Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 12,417
- 30,927
Duniani bado kuna watu wema. Nakumbuka Housegirl wa mh Rais Karume tulipanda basi toka Malawi. Miaka ya 2007/8. Nilimpigisha Sana story njiani mpaka akafurahi sana.
Tulipofika Msamvu usiku kabla stend mpya haijajengwa wakaja wahuni wengi including vibaka. Yule dada kwa kutambua hatari iliyokuwa inanikabili akaniambia twende nyumbani hapa siyo salama. Akakodi taxi tukaenda mpaka kwao maeneo ya soko la mitumba la Sabasaba.
Tulipofika hapo ikakonekana Mimi itakuwa ngumu kulala pale kwao na mbaya zaidi ilikuwa saa nane usiku na wahuni walikuwa wengi sana maeneo yale.
Yule dada akampa dreva tax hela na akamuambia anipeleke guest salama na nikipatwa na tatizo yeye dreva tax atawajibika na alichukua namba yake akahakikisha anaipiga inaita.
Nilipewa hela ya guest pia na yule dada. Dreva taxi akanipeleka guest moja nzuri karibu na soko kubwa mjini Morogoro. Kesho yake nikaendelea na safari ya kwenda Mwanza.
Naomba wewe dada kama ni memba humu tuwasiliane, ulinisaidia mnooo.
Tulikaa siti ya nyuma kabisa ya basi na Wamalawi. Na katika maongezi yetu tuliwafunika Mambo mengi kuanzia exposure mpaka lugha ya Kiingereza.
Mungu mbariki dada yule na familia ya mzee Karume.