Jagarld
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 2,515
- 3,042
Habari zenu ndugu wanajf wenzangu,hamjambo?
Kuna jambo moja linanitesa na kuninyima raha ndugu zangu,ningependa kuliweka wazi kwenu ili mwenye msaada wake aweze kunisaidia.
Nimekuwa na urafiki wa kawaida na dada mmoja ambaye mme wake ni boss wa kampuni moja inayojishughulisha na mambo ya kusafirisha watalii na huyu dada nae ana cheo kikubwa kwenye hii kampuni yao,urafiki wetu ulianza mwaka mmoja wakati nafanya kazi serikalini baadae akaniambia kwanini nisihamie kwenye kampuni yao na kunipa ahadi kibao,alinitaka nimpe nakala ya vyeti vyangu nami kweli nikafanya hivo,baada ya wiki tatu nikaitwa kufanya interview,siku ya interview nilihudhuria akanipigia simu niende ofisini kwake ambako tulianza kupiga stori na interview nikaambiwa imeahirishwa mpaka nitakapojulishwa.
Baada ya wiki mbili nilipokea barua ya kuitwa kazini na nikaenda tukaelewana mshahara na mambo mengine yakawa safi ikanibidi nirudi ofisini na kuandika barua ya kuacha kazi ndani ya masaa 24.
Baada ya wiki moja nikaanza kazi rasmi kwa mwajiri wangu mpya,kwa muda wa miezi minne kazi imekuwa inaenda vizuri lakini mke wake boss akaanza kama matani anataka zawadi,nikamwambia poa zawadi tu utapata wala usijali huku tunataniana.
Kuanzia wiki iliyopita amekuwa mtu wa kupiga simu muda wowote usiku baada ya boss kusafiri,anasema ametokea eti kunipenda tangu siku ya kwanza tunakutana naye ndo maana kafanya kila njia niwe karibu naye,anadai atanifanyia vitu vikubwa zaidi ata ambavyo sijafikiria maishani nikikubali kufanya na kama nitaonesha umasikini jeuri yeye atajua atakavofanya japo anadai ananipenda ana ananihurumia mwisho wangu utakuwa mbaya nikikataa,mda huu ninapoandika hii niponyumbani baada ya kuomba ruhusa kuwa naumwa.
Ndugu zangu nifanyaje?