Sijaamini macho yangu kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza kuteuliwa kuwa DED wa Masasi

Mimi sijaamini macho yangu kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza kuteuliwa kuwa DED wa Masasi.

Ni ushauri wa bure kwa yule anayewateuwa. Kwanza kazi ya DED inahitaji uelewa mkubwa wa Serikali za Mitaa na anayeteuliwa ni vyema atokane na watumishi waliobobea katika Utumishi wa Serikali za Mitaa. Hawa watumishi wamekulia humo mpaka akafikia ngazi za juu kamaa Afisa Mipango, Afisa Kilimo/Mifugo, Mhandisi wa Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Ardhi, Mweka Hazina, Afisa utamaduni n.k.

Halmashauri ni nyingi na wako wengi wenye kisomo na waadilifu. Wateuliwe kutokana na hiyo orodha.

Pili kuna watumishi wazuri toka kwenye Mawizara na mashirika ya Umma wenye kisomo na waadilifu.

Kweli mtu anayeteuliwa ambaye hajui vyema Serikali za Mitaa pili ni kada wa chama?

Kama ni kweli nimepatwa na mshangao mkubwa sana.
NCHI HII INA TATIZI KUBWA LA VIONGOZI
 
Tulia wewe, nchi hii haihitajiki uwe umesoma sana ndio upate cheo. Hata kama hujui kuandika na kusoma ilimradi una connection basi utakula mema ya nchi hii
 
Wapi katiba ya nchi inakataza kumteua DED asiyetoka katika utumishi wa umma?!!!

Unaiwekea mipaka "presidential decree"?!!!
 
Yale yake ya zamani yanarudi kinyumenyume. Kila shirika la umma kulikuwa na tawi la chama na mwenyekiti alikuwa na sauti saana kuliko hata mkurugenzi. Acha tuone tutakapofika si ajabu kushituka tutakuta ni saa saba mchana ndiyo tinatoka usingizini.
 
Huyo atakuwa anamletea longolongo kule kanda ya ziwa kaamua kumtoa kiaina muda si mrefu anatenguliwa na biashara itakuwa imeishia hapo.
 
Umeishia kuandika blaa blaa tu pasipo kuonyesha kwa hoja na ushahidi kuwa aliyeteuliwa hana sifa kama unavyotaka kuaminisha watu hapa. Je unajuwa historia yake katika Taifa hili? Unajuwa kabla ya kuwa mwenyekiti alikuwa nani? Unaifahamu Elimu yake? Unafahamu amefanya kazi maeneo yapi katika Taifa letu? Acha kukurupuka tu hapa.
 
Mimi sijaamini macho yangu kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza kuteuliwa kuwa DED wa Masasi.

Ni ushauri wa bure kwa yule anayewateuwa. Kwanza kazi ya DED inahitaji uelewa mkubwa wa Serikali za Mitaa na anayeteuliwa ni vyema atokane na watumishi waliobobea katika Utumishi wa Serikali za Mitaa. Hawa watumishi wamekulia humo mpaka akafikia ngazi za juu kamaa Afisa Mipango, Afisa Kilimo/Mifugo, Mhandisi wa Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Ardhi, Mweka Hazina, Afisa utamaduni n.k.

Halmashauri ni nyingi na wako wengi wenye kisomo na waadilifu. Wateuliwe kutokana na hiyo orodha.

Pili kuna watumishi wazuri toka kwenye Mawizara na mashirika ya Umma wenye kisomo na waadilifu.

Kweli mtu anayeteuliwa ambaye hajui vyema Serikali za Mitaa pili ni kada wa chama?

Kama ni kweli nimepatwa na mshangao mkubwa sana.
Huyo anayewateua akili yake yote iko kwenye 2025. Ndiyo maana hatuwezi kuendelea kwa kuwa viongozi wanawaza uchaguzi tu na matumbo yao.
 
Tulia wewe, nchi hii haihitajiki uwe umesoma sana ndio upate cheo. Hata kama hujui kuandika na kusoma ilimradi una connection basi utakula mema ya nchi hii
Lini cheo kikawa kwa ajili ya waliosoma ?!!!

Siasa ina mambo yake....
 
Umeishia kuandika blaa blaa tu pasipo kuonyesha kwa hoja na ushahidi kuwa aliyeteuliwa hana sifa kama unavyotaka kuaminisha watu hapa. Je unajuwa historia yake katika Taifa hili? Unajuwa kabla ya kuwa mwenyekiti alikuwa nani? Unaifahamu Elimu yake? Unafahamu amefanya kazi maeneo yapi katika Taifa letu? Acha kukurupuka tu hapa.
Soma post #25 halafu useme huyo Jamaa kama anazo hizo sifa.
 
Back
Top Bottom