Sijawahi kuona Padre kilema

Sijawahi kuona Padre kilema

Kusali kwangu kote hapa duniani sijawahi kukutana na padre kilema. Au ni makanisa ninayo sali tuu? Je nikigezo kimojawapo cha kuwa Padre?
Yani ni hivi
Kwasbb maisha ya upadre ni maisha ya useja(yaani huoi) anatakiwa anayeomba kusomea upadre asiombe tuu kwa sbb labda kutokana na ulemavu au kushindwa maisha ya kawaida ya duniani
Anatakiwa mwimbaji aombe akiwa na msukumo wa kweli kutoka ndani ndio maana zamani walikua wanadiscourage walemavu kwa dhana kwamba mtu asijekuona upadri ama usista ndio sehem ya kujificha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unapotosha.
1. Musa hakuwa "bubu", bali alikuwa na kigugumizi.

2. Musa hakuwa kuhani, hivyo hakuwahi kupakwa mafuta. Kuhani alikuwa Haruni. Wsliokuwa wsnapakwa mafuta kwa desturi ya kiyahudi ni makuhani na wafalme.
Asante kwa kunikosoa.
Hoja hujibiwa kwa hoja, nami nitajibu hoja zako zote mbili hapa hapa.

1/Nilisema Musa alikuwa na ulemavu katika kuongea(Bubu!?). Neno bubu nimeliweka ndani ya mabano likiwa na alama ya mchangao na kuuliza, hivyo neno bubu ni maelezo yangu ya ziada, yenye kushangaa na kujiuliza, nikimaanisha nahisi hivyo japokuwa sina uhakika.
Katika ulimwengu wa sasa wa lugha ya kiswahili, Maneno kama Bubu, Kipofu, Kiwete na Kiziwi yanapigwa vita kutumika kwa sababu yanaunyanyapaa fulani hivi, na yanapotosha. Hivyo kitaalamu hutupendi kuyatumia sana japokuwa kijamii yamezoeleka.

Kitaalamu Bubu(Speech Disability) maana yake ni uwezo duni wa kuweza kuongea au kujieleza ukaeleweka katika hali ya kawaida, na ububu uko katika viwango tofauti sana, kuwa 'bubu' haina maana huwezi kuongea kabisa, wapo 'mabubu' wengi wanaongea kwa sehemu fulani. Kama ilivyo kwa mtu asiyeona(kipofu?), wapo miongoni mwao wanaweza kuona pia, hata kwa 'bubu' wapo wengi wanao uwezo fulani wa kuongea.

Je, Musa alikuwa na Kigugumizi? Hapo inabidi pia uje na maelezo ya kuthibitisha hilo kwa kutumia biblia, otherwise itakuwa ni hadithi ya kutunga.

2/Kupakwa mafuta ni neno la jumla sana, tena la kawaida sana kwenye Biblia likiwa na maana Mungu kukuteua mahususi ili kwenda kufanya kazi yake maalum.
Mungu anaweza 'kukupaka mafuta' kwenda kufanya kazi yake mahususi yoyote. Wapo walioteuliwa kuwa makuhani, wengine mitume, wengine manabii nk.

Makuhani ni watu walioteuliwa na Mungu mahususi kwenda kufanyakazi ndani ya Hekalu tu. Hao ni wapakwa mafuta pia.

Musa aliteuliwa mahususi na Mungu kwenda kufanya kazi ya kuongoza wana wa israeli kutoka utumwani Misri. Hivyo Musa ni mpakwa mafuta kwa 100%.
 
Kusali kwangu kote hapa duniani sijawahi kukutana na padre kilema. Au ni makanisa ninayo sali tuu? Je nikigezo kimojawapo cha kuwa Padre?
Kazi ya upadre wa Katoliki inataka kabla ya kujiunga uwe physically & mentally fit. Vilema wapo lakini wamevipata wakiwa kazini. Wengi wa namna hiyo hupewa special duties.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni dhana iliyo wazi tu...! Aihitaji kuumiza kichwa katika tafakari ya mleta UZI...!

Kumbuka ni hawa Mapadri ambao pengine hujivika UNABII wa Kitapeli, kujifanya wanatibu VILEMA na VIPOFU...!!

Je...unafikiria nini, ikiwa huyo Padiri/Mchungaji/Askofu atasimama Madhabahuni ama katika jukwaa, akiwa na nia ya KUULAGHAI UMMA kuwa anatibu/anaponya VILEMA, wakati nae akiwa Kilema...!!?

Yawezekana huu ukawa ni Mpango ulioandaliwa mapema na kwa malengo mahususi...!!

Tafakari....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni dhana iliyo wazi tu...! Aihitaji kuumiza kichwa katika tafakari ya mleta UZI...!

Kumbuka ni hawa Mapadri ambao pengine hujivika UNABII wa Kitapeli, kujifanya wanatibu VILEMA na VIPOFU...!!

Je...unafikiria nini, ikiwa huyo Padiri/Mchungaji/Askofu atasimama Madhabahuni ama katika jukwaa, akiwa na nia ya KUULAGHAI UMMA kuwa anatibu/anaponya VILEMA, wakati nae akiwa Kilema...!!?

Yawezekana huu ukawa ni Mpango ulioandaliwa mapema na kwa malengo mahususi...!!

Tafakari....!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii sijui imekaaje! Ila kwa mapadre ni nadra sana kusikia anasema njoooni kwangu wenye mapepo niwaombee wasiojiweza watajiweza. Na toka nianze kusali katoliki mwaka wa 38 sasa sijawahi ona mtu kaanguka kisa pepo ndani ya kanisa.
 
Kigugumizi,mwanya,kengeza,ni maumbile tu siyo ulemavu otherwise wote tungekuwa walemavu basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wagalatia mnajua sana kuchakachua mambo. Mnajua kutunga maneno.

Biblia inasema Musa alikuwa hawezi kuongea vyema(Permanent Speech Disability) kiasi ambacho ikabidi Haruni awe anaongea badala yake...

Kuna mtu anasema alikuwa ana kigugumizi(Sijui ametoa wapi hiyo maneno?), Na wewe unasema ni maumbile tu lakini sio ulemavu!!!!
 
Mkuu usikufuru.
Mbele ya Mungu, mapungufu yako ya kimwili sio issue kabisa. Mungu akikuchagua, hakuna wa kupinga. Yeyote yule anaweza kupakwa mafuta. Ni mungu mwenyewe anaamua.

Unamjua Musa wewe?
Nenda kamsome halafu utagundua alikuwa na ulemavu gani.
Kwa kweli Biblia ni kitabu kitakatifu sana na unaitaji kujipanga sana kuelewa maandishi ya kibibilia. Wee bwana wee biblia sio novel. Sikia wanaposema Musa akuwa na uwezo wa kuongea jitahidi sana kuelewa spiritual sense ya andiko ilo. Musa alikuwa fit kuliko unvyofikilia hiyo ni lugha ya kibibilia. Nyie ndo mkisikia anayenipenda abebe msalaba wake kila siku anifate, mnakimbia mnachonga misalaba mnabeba mabegani. Take care with the Bible wenzio wanasomaga miaka mingi kuja kuhubili sio unakurupuka from colomije unavamia faculty za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom