 
Kosa tunalofanya wanaume ni kuwafukuza wake pindi tunapo tofautiana. Ushauri wangu wangu endapo umetofautiana na mwenz na unaona hamtoweza kuishi pamoja na tayari mna watoto ni bora mwanaume uondoke wewe utafute sehemu ya kujihifadhi na kutengeneza maisha huku watoto wako wakiendelea kuishi na mama yao kwenye nyumba yenu huku ukiwatembelea na kutoa msaada wa matumzo kwa watoto wako. Tatizo sisi watz tupo selfish na kwa staili hii watoto wa mtaani hawataisha katika jamii zetu ...

Ameshasema mama amewahi kuwakimbia watoto wake mwenyewe kwa muda unazidi siku sits sasa jiulize je huyu mama anaupenda kwa watoto? Baba angeondoka amwachie nyumba nini kingetokea? Labda angekua huru kuleta hawara zake, na angewaharibu watoto kisaikolojia.
 
mkuu unahakika watoto wote ni wako??
mkuu lengo hapa sio kujua watoto ni wangu au lah, ninachoamini mimi nikua hawa watoto wamezaliwa ndani ya nyumba yangu, nimewalea kwa gharama zangu, and thanks god they are very happy. hata kama nilidanganywa nakuhakikishia hakuna baba mbadala wa hawa watoto. kwahiyo issue ya kwenda kucheki DNA kwangu haitanisaidia kwani kwa vyovyote vile mi ndio nitabaki mlezi wa hawa watoto.
 
Mtoto wa Miezi 9 unachepuka? Pole kaka swala la kuoa kwa sasa huna haja ya kulifikiria
 
mkuu lengo hapa sio kujua watoto ni wangu au lah, ninachoamini mimi nikua hawa watoto wamezaliwa ndani ya nyumba yangu, nimewalea kwa gharama zangu, and thanks god they are very happy. hata kama nilidanganywa nakuhakikishia hakuna baba mbadala wa hawa watoto. kwahiyo issue ya kwenda kucheki DNA kwangu haitanisaidia kwani kwa vyovyote vile mi ndio nitabaki mlezi wa hawa watoto.

Mkuu nilikuwa nasubiri majibu ya hili swali ili nijue kwa kiasi wewe ni mtu wa namna gani.Una moyo wa kipekee sana aisee sijui kwanini huyo mwanamke hakuliona hilo.

Jitahidi ulee watoto wako kwa moyo wote watakupatia baraka nyingi sana.Waweza mtafuta dada wa kazi ukamlipa vizuri akakusaidia majukumu hapo nyumbani.

Usifikirie kumrudisha mwanamke yule hapo nyumbani.Ni mzinzi, na wazinzi hawana jema la kuwapa watoto wako.MUNGU alikuwa na maana yake kukuonyesha tabia za huyo mwanamke ili uzijue ujiokoe na wanao.

Kwa umri wako bado Una uwezo wa kupata mke mzuri tu baadae lakini usiwe na haraka.Nenda taratibu ili kosa la kuoa kurubembe lisijirudie.

Kila la heri.
 
Pole sana mkuu.... maana hata Avatar yako inaonesha unapenda sana familia.
 
Mbaya zaidi kiongozi, wakati wa purukushani hii, huyu wife alishawahi kuwakimbia hawa watoto sio chini ya mara tatu. alidiriki kuondoka nyumbani zaidi ya siku sita, hiki hasa ndo kilichonifanya nisiwaze hata mara moja kumwambia aondoke kwangu. haikua rahisi na ni mengi sana nimeyaona sijayaweka hapa. najuta kumfahamu huyu mwanamke

Achana nae atakuletea magonjwa huyo.
 
Wanajamvi, natumaini muwazima wa Afya,
Nimeona nije kwenu walau mujue yanayonisibu, sio kitu kipya hapana, ila kimeniweka kwenye mazingira magumu sana, japo najitahidi kufanya kila linalowezekana walau upepo huu upite.

kifupi ni hivi Mama wa Watoto wangu (Mke) nimeamua kumrudisha kwao baada ya kugundua hakua mwaminifu kwangu ie niligundua anamahusiano ya Kimapenzi na Watu wengine Nje ya Ndoa, nilifanya uchunguzi wa kina nakugundua uchafu huo, baada ya mikimiki ya hapa na pale alikiri mbele ya wazazi wake kua yote niliyowaeleza ni ukweli mtupu. baada ya mashauriano ya muda mrefu nilifikia uamuzi wa yeye aondoke kwangu. hili halikua gumu sana kuamua kwa kila kitu kilikua wazi

So issue yangu kubwa ni nini nifanye baada ya hapa, ukizingatia yafuatayo:

1. tuna watoto watatu , mdogo kabisa ana miezi 9

2. hawa watoto nawapenda sana na mpaka sasa naishi nao

3.mimi mwenyewe umri umekimbia am 35 yrs now

4. mama watoto kila siku anapiga simu kuomba msamaha( japo najua kabisa jasiri haachi asili)

5. najiuliza hata kama nikitaka kuoa tena, will it be fair to my children?

