Undani kuhusu ajali ya Ndege ya Precision Air, Kudondoka kwake hadi hatua za Uokozi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Watanzania 18 na Mwingereza mmoja, jana walishindwa kuingia mini Bukoba, wakiwa hai baada ya maisha yao kukatizwa na ajali ya ndege ilivowatoa Dar es Salaam wakiwa salama.

Hawa ni miongoni mwa abiria 43 walioelezwa kuwamo ndani ya ndege aina ya ATR42-500 mali ya Shirika la Precision ilivolazimika kutua ndani ya Ziwa Victoria, mita 150 kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Ndege hiyo yenye usajili 5H-PWE namba PW 494 ilivoanza safari vake kuelekea Bukoba alfajiri ya Jumapili, Novemba 6, mwaka huu, ilingia anga la mi huo pembezoni mwa Ziwa Victoria, lakini rubani wake, Buruani Rubaga alishindwa kutua uwanjani kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.

Mashuhuda waliokuwamo ndani ya ndege hiyo wamelieleza Pambazuko kuwa Rubani Rubaga, akisaidiwa na rubani msaidizi, Peter Odhiambo, alilazimika kuwatangazia abiria kwamba hataweza kutua uwanjani hapo kwa kuwa hali ya hewa kuwa mbaya.

Anga la Bukoba - hasa eneo la uwanja wa ndege jana lilionekana kugubikwa na ukungu na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha tangu alfajiri ya siku hiyo.

Hata hivyo, baadaye rubani hiyo, inaelezwa aliamua kutumia uzoefu wake kutaka kutua uwanjani hapo kupitia eneo la Nshambya ambapo kulikuwa na upepo mkali, hali iliyosababisha kushindwa kuimudu na hatimaye kutua majini.

Kawaida, ndege hiyo hutua kupitia eneo la Musira ambalo kwa jana lilikuwa na hali mbaya ya hewa - kutanda kwa ukungu mzito.

Baada ya ndege hiyo kulazimika kutua majini, saa 2.53 asubuhi, wavuvi waliokuwa ziwani, ndiyo walikuwa wa kwanza kufika eneo ilipotua ndege hiyo, ikiwa imezama sehemu kubwa ya mbele na kubakiza eneo la nyuma likionekana juu ya maji. Ndege hiyo ilitarajiwa kutua saa 2.30 asubuhi na kuondoka kurejea Dar es Salaam kupitia Mwanza saa 2.50 asubuhi.

Mmoja wa waandishi wa Pambazuko aliyekuwapo uwanjani hapo, alishuhudia maji mengi yakiruka, mfano wa wimbi kubwa la maji, kabla ya kubaini kuwa ni ndege alivotarajia kupanda kurejea Dares Salaam, ndiyo imetua ziwani.

Shughuli za uokozi zaanza
Baaada ya "kishindo" hicho ndani ya maji, takribani dakika 27, gari la Zimamoto lililokuwa uwaniani hapo lilionekana likiondoka mahali linapoegeshwa huku likiwasha vimwekamweka na likipiga king'ora na ndipo kuwashtua wafanyakazi uwaniani hapo "waliovamia" uwania na kuanza kulia kwa kelele.

Pambazuko liliwashuhudia wafanyakazi hao wakipiga yowe na kulia na ndipo idadi kubwa va watumishi wa uwanja huo walipoungana nao kukimbia wakielekea eneo la tukio.

Ndege hiyo ya abiria ilitua ndani ya ziwa hilo, mita takribani 180 kutoka kwenye barabara ya kutua.

Baadaye idadi ya wavuvi iliongezeka huku ndege ikiwa imezima na ghafla, saa 3.11 asubuhi, mlango wa nyuma wa ndege ulifunguka na wavuvi waliokuwa jirani walingia ndani ya ndege hiyo kuanza uokozi.

Dakika 13 baadaye, askari wa Zimamoto na mwanajeshi mmoja alivetaijwa kuwa mtumishi wa uwanja huo, mwenye uzoefu wa kuogelea, aliingia ndani ya ndege hiyo na kuongeza kasi ya kuokoa idadi va watu waliokuwa wakisukumwa kutoka ndani ya ndege hiyo.

Pambazuko lilishuhudia wanajeshi wachache mgambo wakiingia uwanjani hapo saa 3.27 wakikimbia kuelekea ukingoni mwa ziwa kwa ajili ya kuongeza nguvu za kuokoa, hata hivyo, hawa hakuna aliyekwea mtumbwi ili kwenda kuingia ndani ya ndege kusaidia uokozi.

Hawa walifika wakiwa na mavazi vao ya kazi, magwanda bila vifaa vya uokozi ndani ya maji. Hata hivyo, baadaye ilikuja timu ya wanajeshi wakiwa na vifaa vya kuogolea na kwenda kuongeza kasi ya kutoa abiria ndani ya ndege hiyo wakisaidiana na wavuvi.

Kazi ya kuokoa yasitishwa
Ilipofika saa 5.21 asubuhi, wanajeshi wachache na wavuvi waliokuwamo ndani ya ndege wakipambana kuokoa maisha, walioanza kutoka ndani, huku nyuso zao zikionekana kukata tamaa na 'kuvaa' sura zenve huzuni.

Mmoja wao amezungumza na Pambazuko na kueleza kwamba walilazimika kutoka ndani kwa kuwa maji yaliongezeka, hivyo kuhofia madhara zaidi na wao kuiinusuru kwa kuwa abiria kadhaa waliwaona wamefariki dunia tayari.

"Maji yaliongezeka, waokozi wengi tulikuwa tunatembea wakati maji yalikuwa viunoni, lakini baadaye yakafika vifuani, na hapo tukaona heri kupambana kuokoa tukiwa nie ya ndege maana kubaki ndani kungeweza kuleta maafa zaidi," ameliambia Pambazuko mmoja wa waokoaji aliyekatataa kutajwa jina.

Shuhuda huyo na mwokozi wa abiria anaeleza kuwa ndani ya ndege, abiria waliokuwa wamefariki walikutwa wamefunga mikanda, huku wengi wakiwa wanavuja damu kwenye mapaji ya uso.

"Inaonekana abiria wengi walipata majeraha vichwani na wengine kubainika wamevunjika shingo, hawa tulioona wamefariki, tuliwaacha kwanza na kupambana na wale waliokuwa wakipumua, anaongeza muokoaii mwingine, Geofrey Mshemwa.

Aokolewa na kukimbia
Abiria mmoja, mongoni mwa hao 26 waliookolewa, alikimbia mara baada va kufikishwa nchi kavu na hakuweza kukamatwa, licha ya kufuatiliwa na wana usalama wa uwanja huo.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa abiria huyo mwanaume, huenda alichanganyikiwa na asijue alilokuwa akilifanya kutokana na mshtuko wa ajali hiyo.

Shuhuda mwingine anena
Mmoia wa mashuhuda aliyekubali kutajwa jina lake ni Richard Komba, ambaye aliliambia Pambazuko kwamba ndege waliyopada iliondoka Dar es Salaam saa 6.15 alfajiri jana, ikiwa ni dakika 15 kuchelewa kuliko ilivyopangwa.

Amesema kuwa safari yao ya kwenda Mwanza kupitia Bukoba haikuwa na msukosuko angani, lakini baadaye walihisi kuwepo kwa hali maya ya hewa walipokuwa wakikaribia Bukoba kwani ndege ilionekana kuyumba na kusokwasokwa na nguvu ya upepo.

"Tulipokaribia uwanja wa ndege wa Bukoba rubani alitufahamisha kuwa ameshindwa kutua na alikuwa anaendelea kuna uwezekana wa kutua salama ama kuelekea Mwanza kwanza, lakini inaonekana alishindwa kumudu hali ya hewa na ghafla tukajikuta tumetumbukia majini," amesema.

Komba amesema mara baada va kutua kwa kishindo majini, abiria walionekana kuchanganyikiwa, baadhi wakiwa wanapiga kelele na wengine wakionekana kupambana kutafuta mahali pa kujiokoa na ghafla mango wa nyuma ulifunguliwa na ndipo hekaheka za kujiokoa zikashika kasi, na muda mfupi baadaye aliona watu wakiingia kuwaokoa.

Waliookolewa watajwa
Majina ya watu waliookolewa yametajwa na kwamba wengi walipelekwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Wapo waliorhusiwa kuondoka jana jioni na wengine kubaki kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Hawa ni pamoja na Ragi Samwel Invoma (28) mkazi wa Dares Salaam, Rausath Hassan (26) mkazi wa Bukoba, Anna May Mitabalo (40) mkazi wa wilaya ya Karagwe, Kagera, Dkt. Felix Otieno (37) mkazi wa Bunda, Mara, Shamiru Ismail (34) mkazi wa Bukoba, Protas Mussa (38) mkazi wa Ngara, Kagera, Amos Skoth (38) makazi wa Mwanza, Grace Rugambwa (67) mkazi a Bukoba na Amina Abdallah Karwandira (62) mkazi wa Bukoba.

Wengine ni Revina Theonest Rutinda (29) mkazi wa Geita, Emili Victor Mwesiga, Jesca Julius Titus (27) mkazi wa Dar es Salaam, Zang Lin (30) - Mchina, Richard Komba (42), Emmanuel Amani (28) mkazi wa Mwanza, Nikson Jackson Kawiche (35) mkazi wa Dar es Salaam, Saleh Omary (46), Edwin Bitegeko (33) mkazi wa Dares Salaam, Eva Dickson Mcharo (38) mkazi wa Sengerema, Mwanza, Josephine Joseph Mwakisambwa (34)mkazi wa Dar es Salaam, Theodora Stanslays Mpesha (46) na oseph Laurence Mbago (57) mkazi wa Dares Salaam.

Wahudumu walionusurika katika ajali hiyo ni wawili; Brenda Selvuli Temba (23) mkazi wa Dar es Salaam na Lvdia Ibrahim Ramadhan (25) nave mkazi wa Dar es Salaam.

Waliofariki dunia watajwa
Abiria ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na Atulinde Biteya, Aneth Biteya, Neema Faraja, Hanifa Hamza, Aneth Kaaya, Victor Laurean, Said Malat Lyangana, Iman Paul, Faraji Yusuph, Lin Zhang, Sauli Epimark, 'Zacharia Mlacha, Eunice Ndirangu, Mtani Njegere, Zaituni Shillah na Dkt. Alice Simwinga.

Rubani aliyepoteza maisha ni Buruani Rubaga na msaidizi wake Peter Odhiambo.

Majaliwa kuaga mili leo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliwasili mjini Bukoba jana jioni, na kutembelea manusura waliopelekwa hospitali ya Bukoba, leo anatarajia kuungana na Watanzania katika shughuli ya kuaga mili ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Shughuli za kuaga mili hiyo zitafanyika katika Uwanja wa Kaitaba na wananchi wameombwa kuitokeza kwa wingi kuaga marehemu.

Chanzo: Pambazuko
 
bado nauliza swali, kama Rubani angeamua kurudi Mwanza ama kutua uwanja wa Magufuli Chato au Kahama asubiri hali ya hewa itengemae hilo lisingewezekana?

kuna muda sisi tulitoka Mza - Ngara, hali ya hewa ikawa mbaya balaa Ngara, ikabidi turudi Mwanza - baada ya masaa 3 tukarudi tena - ni gharama ila unaepuka ku risk.
 
bado nauliza swali, kama Rubani angeamua kurudi Mwanza ama kutua uwanja wa Magufuli Chato au Kahama asubiri hali ya hewa itengemae hilo lisingewezekana?

kuna muda sisi tulitoka Mza - Ngara, hali ya hewa ikawa mbaya balaa Ngara, ikabidi turudi Mwanza - baada ya masaa 3 tukarudi tena - ni gharama ila unaepuka ku risk.
Rubani alitaka kufanya hivyo pia ikashindikana kwasababu ya hali ya hewa ilikua mbaya,soma vizuri.
 
bado nauliza swali, kama Rubani angeamua kurudi Mwanza ama kutua uwanja wa Magufuli Chato au Kahama asubiri hali ya hewa itengemae hilo lisingewezekana?

kuna muda sisi tulitoka Mza - Ngara, hali ya hewa ikawa mbaya balaa Ngara, ikabidi turudi Mwanza - baada ya masaa 3 tukarudi tena - ni gharama ila unaepuka ku risk.
Mkuu tukiacha na yote, uzembe, hili na lile kuhusu ajali nzima.....

Siku ya kufariki ikifika sababu lazima isikosekane, iwe uzembe, ugonjwa au lolote, lazima kifo kinakuwa na sababu.

