Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.