Siasa za CCM ni kama Maisha ya Nyoka, kujichubua na kutaga mayai

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
SIASA ZA SISIEMU NI KAMA MAISHA YA NYOKA, KUJICHUBUA NA KUTAGA MAYAI.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Aliyesema SISIEMU itadumu daima hakusema kwa bahati mbaya. Alisema huku akijua kuwa Ukoloni upo na mpaka leo unadumu. Ili SISIEMU ife itahitaji Ukoloni nao ufe. Nazungumzia Ukoloni wa wale mabeberu. Kwa akili zangu hizi ndogo ninajua kabisa ukoloni hauwezi kuisha, na kama utaisha itachukua miaka zaidi ya elfu moja. Sijajua ni mfumo gani utakaokuwepo miaka hiyo.

Maisha ya Nyoka yanashangaza, hanamiguu lakini anajongea, sio samaki lakini anauwezo wa kuishi majini kwa muda. kilikuwa na nyoka wale wenye mabawa. Hiyo ni habari ya siku nyingine. Nyoka ndiye mnyama pekee ambaye amepewa uwezo wa kujirenew, ukiachana na ndege ambao hujinyonyoa manyoya ili yaote mwengine.

Tawala nyingi zinatumia mfumo wa nyoka kama sio majoka. Alama ya nyoka ni ishara ya utawala usio na kikomo.

Nyoka na kujichubua na kujivua gamba lake.
Nyoka na mayai yake.
Nyoka anapojichubua haimaanishi kuwa amekuwa nyoka mwingine. Ni nyoka yuleyule katika upya wa nje.

SISIEMU ni matokeo ya Ukoloni, kama utafuatilia kwa kina utagundua kuwa mifumo ya Wakoloni ndio ileile wanaotumia SISIEMU. Ni mambo machache sana ambayo yamebadilika. Na ni dunia nzima. Sio tuu Tanzania.

Kwa mwananchi wa kawaida anayeishi katika ulimwengu huu asitegemee mabadiliko makubwa sana katika maisha yake kwa kuitegemea siasa.

SISIEMU kama itaishiwa nguvu kama vile ukoloni wa wazungu ulipoishiwa nguvu na kuzeeka. Itajibandua na kujichubua ngozi, kisha lile gamba lenye title ya SISIEMU litaondoka na nyoka huyo atapata jina jingine ambalo kwa Watu wa kawaida wataona ni chama kipya cha ukombozi lakini kumbe ni kilekile kilichotokea kwenye ukoloni.

Kwenye utawala wa nyoka, demokrasia ni silaha muhimu sana ambayo inatumika kama nyenzo ya vyama kujichubua na kujifanya chama kipya ilhali ni kilekile.
Nyoka hupenda demokrasia na kusikiliza ili kujua nini kinachoendelea kwenye vichwa vya wanaowatawala.

Hii ni tofauti na mfumo wa kidikteta ambao sio mfumo sahihi wa nyoka. Zingatia, nyoka ni mwerevu hivyo kupitia demokrasia anajua yeye anauwezo wa kushawishi na anaakili za kilaghai.

Nyoka hapendi Udikteta, na mara nyingi Haki ndio huita Udikteta.

Mayai ya nyoka hutagwa kama warithi na wapigania urithi wa utawala wa jokamama. Hawa huzuga kama wanapambana na nyoka mkubwa lakini kimsingi ni ulaghai tuu.

Acha nipumzike sasa
 
Sisiemu sio rahisi idodondoke maana imejaa mikakati ya kupumbaza watu Kama ujio wa simba na yanga unauonaje.?
 
Sisiemu sio rahisi idodondoke maana imejaa mikakati ya kupumbaza watu Kama ujio wa simba na yanga unauonaje.?
Wanampumbaza nani tena? Siku za nyuma kweli waliweza kupumbaza watu maana ilikuwa ni kizazi chao. Kwa sasa uoga dhidi ya vyombo vya Dola ndio imebaki Kinga Yao. Siku uoga ukiisha ndio itakuwa kwaheri.
 
Back
Top Bottom