Siendi tena Karume Soko la Mitumba!

Siendi tena Karume Soko la Mitumba!

Ungemaliza kwa kiswahili ungelinda heshima yako.
mkuu umeanza lini kwenda hapo karume?? dar umekuja mwaka gani??

kama unasimamishwa unataka mwenyewe kusimama sio kusingizia dawa

mwezi uliyopita niliingia pale hao unaowasema walinifata nikawaignore nikafata vitu vyangu nikasepa vizuri tu

kama ni mgeni hapa dar hao watu watakutesa sana sababu wapo kila sehemu hata kwenye kupanda daladala wapo if you what i mean hommie
 
Wanakuzungushaje kwa mfano. Wewe nenda uso serious humuangalii mtu usoni. Huwa naenda kule nshajipangia bei ya viatu, raba na tisheti. Nikifika hata wanashauri vipi naonsoka nisiporidhika. Hali ngumu mkuu watu badala ya kwenda kuiba wameamua kuwa madalali!!!
 
Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
pole sana pale tulishaachaga siku mingi, hata pale tip top maumivu tupu
 
Mimi yalinikuta hayo, nikachoma laki kwa vishati vinne vya mtumba vimechoka balaa, nimevifungua nyumbani mpaka nikaanza kujishangaa, jamaa aliniingiza uchochoroni kiduka kiko ndani ndani mno, wakati kayapita maduka kama 100, kumbe ni winga/dalali; na hiyo kuwaonea huruma ndio ikaniponza, na walijua kabisa bei hiyo wakitaja pesa nitakuwa nayo, hawakurogi ila ni wanacheza na saikolojia vibaya mno! Mashati yenyewe nikakuta hata vishkizo hayana eti
 
Hamna soko lina vitu vizuri kama karume ila viatu nafkiri ndo zaidi pale. Halafu kuna ujinga wanawafanyiga wasiojua; wanachukua kiatu cha 30000 dukani wanakiqeka ktk mtumba halafu kinauzwa kuanzia 80. Vingine wanavisugua ktk soli vionekane vya mtumba ila kwa watalaam unavicheki tuu Unahitajika umakini usikubali kuambiwa subiri nikuletee we usifuate mwenyewe utakikuta tuu hukohuko.
 
Watu kama nyie kwenye chaguzi za kisiasatunawaita 'Swing voters' maana hadi siku ya mwisho wa kampeni hujui nani au chama gani ukipigie kura.
 
kwenda karume au kariakoo kununua shati sijui raba huwa naona ni kupoteza mda tu kwanza utazunguka weee ni mara 100 nizunguke minadani kuna vitu vikali na bei rahisi na kupigwa sio rahisi nikikosa uko nanunua kwa wanaotembeza tena asubuhi au jioni wakiwa na njaa unachukua kwa bei poa sana
 
Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
Ukiona sehemu ina Wamakonde wengi iogope sana...
 
Niliuziwa sandals feki kwa elfu 45, wakati naiangalia niliona ni original kabisa lakini baada tu ya kulipa pesa nikapanda daladala nikaanza kujiuliza "hivi sandal ni og hizi kweli?" Nikazichungulia nikaona feki hapo ndio akili imerudi, wale jamaa wana dawa nawaambia.
 
Kuna siku nilienda pale jamaa akanidaka na kunipeleka duka fulani nkakuta kiatu safi kizuri sana na kikanitosha fresh tu......kuuliza bei akanambia elfu 60, bei ya mwisho mpaka 40. Nikaondoka halafu baada ya dakika 5 nikarudi nikiwa na uhakika yule dalali hayupo hivyo ntamkuta mhusika mwenye duka. Kiatu cha elfu 60 nikannua kwa elfu 15 kiungwana kabisa
My point; usiogope wale jamaa wakikuambia wakakuonyeshe vitu vizuri vilipo. Ila wewe tumia akili yako binafsi kwenye ku-bargain kulingana na bajeti yako mfukoni.
 
Back
Top Bottom