Sijawahi kupanda ndege...Nielimisheni

Sijawahi kupanda ndege...Nielimisheni

Mkifika kwenye mataa anagani kutakuwa na jamu ya kufa mtu kwa zaidi ya saa nzima mtakuwa mmeganda hewani kusubili trafiki aruhusu upande wenu , tena usiombe mkutane na boda boda , we mbona utajuta kupita njia hiyo ya angani. ila usisahahu kubeba mapanki na ugali wa udaga kwajili ya msosi njiani, safari njema abandugu.
 
Kueni serious basi nyie watu wa daslamu. Najua mnajua vitu vingi sana but wachoyo sana kuelimishana. Hua mnamaana gani kusema mjini shule kama majibu mnayonipa ndio haya ya kisembesembe?..Mnajibu utumbo utumbo tu kama Mwigulu Nchembe. Mnnfyuuuuusss

Basi ngoja nikusaidie, naona wengi hapo juu wanakusaidia na madongo juu.
Mie mwenyewe sijawahi kupanda, ila nakupa uzoefu kutoka na stori za kwenye kijiwe chetu cha kahawa.
  1. Andaa begi lako mwenyewe unapotaka kusafiri na ndege, usikubali mtu akuandalie, hata kama unamwanini sana.
  2. Usibebe silaha kwenye begi lako (pinde, mishale, mikuki, bastola, visu, wembe nk) kwani watakupokonya ukifika uwanja wa ndege. Pia usibebe vimiminika (mafuta ya jamii ya lotion nk).
  3. Ukifika uwanjani mizigo yako itakaguliwa kwenye skana (scanner), ila kama unaondokea uwanja wa Mwanza sometimes skana yao mbovu, utakaguliwa kwa mikono tu na wanoko waliopo hapo.
  4. Kwa ndege zinazosafiri ndani ya nchi, muda wa kuripoti ni dk 45 kabla ndege haijapaa, na za kimataifa ni saa 2 kabla ndege haijapa
  5. Mambo mengine yote utaelekezwa ukifika uwanjani
Kila la kheri
 
1.jiandae kukumbana na jamu ya hatari mtapokuwa mmefika junction ya pembeni kutokana na msafara wa mnene fulani.

2. pia jiandae kupishana na boda boda nyingi angani ambzo usipokuwa makini zinaweza wapiga pasi.

3. pia ukipanda ndege usipende kukaa siti ya dirishani kwani unaweza kwapuliwa saa yako na vibaka.
ukitaka msaada unaweza shuhwa hata kabla ya kufika uwanjani yaani wankuacha kituo cha msaada kama ulivyoomba.

4.Itakubidi ubebe kadumu ka lita 5 ya ulanzi au ugimbi bila kusahau kale "ka-mfugo ketu...wuwuwuwuwuuu" kwani hawagawi kinywaji kama soda kama wanavyofanya kwenye mabasi.

5. Ng'an'ania kiti kwa nguvu zako zote pindi mtapofika kwenye kona kali na miteremko mikali sana kama ya senkenke.

6. ukitaka kupuga/ja...mba kwenye ndege we jiachie tu tena kwa nguvu au kile cha kimya kimya coz kwenye ndege hakinuki wala sauti kusikika kama kwenye dala dala.

Ni hayo kwa sasa , baadae ntakuongezea mengine zaidi ili usije pata bugdha utapokuwa njiani. Adios amigosi.
 
Kaka nakushukuru kwa jibu la busara. Toka nimejiunga humu. Hili ndilo Jibu zuri na la kwanza kuliona. Kiufupi...kama ungekua unagombea. Ningekupa kura yangu. Asante sana.
 
Wengine huenda tunamcheka lkn hatujawahi panda ila kimya kimya tu:

Ngosha pia utakuta screen ya movie, tracker na cd player mbele ya kiti chako: hasa ukipanda ndege za masafa kama Dubai-Brisbane 15hrs flight. Kwa daladala za hapa Tz utapewa juic azam na bagia.

Usijali hakuna aliezaliwa anajua kila kitu!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1378984426.123774.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1378984426.123774.jpg
    81.7 KB · Views: 328
  • ImageUploadedByJamiiForums1378984499.442362.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1378984499.442362.jpg
    110.7 KB · Views: 253
Mnaudhi sana humu. Mavi kabisa....mmnfyuuuuuuussss
Hapana bhana wako sahihi kabisa ,wanajibu kwa kuzingatia umri wako!yaani wewe unafikiri kupanda ndege ni starehe tu kiasi kwamba una hamu ya kupanda? pia kama unahamu hivyo changa mapene yako jitie japo kwenye coastal /zan air /auric air au precission uje zenji kunitembelea na nahisi hata fast ferry hujapanda,hii nitakupa offer ya ticket ya kurudi unasemaje mkwimbakwimba?
 
[h=1]Maelekezo I: Unayotakiwa kufanya ukisafiri na ndege kwa mara ya kwanza[/h][h=1]Ikiwa ni mara yako ya kwanza kusafiri kwa ndege unaweza kuona ugumu na pengine kuwa na shaka juu ya usafiri wa anga kutokana na kukosa taarifa za kutosha.
Nalazimika kutoa maelekezo haya kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kukupatia wakati wa safari yako hasa kutokana na watu wengi utakaokutana nao kwenye ndege kuwa na uzoefu wa kusafiri mara kwa mara na kufikiri kila aliyemo ndani naye ni mzoefu.
Mambo ya muhimu kuzingatia wakati unapanga kusafiri kwa ndege ni pamoja na wakati wa kukata tiketi, wakati wa kupaki mizigo yako, nini cha kufanya unapofika uwanja wa ndege, uende wapi, vitu vya kuzingatia wakati wa safari, nanma ya kushughulikia uunganishaji wa safari (kama unasafiri masafa marefu na unahitaji kuunganisha ndege nyingine), wapi pa kuchukua mizigo yako ukifika uendako na kujua swala la usalama wako na mizigo yako.
Wala hupaswi kupaniki, japo kuwa kusafiri kwa ndege kunaweza kukuchanganya kwa mara ya kwanza lakini ukishakuwa mzoefu utaona kila kitu mteremko na kuenjoy safari zako zote.
Sasa wengi wetu huwa hatutaki kujulikana kama ni ma-first time flyers kwa kuogopa kuchekwa, lakini tambua kuwa kila unayemuona kwenye ndege inaweza kuwa ni mara yake ya kwanza kusafiri na ndege hata kama sio lakini naye alikuwa first time flyer wakati anaanza kutumia usafiri huo, kwa hiyo usisite kuuliza wahudumu au hata msafiri mwenzako kwa msaada zaidi.
Baada ya utangulizi huo sasa tuyaone maeneo muhimu wakati wa safari yako ya ndege;
[/h][h=2]Tiketi; Kuna aina mbili za tiketi za ndege, tiketi za mtandao za elektroniki (e-ticket) na zile tiketi za kawaida (traditional tickets) hata hivyo mashirika mengi ya ndege siku hzi yanatoa sana tiketi za mtandaoni kutoka na kuwepo mfumo wa kulipa kwa njia ya mtandao.[/h][h=1]Ili kupata ticketi yako unatakiwa kuwa na kitambulisho kama vile, leseni ya udereva, kadi ya mpiga kura (kwa wasafiri wa ndani ya nchi) na pasi ya kusafiria (passport kwa wasafiri wanaosafiri nje ya nchi). Njia za kufanya malipo ya tiketi yako ni pamoja na kadi za benki (visa card and master card), kwa Tanzania pia unaweza kulipa kwa kutumia M-pesa, Tigo-Pesa, Airtel-Money na Ezzy Money.
[/h][h=3]Unachopaswa kujua wakati unakata tiketi[/h][h=3]Kuna aina tatu ya madaraja ya tiketi; Economy, Business na First Class na hata haya madaraja pia yamegawanyika kwa namna yake lakini kukibwa ni kwamba kila daraja lina gharama zake kulingana na huduma zinazotolewa kwa abiria akiwa safarini.[/h][h=3]Economy; hili ni daraja la chini na hivyo gharama zake za nauli ni ndogo na mara nyingi huduma zake ndani ya ndege zinajumuisha vitu vichache pia[/h][h=3]Business and First Class; Haya ni madaraja ya juu ambayo gharama zake za nauli ni kubwa na huduma zake ni nzuri zaidi kwa abiria, ni vizuri kuuliza ni mambo gani utapata ukikata tiketi ya aina hii ili kuona uhalali wa pesa yako.[/h][h=3]Una mahitaji maalumu?[/h][h=1]Endapo wewe ni mlemvu, unasafiri na watoto na nk, inashauriwa kutoa taarifa hizi wakati ukikata tiketi ili usije kupata shida wakati wa safari yako ukifika.
[/h][h=3]Unahitaji Chakula maalumu?[/h][h=1]Kama tiketi yako inaonyesha kuwa utapata na chakula wakati wa safari yako unahitaji kutoa taarifa ya aina ya chakula unachokula, maana kuna wengine hawali nyama (vegiterians) toa taarifa hizo wakati ukifanya booking ya tiketi yako. Zingatia kuwa sio kila ndge hutoa huduma ya chakula mashirika mengine hayafanyi hivyo.
[/h][h=3]Unapenda kukaa siti ya dirishani?[/h][h=1]Ni kawaida unaweza kuchagua nafasi ya dirishani (kama kuna nafasi), mara nyingi mashirika mengi ya ndege hukupa nafasi ya kuchagua siti wakati wa kukata tiketi yako. Siti za dirishani ni nzuri sana kwa watu wanaosafiri kwa mara ya kwanza kwa maana huwapa fursa ya kuona nje ya ndege lakini wale watu warefu sana ni vyema kukata tiketi ya kwenye korido ili waweze kukaa vizuri.
[/h][h=3]Ratiba[/h][h=1]Iwe unanuanua tiketi yako kwenye ofisi moja kwa moja au kwa njia ya mtandao, omba kupatiwa ratiba ya safari yako, kuna taarifa ndogo lakini muhimu ambazo watu huwa wanajisahau na baade kukutwa na majanga, lazima ujue, ndege inaondokea uwanja gani, muda, reservation number, uunganishaji wa ndege, na kadhalika (mara nyingi e-tickets inakuwa na taarifa hizi zote hivyo ni vizuri kuisoma).
Itaendelea………..
Chanzo: tabianchiblog
[/h]
 