6. nina watoto 3, will it suit me kuoa mwanamke ambaye hajazaa? ataweza kulea kwa upendo hawa watoto?

7.je nikioa mwanamke mwenye mtoto/watoto tayari si atataka naye awalete waishi kwangu? huu mzigo utaniua

8.je ni haki niwapeleke boarding hawa watoto ili mi niishi peke yangu?
kiukweli nipo njia panda, tafadharini yeyote anayeweza nisaidia kimawazo nitashukuru
asanteni!

kahema!
pole sana! usibabaike hauko peke yako. kwanza tafita sababu kwa nini mkeo anaenda nje hill ndio swala la singi sababu inswezekana wewe ndio kidonda hivyo hata ikioa mwingine atafanya hiyo hiyo! pili, kuwapenda watoto wako kusikuzuie maisha yako ya baadae it all depends on how you plan it especially on choosing your next spouse but since you have three children already, I advice you to go for a woman who has one child and is also desperate with life like you, you can cope. But But I warn you this shouldn't be your fore most thought or idea, first scrutinize the innermost relationship with your wife if at you all find you find yourself weak somewhere don't dare attempting any act forward other than reconciling with your wife because it is said A DEVIL YOU KNOW IS BETTER THAN AN ANGEL YOU DONT KNOW.nitafute ritchelous@gmaii.com yaliishanipata hayo am 64 now mwisho kabisa nimeoa Guyana.
 
kwa ajili ya watoto msamehe si kwa ajili ya dhambi aliyokutendea bali kwa ajili malezi ya hao watoto.
mrudishe umfanye kama mlezi wa hao watoto kwa sababu hata ukiwapeleka boarding angali wakijua mama yao hampo pamoja hawatatulia kwenye masomo yao.
we mrudishe alafu kwa sababu hautakuwa na mapenzi naye kama zamani tafuta kipozeo ambaye ukitoka kwake ukifika nyumbani hautamchukia tena mkeo kwa kuwa ngoma itakuwa droo.
 
Kwanza nenda kapime huu ugonjwa wa Kisasa, then vuta pumzi za kutosha kulea wanao na mwisho usifikirie kumrudisha mkeo kwa sasa na pia usiwaze kuoa kwa kipindi kifupi kijacho kwani wapo na utawapata au pengine baada ya tafakari na tafakuri ukamrudia mkeo. Kama una uhakika kakucheat na vidume V3 ni wazo huyo mkeo haridhiki hata kama mngemuoa wanaume w2 na aina hii ya wanawake na hata wanaume ni pasua kichwa kwani hata ufanye juhudi kiasi gani starehe yake ni kukutana na wanaume tofauti tofauti na siyo kuridhishwa. Anza hatua sasa na hutoijutia safari yako ila ukigeuka kurudi nyuma nachelea kusema hata usalama wako na wanao uwapendae utakua shakani. Pole kwa masaibu na Happy New Year of 2015.
 
Kahema nimesoma tena thread yako pamoja na comments za watu na wewe ulivyojibu. Nimegundua kuna tatizo kubwa nyuma yenu ambalo hujafunguka. usipofunguka hata kwa kifupi, itakua ngumu kupata ushauri muafaka. na withdraw kwa sasa comments zangu za mwanzo za nini ufanye. Jaribu kufunguka kidogo ili tukupe ushauri unaostahili. Sipati picha mke kukimbia watoto wake for 6 days...!!! what went wrong, hebu funguka hapa na utuambie mlikutana wapi katika mazingira gani. Kingine usimlaumu sana, duniani hapa kuna mambo mengi, kuna mwanamke namfahamu alimkimbia mume wake na watoto watatu, mdogo akiwa na 9 months, akaenda kwa mwanamme mwingine, huko akazaa watoto wawili. hapa ninapoandika comments hizi, alishaachana na huyo mwanamme wa pili sasa hivi ni teja (mla unga na bangi) wa kupindukia. Ni mama mwenye degree yake huyu, above 40 lakini hapa ndipo alipoishia. watoto wake wote kaacha kwa baba zao. familia yake inadai aliondoka kimazingara kwa mume wa mwanzo. sina hakika na hili. hainingii akilini mwanamke kupotea na kuacha watoto watatu. mimi hata mmoja simuachi no matter what... Funguka kaka yangu, hapa ndio penyewe kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom