Musa alikuwa na kigugumizi na karibu yake alisogea haruni kwa hiyo MUNGU alipozungumza na musa kwa maelekezo kwa wana wa Israel mMUNGU huyo huyo alimwambia musa mwambie Haruni awaambie wana wa Israel maneno hayo na huo ulikuwa mpango wa MUNGU na ndiyo maana kuhani mkuu wa kwanza alikuwa haruni kwann hakuwa musa?musa alikuwa mkuu wa msafara kuwa vusha wana wa Israel na kumbuka pia musa alipopewa maelekezo ya kimueleza farao walikwenda na haruni kwa hivyo basi musa hakuwa kuhani,mapadre ni makuhani kama ilivyokuwa kwa watoto wa haruni,kwa kutambua mapungufu ya musa hakumfanya kuwa kuhani.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu naona unaandika kwa kubahatisha sana, una unga unga maelezo sana.
Ngoja nikupe ufafanuzi wa kina kidogo.
1/Musa ndio alikuwa mtu wa kwanza kutumika katika Madhabahu ya kikuhani. Aliandaa yeye madhabahu na akaizindua yeye. (
Kutoka 40:1-11)
2/Ndio kuhani pekee wa madhabahu ya kwanza aliyepakwa mafuta na Mungu mwenyewe. (
Kutoka 3:12)
3/Na ni yeye Musa aliyewapaka mafuta makuhani wengine wote waliofuata kuja kutumikia madhabahuni.(
Kutoka 40:12-16)
4/Hakuna mahali popote ambapo Biblia inasema Musa alikuwa na Kigugumizi, Biblia inasema Musa alikuwa hawezi kuzungumza vizuri kwa sababu alikuwa ana ulimi mzito. (
Kutoka 4:10-12). Kitaalamu Kuwa na ulimi mzito kunaweza kumfanya mtu ashindwe kuzungumza vyema(Slagish speech) lakini hakuwezi kumfanya mtu awe na kigugumizi.
5/Suala la kuwa kuhani lilikuwa ni Full time duty, kwa nafasi aliyokuwa nayo Musa lisingewezekana kwake(Alikuwa akihusika na mambo mengi sana), na Mungu aliichagua koo ya haruni kutoka kabila la walawi kuwa jamii pekee ya ukuhani.
Zipo dhana za kiimani zinazosema kuwa kwa sababu Musa alikuwa na damu ya hatia(Aliwahi kuua) hivyo nafasi ya kuwa kuhani mkuu isingempasa, na wapo wanaosema japokuwa Musa alikuwa Mlawi, lakini uzao rasmi wa Musa ulikuwa una utata fulani kwa wayahudi(inasemekana Musa alioa mwanamke kutoka Afrika!!), hivyo suala ukuhani kwenda kwa Musa lingekuwa tata pia.
6/Hakuna uhusiano wowote wa kimantiki kati ya Ukuhani wa Kwenye Biblia na Upadri wa kanisa katoliki, kwa sababu hizi...
-Makuhani walioa na kuzaa.
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikabila tu(Kabila la Walawi)
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikoo tu(Ukoo wa Haruni tu)
-Ukuhani lilikuwa ni jambo la kiyahudi tu.
-Ukuhani ulikuwa kwenye Hekalu/Hema tu.