Sijawahi kuona Padre kilema

Hawaruhusiwi na biblia imewatenga vilema:

Biblia Mambo ya walawi 17
Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

18 Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

19 au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

20 au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

21 mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za Bwana kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.
 
Akiwa kilemaa ataweza kufanya ilee miujizaa ya uongo kama mwenyewe mtumishi wa mungu ameshindwa kujiponya haya akija kilema mwingine aataweza lilee game kaka haya maisha akili tu .........wakristo shutukenii mjee hukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimependa hoja yako,ila ni yupi alikuwa mkuu kati ya hawa wawili?mbona akazungumza na musa badala ya Haruni?Ni kazi ya kuhani kwenda mbele za Bwana kwa niaba ya kundi sasa hapa ukisema musa hakuwa kuhani napata shaka kidogo kwani hata waliposubu sanamu ni musa aliyeanguka kifudifudi kwa siku 40 mbele za mungu je hili unalizungumziaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili kupata majibu mazuri kabisa nakuomba usome habari ya safari ya wana wa Israel ambyo utaipata mwanzo mwishoni na kutoka mwanzo hadi mwisho utayapata yote lkn niseme hivi musa alichaguliwa na kuwa karibu na mungu kwa kila agizo kama kiongozi wa kuwapeleka wana wa Israel ktk nchi yao toka misri utumwani lkn alimwambia MUNGU ya kuwa nitawezaje ikiwa mimi ni mwenye kigugumizi kikari ndipo akawepo haruni ambaye baadae alikuja kuwa kuhani mkuu pamoja na wanawe wane wa kiume lkn baadae walikufa wawili walipokwenda kinyume na maelekezo ya MUNGU wakabaki wawili pamoja na baba yao wakawa watatu MUNGU anama kusudi yake ktk ukuu musa ndo alikuwa juu kwakuwa yeye aliongea na MUNGU mojakwamoja na kiasha akaambiwa mwambie haruni awaambie wana wa Israel kwa mawna hiyo musa alikuwa mtumwa wa MUNGU au kiunganishi na haruni lkn mwishoni huko utaona alikuja kuanza kuongea nao wote lkn pia mtekelezaji wa maelekezo yote ya MUNGU alikuwa haruni,ila pia wakuu wa kabila zote 12 waliokuwa wakuu wa majeshi MUNGU aliwateuwa lkn pia walikuwa walinzi wa kuhani haruni na watoto wake ambao pia walikuwa makuhani lkn pia kumbuka walikuwa kwa ajiri ya kulonda lile sanduku la agano la MUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu naona unaandika kwa kubahatisha sana, una unga unga maelezo sana.

Ngoja nikupe ufafanuzi wa kina kidogo.

1/Musa ndio alikuwa mtu wa kwanza kutumika katika Madhabahu ya kikuhani. Aliandaa yeye madhabahu na akaizindua yeye. (Kutoka 40:1-11)

2/Ndio kuhani pekee wa madhabahu ya kwanza aliyepakwa mafuta na Mungu mwenyewe. (Kutoka 3:12)

3/Na ni yeye Musa aliyewapaka mafuta makuhani wengine wote waliofuata kuja kutumikia madhabahuni.(Kutoka 40:12-16)

4/Hakuna mahali popote ambapo Biblia inasema Musa alikuwa na Kigugumizi, Biblia inasema Musa alikuwa hawezi kuzungumza vizuri kwa sababu alikuwa ana ulimi mzito. (Kutoka 4:10-12). Kitaalamu Kuwa na ulimi mzito kunaweza kumfanya mtu ashindwe kuzungumza vyema(Slagish speech) lakini hakuwezi kumfanya mtu awe na kigugumizi.

5/Suala la kuwa kuhani lilikuwa ni Full time duty, kwa nafasi aliyokuwa nayo Musa lisingewezekana kwake(Alikuwa akihusika na mambo mengi sana), na Mungu aliichagua koo ya haruni kutoka kabila la walawi kuwa jamii pekee ya ukuhani.
Zipo dhana za kiimani zinazosema kuwa kwa sababu Musa alikuwa na damu ya hatia(Aliwahi kuua) hivyo nafasi ya kuwa kuhani mkuu isingempasa, na wapo wanaosema japokuwa Musa alikuwa Mlawi, lakini uzao rasmi wa Musa ulikuwa una utata fulani kwa wayahudi(inasemekana Musa alioa mwanamke kutoka Afrika!!), hivyo suala ukuhani kwenda kwa Musa lingekuwa tata pia.

6/Hakuna uhusiano wowote wa kimantiki kati ya Ukuhani wa Kwenye Biblia na Upadri wa kanisa katoliki, kwa sababu hizi...
-Makuhani walioa na kuzaa.
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikabila tu(Kabila la Walawi)
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikoo tu(Ukoo wa Haruni tu)
-Ukuhani lilikuwa ni jambo la kiyahudi tu.
-Ukuhani ulikuwa kwenye Hekalu/Hema tu.
Ktk hayo yote nimekosa nn?kwani hata huko ulikopita nimepita lkn ikiwa nawe ulitaka kusema basi ungesema tu kuliko hivyo je ni wapi paliandikwa ya kwamba musa alikuwa kuhani?lkn pia kuandaa maskani ile ilitosha kuitwa kuhani?mpango wa MUNGU ulikuwa na hatua mkuu lkn pia ubarikiwe kwa hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu naona unaandika kwa kubahatisha sana, una unga unga maelezo sana.