Kwa hiyo pamoja na yote yaliyotokea Kwa ndugu zetu, huenda siku Yao ilifika, ndio maana wenye ahadi ya kufariki Jana walifariki, na waliokuwa ahadi Bado walifanikiwa kutoka.

Mungu awapumzishe wanapostahili.
 
Uwezo wa CCM ndiyo umeishia hapo. Kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Kaitaba. Uwajibikaji ni zero!
IMG-20221107-WA0033.jpg


RIP Ndugu zetu
 
Kweli ukiambiwa changanya na zako! Binafsi nimeamua kupuuza kila taarifa ya ajali hii ilivyo tokea zaidi ya kuanzia kwenye uokozi tuliyo shuhudia wenyewe, ila nyuma ya hapo nasubiri majibu ya BLACK BOX maana nyie wengine mnatuchanganya kila mtu ana story yake.

Kuna uzi mwingine unaelezea ajali hii tangu ndege haijaingia ziwani na sababu ya ajali sio hali ya hewa kama ww unavyo tupanga hapa

Siasa mbaya sana kwenye vitu kama hivi hatuitaji hoja tunataka facts bhasi.
 
Sasa ndo tumepata maelezo mazuri, yenye kuonesha kilichotokea
Kuna maelezo mengine mtaa wa pili huko nayo ukikutana nayo ni kama ya ukweli kuliko haya 2subiri BLACK BOX tu maana ina kila kitu mpaka sound record ya sinema zima
 
Mkuu tukiacha na yote, uzembe, hili na lile kuhusu ajali nzima.....

Siku ya kufariki ikifika sababu lazima isikosekane, iwe uzembe, ugonjwa au lolote, lazima kifo kinakuwa na sababu.

Kwa hiyo pamoja na yote yaliyotokea Kwa ndugu zetu, huenda siku Yao ilifika, ndio maana wenye ahadi ya kufariki Jana walifariki, na waliokuwa ahadi Bado walifanikiwa kutoka.

Mungu awapumzishe wanapostahili.
ni kweli kwa sisi waafrica tunajua neno moja tu la kujipa faraja kwamba "bwana ametwaa" ila kusema ukweli for the better future huwa ni wagumu sana, hapa ndipo wenzetu weupe wanapotuzidi.

RIP, na wanafamilia Mungu awape nguvu.
 
Kuna maelezo mengine mtaa wa pili huko nayo ukikutana nayo ni kama ya ukweli kuliko haya 2subiri BLACK BOX tu maana ina kila kitu mpaka sound record ya sinema zima
Lazima alituma signal ya Mayday baada ya kuona kaishindwa ndege, Mayday call lengo lake ni uokozi
 
Kweli ukiambiwa changanya na zako! Binafsi nimeamua kupuuza kila taarifa ya ajali hii ilivyo tokea zaidi ya kuanzia kwenye uokozi tuliyo shuhudia wenyewe, ila nyuma ya hapo nasubiri majibu ya BLACK BOX maana nyie wengine mnatuchanganya kila mtu ana story yake.

Kuna uzi mwingine unaelezea ajali hii tangu ndege haijaingia ziwani na sababu ya ajali sio hali ya hewa kama ww unavyo tupanga hapa

Siasa mbaya sana kwenye vitu kama hivi hatuitaji hoja tunataka facts bhasi.
Cha kushangaza picha zinawaumbua kuhusu Hali ya hewa maana tungeona tu
 
Lazima alituma signal ya Mayday baada ya kuona kaishindwa ndege, Mayday call lengo lake ni uokozi
Kuna uzi unaelezea sababu ya ajali sio hali ya hewa bali ni tairi zilishindwa kufungu ana kutaka maelekezo akalazimika kuzurula huku akingoja maelekezo, anadai baada ya kuzunguka mda mrefu akahofia wese kukata ikabidi wamuelekeze akatue ziwani timu ya uokozi ipo tayari inamfuata, ndugu yetu akajiamini akaenda kuchumpa na maji yalivyo shida ikawa imefika car wash! Kilichofuata mpaka wanatua wote walikua salama na bado walikua wanawasiliana wakati tayari wakiwa salama salmini yaliyo fuata wote tumeshuhudia ss na huyu ndugu yetu anatuambia tatizo lilikua hali ya hewa wapi na wapi
 
Back
Top Bottom