Siendi tena Karume Soko la Mitumba!

Siendi tena Karume Soko la Mitumba!

Uchunjuba Punjubi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
799
Reaction score
624
Wakuu, habari zenu!

Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale.

Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana?

Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile.

Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli?

Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
 
Kumbe sababu ushaijua tayar "mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? "
Hiyo nimeisemea kibinaadamu lazima uwaze hivyo, maana wanahustle sana, ila akili yako inakuwa haiko sawa kwa muda hivi.
 
mkuu umeanza lini kwenda hapo karume?? dar umekuja mwaka gani??

kama unasimamishwa unataka mwenyewe kusimama sio kusingizia dawa

mwezi uliyopita niliingia pale hao unaowasema walinifata nikawaignore nikafata vitu vyangu nikasepa vizuri tu

kama ni mgeni hapa dar hao watu watakutesa sana sababu wapo kila sehemu hata kwenye kupanda daladala wapo if you know what i mean hommie
 
Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
Na kwa taarifa yako katika vitu vyote ulivyonunua kuna "Cha Juu" umewekewa na hao jamaa. Haiwezekani mtu akawa eti anamiliki au yuko share kwenye hayo maduka yote.
 
Ni kweli mkuu karume ukiuliza kitu utazungushwa soko zima na mtu anakuwa na juhufi hachoki mwishowe unaweza kununua hata kitu usicho kikusudia
Duh kweli! Nimekumbuka siku moja niliwahi kuulizia kitu, hali ilikuwa hivo
 
Sehemu nyingine ni stand kuu ya ubungo ya kukatia tiketi,

Kuna siku moja nilienda mitaa ya posta mpya nikakutana na jamaa watatu wamevalia suti moja matata sana, sijui wale wakuda walizishonea Paris Ufaransa, sasa napita zangu nipo na mshkaji wangu akaniambia wale jamaa pale ni matapeli, na ukipita karibu nao wanakupiga kila ulicho nacho kwa maneno tu..
 
Wakuu, habari zenu! Huu ni uamuzi wangu ambao nimeamua kuuchukua baada ya kuona napata hasara kila ninapoenda soko la mitumba pale karume, opposite na makao makuu ya TFF pale. Kitu cha kwanza ni ile system yao ukiulizia kitu basi watahakikisha wanakuzungusha karibia soko zima, yaani wanakuweka kwenye chain flan ambayo hutoki( sijui wana dawa wale) utasikia twende huku ukaangalie, kaa hapa tukuletee, vitu usipovipenda utaambiwa subiri tukuangalizie, twende huku, ukiwaambia nimeahirisha hawakuelewi kabisa, ni kama akili yako wanakuwa wameiteka hivi mpaka unaanza kuwaonea huruma kwa jinsi walivyokuhangaikia hivyo usiponunua hata kimoja si itakuwa shida sana? Kingine ni bei zao, wanasaikolojia ya juu sana wale watu, wanakujua kabisa huyu bei zake ni hizi, huyu zile. Kuna siku nimeenda pale nimechoma laki tatu hivi hivi nimekuja kutafakari vitu nilivyonunua hata havieleweki kabisa, mpaka nikawaza hawa jamaa walinipa nini, hivi nilikuwa na akili yangu timamu kweli? Kwa sasa nilichoamua ni kutokwenda kabisa karume, ntakuwa naingia madukani tu au Tandika na sehemu zingine zenye mitumba.
Hao jamaa japo sijawahi kutana nao ila kwa sifa hizo tunapaswa kuwapongeza mkuu.Shughuli za biashara wanaweza maana wana uwezo wa kumshawishi mteja awaamini na kupenda bidhaa bila kuweka mashaka.
 
Mtoa maada umenikumbusha na Mimi ishanitokea Sana hapo karume nikifika kwanza mule ndani Kuna kaharufu Fulani sijui waga Cha madawa .wengi wao matapeli tu me mwenyewe pale nikifika nanunua tu official shati basi kwenye viatu siendi ntakuja kudakwa na kwenye suruali Bora ninunue kwa wamachinga wale wa barabaran Uhuru hapo
 
Dar es salaam karibia kila duka au site kuna madalali. Cha kwanza kabisa ukifika mahali mtambue muhusika mkuu au mmiliki.
Usipokuwa makini unaweza kuuziwa vitu na dalali wa pili au wa tatu.
Mtu utamkuta hana bidhaa ile anakwambia subiri au twende. Kwani wewe mbu mpaka upelekwepelekwe.
La muhimu ni kwamba ujue unakwenda mtaa upi, kununua nini na bei gani umepanga kununulia hiyo bidhaa. Ukizingatia hayo utasave money. Wale ni matapeli wakubwa. We biashara gani inamilikiwa na watu mpaka watano!
 
Back
Top Bottom