Ngoja nikupe ufafanuzi wa kina kidogo.

1/Musa ndio alikuwa mtu wa kwanza kutumika katika Madhabahu ya kikuhani. Aliandaa yeye madhabahu na akaizindua yeye. (Kutoka 40:1-11)

2/Ndio kuhani pekee wa madhabahu ya kwanza aliyepakwa mafuta na Mungu mwenyewe. (Kutoka 3:12)

3/Na ni yeye Musa aliyewapaka mafuta makuhani wengine wote waliofuata kuja kutumikia madhabahuni.(Kutoka 40:12-16)

4/Hakuna mahali popote ambapo Biblia inasema Musa alikuwa na Kigugumizi, Biblia inasema Musa alikuwa hawezi kuzungumza vizuri kwa sababu alikuwa ana ulimi mzito. (Kutoka 4:10-12). Kitaalamu Kuwa na ulimi mzito kunaweza kumfanya mtu ashindwe kuzungumza vyema(Slagish speech) lakini hakuwezi kumfanya mtu awe na kigugumizi.

5/Suala la kuwa kuhani lilikuwa ni Full time duty, kwa nafasi aliyokuwa nayo Musa lisingewezekana kwake(Alikuwa akihusika na mambo mengi sana), na Mungu aliichagua koo ya haruni kutoka kabila la walawi kuwa jamii pekee ya ukuhani.
Zipo dhana za kiimani zinazosema kuwa kwa sababu Musa alikuwa na damu ya hatia(Aliwahi kuua) hivyo nafasi ya kuwa kuhani mkuu isingempasa, na wapo wanaosema japokuwa Musa alikuwa Mlawi, lakini uzao rasmi wa Musa ulikuwa una utata fulani kwa wayahudi(inasemekana Musa alioa mwanamke kutoka Afrika!!), hivyo suala ukuhani kwenda kwa Musa lingekuwa tata pia.

6/Hakuna uhusiano wowote wa kimantiki kati ya Ukuhani wa Kwenye Biblia na Upadri wa kanisa katoliki, kwa sababu hizi...
-Makuhani walioa na kuzaa.
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikabila tu(Kabila la Walawi)
-Ukuhani ulikuwa ni wa kikoo tu(Ukoo wa Haruni tu)
-Ukuhani lilikuwa ni jambo la kiyahudi tu.
-Ukuhani ulikuwa kwenye Hekalu/Hema tu.
Lkn kingine fuatilia kwa makini sana utaratibu wa ki katoriki utayaona hauo kalibia aslimia kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa mkatoliki nadhani swali la kitoto hivi usingeliuliza hapa. Upadre ni kujitoa kwa Mungu na huwezi kumtolea Mungu kitu chenye kasoro. Lazima uwe mkamilifu usie na mawaa ndipo unaweza kujitoa kumtumikia Mungu na kanisa kama kuhani(padre)
Mbona mapadre wengi wengi wamefeli form six wakaona upadre ndo option pekee ya kukimbilia? Kuna rafiki yangu padre ana division four ya hgl lakini ni padre. Je huyo naye utasema ni wito?
 
Mbona mapadre wengi wengi wamefeli form six wakaona upadre ndo option pekee ya kukimbilia? Kuna rafiki yangu padre ana division four ya hgl lakini ni padre. Je huyo naye utasema ni wito?
Kupaya div four ndiyo kufeli? Kwanza hamna Padre mwenye div four. Huo ni uongo.
 
Mbona mapadre wengi wengi wamefeli form six wakaona upadre ndo option pekee ya kukimbilia? Kuna rafiki yangu padre ana division four ya hgl lakini ni padre. Je huyo naye utasema ni wito?
Four kwenu ni Fail!??

Tanzania ni PASS.
 
Kupaya div four ndiyo kufeli? Kwanza hamna Padre mwenye div four. Huo ni uongo.
Mi nilisoma naye na alikuwa kilwza sana. Alipata div four believe me. Waseminari vipanga huwa hawawi mapadre ispokuwa wale wanaochechemea ndo wanajifanya kuwa na wito
 
Mbona mapadre wengi wengi wamefeli form six wakaona upadre ndo option pekee ya kukimbilia? Kuna rafiki yangu padre ana division four ya hgl lakini ni padre. Je huyo naye utasema ni wito?
Nani kakudanganya..yani Div four uende Upadre...? hebu cheki Matokeo ya Seminari uone..Au huzijui Catholic Seminary
 
Mi nilisoma naye na alikuwa kilwza sana. Alipata div four believe me. Waseminari vipanga huwa hawawi mapadre ispokuwa wale wanaochechemea ndo wanajifanya kuwa na wito
Aisee.....hivi una habari watu Intelligent ni mapadre...? We naona unaliangalia kanisa Katoliki kwa jicho la kibashite...Ogopa hii taasisi....
 
Back
Top Bottom