Kwa kuwa umetokea Mwanza jihadhari kuna jamaa mmoja aliuziwa pamba wakiwa angani.
 
Basi ngoja nikusaidie, naona wengi hapo juu wanakusaidia na madongo juu.
Mie mwenyewe sijawahi kupanda, ila nakupa uzoefu kutoka na stori za pkwenye kijiwe chetu cha kahawa.
  1. Andaa begi lako mwenyewe unapotaka kusafiri na ndege, usikubali mtu akuandalie, hata kama unamwanini sana.
  2. Usibebe silaha kwenye begi lako (pinde, mishale, mikuki, bastola, visu, wembe nk) kwani watakupokonya ukifika uwanja wa ndege. Pia usibebe vimiminika (mafuta ya jamii ya lotion nk).
  3. Ukifika uwanjani mizigo yako itakaguliwa kwenye skana (scanner), ila kama unaondokea uwanja wa Mwanza sometimes skana yao mbovu, utakaguliwa kwa mikono tu na wanoko waliopo hapo.
  4. Kwa ndege zinazosafiri ndani ya nchi, muda wa kuripoti ni dk 45 kabla ndege haijapaa, na za kimataifa ni saa 2 kabla ndege haijapa
  5. Mambo mengine yote utaelekezwa ukifika uwanjani
Kila la kheri

Bastola wanaruhusu ukifika unadeclear-na receipt za kuonyesha umiliki.dk 45 Sikh hizi wanakuwa wameshafunga check in tenakama hawa nafuu' nafuu'ndo watu wanalia sana
 
Kueni serious basi nyie watu wa daslamu. Najua mnajua vitu vingi sana but wachoyo sana kuelimishana. Hua mnamaana gani kusema mjini shule kama majibu mnayonipa ndio haya ya kisembesembe?..Mnajibu utumbo utumbo tu kama Mwigulu Nchembe. Mnnfyuuuuusss

Ndege anapandwa na ndege mwenzake, kuku na bata hivyohivyo. Kuna jamaa wachache wamebambwa wakipanda mbuzi au ng'ombe. Wewe unataka kupanda ndege, jiangalie!
 
Hakikisha ndege unayopanda ina 4WD,maana hizi mvua za vuli full majanga.
 
Mpaka sasa...sijapata jibu lolote. ..watu wa jf mnaudhi wakati mwingine..daah. Mnajibu mavimavi tu

Mlolongo wote nadhan unaujua, ila sharti ni kuwa ukishapanda mkaanza safari usijechungulia chini, vinginevyo utawaangusha na wenzio na kudondokea paa za watu, ushauri tu ukataka acha.
 
Kuna uzi humu wa mwaka jana kama sikosei. Mwenzio aliuliza swali kama hili alikuwa anajiandaa kutoka Mwanza kwenda Dar .Majibu aliyapata, nikikumbuka nacheka sana. Utafute uzi huo.

yaani nikikumbuka mjibu aliyopewa yule mdau nilikoma kuomba msaada hapa jf,lakini awe mpole asaidike.
 
Back
Top Bottom