Sijawahi kuona Padre kilema

Sijawahi kuona Padre kilema

Mkuu usikufuru.
Mbele ya Mungu, mapungufu yako ya kimwili sio issue kabisa. Mungu akikuchagua, hakuna wa kupinga. Yeyote yule anaweza kupakwa mafuta. Ni mungu mwenyewe anaamua.

Unamjua Musa wewe?
Nenda kamsome halafu utagundua alikuwa na ulemavu gani.
Sijawahi gundua hilo mkuu,labda unijulishe kama alikuwa na ulemavu gani na ulianzia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa mkatoliki nadhanj swali la kitoto hivi isingeliuliza hapa. Upadre ni kujitoa kwa Mungu na huwezi kumtolea Mungu kitu chenye kasoro. Lazima uwe mkamilifu usie na mawaa ndipo unaweza kujitoa kutumikia kanisa kama kuhani(padre)

Ok.
 
Kwani kuna sakrament ngapi? Na mafuta yapi wewe ulisungumzia? Je mafuta hayo yanatofauti gani na yale anayopakwa padre?
Mkuu sakrament ni nyingi tu,na hakuna anayepata zote,kwa mujibu wa kanisa. Lakini katika biblia hizo sakrament sijaziona ndio maana nimezungumzia kupakwa mafuta maana hilo lipo kibiblia,isijekuwa tunazungumzia vitu tofauti hapa. Je kuna mpakwa mafuta aliyekuwa mlemavu katika biblia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa mkatoliki nadhanj swali la kitoto hivi isingeliuliza hapa. Upadre ni kujitoa kwa Mungu na huwezi kumtolea Mungu kitu chenye kasoro. Lazima uwe mkamilifu usie na mawaa ndipo unaweza kujitoa kutumikia kanisa kama kuhani(padre)
Kwani mpaka leo bado kuna makuhani?
 
Ndio ni kigezo kimojawapo...Na pia hakuna padre hanithi(ashakum si matusi)

Kwanini...?

Upadre na Sadaka(Sacrifice)...yani unajitoa mzima mzima kama ulivyo....Yani si una-opt kuwa padre kwasababu wewe ni mlemavu, au wewe audi.n...d ndio unakimbilia upadre..upadre ni Sadaka iliyosafi..ni kujitoa..bila kujibakiza..

Wajuzi watajazia nyama
Sahihi mkuu. Upadre ni kama kuwa mwanajeshi. Huingii kwa kufanya escapism ya maisha ya kawaida. Unapaswa kuwa mzima tena mzima hasa. Ni uzima wa kimwili, kiroho na kiakili pia.
Uwe vema kiuweledi, nidhamu, uchaji wa MUNGU nk. Kule kwa uelewa mzuri si kichaka cha kujificha na kuyakimbia maisha ya kawaida.
 
Sijawahi gundua hilo mkuu,labda unijulishe kama alikuwa na ulemavu gani na ulianzia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana.
Biblia inasema Musa alikuwa na ulemavu wa kuongea (Bubu!?), hakuwa na Uwezo wa kuongea kwa sauti akasikika na kuelewekeka. Na ni ulemavu aliokuwa nao hata kabla hajapata utume(kupakwa mafuta), na hata alipopakwa mafuta ya kwenda kutumikia kazi ya Mungu, Musa alikataa kwa sababu hiyo ya ulemavu huo. Mwisho wa siku Mungu akamchukua Haruni kuwa msaidizi wa Musa katika kuongea mbele za watu nk.

KUTOKA 4:10-17
 
Kusali kwangu kote hapa duniani sijawahi kukutana na padre kilema. Au ni makanisa ninayo sali tuu? Je nikigezo kimojawapo cha kuwa Padre?
Nimesoma mara tano sijakuelewa.Yaani unashangaa kwamba hujawahi kumwona padre kilema au umeshangaa kuona padre kilema? Hebu fafanua ndugu.
 
Back
Top Bottom