Nyoka na kujamiiana: Kwanini anakonda wa kike hummeza wa kiume baada ya tendo?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,882
155,863
Ngono ni jambo gumu. Kadiri tafiti zinavyofanywa kuhusu ngono, ndivyo mambo ya kushangaza yanavyozidi kuja.

Jesus Rivas ni mtaalamu wa nyoka anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mexico Highlands nchini Marekani. Hivi karibuni Jesus alijifunza jambo la ajabu kuhusu maisha ya ngono ya nyoka mkubwa anayepatikana Amerika Kusini, anakonda.

Anakonda mwanamke hula dume baada ya ngono. Hapo awali, wanasayansi waliamini kwamba nyoka dunme hutawala wakati ngono. Lakini habari hii kuhusu anakonda jike imewashtua. Kulingana na Jesus, hii ndiyo habari ya hivi punde ya kushtusha kuhusu kujamiiana ya nyoka.

Kwa viumbe wengine, wanaume ni wakubwa, wana nguvu zaidi, lakini katika kesi ya nyoka ni kinyume chake. Kwa nyoka aina ya anakonda, jike mara nyingi ni mkubwa mara tano kuliko dume. Kwa hivyo anaweza kummeza kwa urahisi.

Ukubwa wa nyoka wa kike humsaidia kutaga mayai zaidi na kuangua watoto. Kwa hiyo nyoka wadogo wa kiume hutafuta jike kama washirika wa ngono, lakini swali ni jinsi gani wanaweza kupata nyoka jike kwa ngono wakati nyoka hawaoni vizuri?

Utafiti umegundua kuwa hamu ya ngono inaonyeshwa kwanza na jike. Nyoka wa kike hutoa gamba lake anapotoka kwenye hali ya baridi kali au joto. Kisha hutoa homoni inayoitwa pheromone. Kutokana na hali hiyo, nyoka wa kiume huvutiwa kwa msaada wa homoni hiyo.

Kadiri jike anavyokuwa mkubwa wakati wa msimu wa kuzaliana, ndivyo homoni nyingi zaidi hutolewa kutoka kwa mwili wake. Kwa kumfuatilia, nyoka wa kiume humfikia nyoka wa kike kwa ajili kufanya ngono.

FRRERJJER

Nyoka jike anao uwezo wa kukaa na shahawa za nyoka dume mwili mwake kwa siku kadhaa

Kwanini nyoka jike hujamiana na madume wengi?​

Ikiwa hajaridhika na uhusiano wa kimapenzi na nyoka wa kiume, mara moja atamsukuma na kutafuta mwenzi mwingine. Sasa swali kubwa ni je, nyoka jike anaamuaje nyoka dume hafai au anafaa kufanya naye mapenzi?

Wanasayansi hawajaweza kupata jibu la wazi la swali hilo hadi leo. Inaweza kutegemea uwezo na tamaa ya nyoka wa kiume. Au jike anaweza kuwa anapata hisia ya nguvu za dume kwa uwezo wake wa kugusa.

Si lazima nyoka jike afanye ngono na nyoka mmoja tu. Nyoka wa kike wameonekana mara nyingi wakifanya mapenzi na nyoka kadhaa wa kiume. Kwa upande mwingine, nyoka wa kiume huwa waaminifu kwa jike anapokubali kufanya ngono. Hata nyoka wa kike anapolala, nyoka wa kiume huendelea kumzunguka.

Labda ni kuongezeka kwa hamu ya ngono au kwa kufanya ngono na nyoka kadhaa, nyoka wa kike huamua ni dume gani atakayezaa mtoto mwenye nguvu. La muhimu kujua ni kuwa, madhumuni ya ngono kwa nyoka ni kuzaa tu.

Jike ana uwezo wa kuhifadhi manii ya nyoka wa kiume katika mwili wake kwa siku chache. Huenda hiyo ndiyo sababu ya kufanya ngono na nyoka kadhaa wa kiume, akihifadhi mbegu za kiume ambazo zinaweza kutoa mtoto mwenye afya zaidi.

Tazama maumbile ya asili; nyoka za kike hutoa aina maalum ya homoni ya pheromone baada ya ngono mara kadhaa ili kutuma ujumbe kwa nyoka wa kiume kwamba hatafanya ngono tena. Hakuna anayeweza kumlazimisha nyoka jike.

Ndani ya njia ya uzazi ya nyoka ya kike hufungwa. Yaani hata nyoka dume akitaka hawezi kuzalisha kwa kufanya mapenzi na jike maana mbegu zake haziingii ndani.

Anakonda jike humeza dume baada ya tendo

TYUFGD

Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Sababu ya jambo hilo haijajulikana, lakini kifo cha nyoka dume kinaweza kuwa sababu ya kumpa anakonda jike mlo wenye lishe, kwani anakonda jike mjamzito hali wala kunywa chochote kwa muda wa miezi saba.

Mitindo wa ngono katika nyoka ni migumu kama wanadamu, lakini nyoka wana tabia sawa na buibui. Ni wakubwa kwa umbo kuliko nyoka dume, na ushindani mkubwa hutokea miongoni mwa nyoka dume wakijaribu kuvutia nyoka jike. Nyoka jike ana udhibiti kamili wakati wa kujamiiana na mara nyingi hula dume baada ya ngono.

Source: BBC Swahili
 
emoji3064.png
emoji848.png
 
Male species wote hatima yetu ni moja ama inafanana, aitha wanawake watuue ama watuletee maisha magumu tufe mapema.

Ndio maana sina huruma na wanawake, nawachakata kwa hasira sana, na nawachakata bila huruma.

Ikiwa bado una meno, kula mifupa, itafika muda mifupa itataka kukukula na hua haina huruma na wala haina kumbukumbu kwamba uliitendea mema.

Once you are a male species, bila kujali ni nyoka, mbwa, jogoo, binadamu ama nzi, wote mwisho wetu unafanana.
 
Kuna dada humu ndani alikuwa na shamba la majoka, kawafuga wengi sijui alikuwa akiwauza nje? Sikumbuki
Uzi huu hapa
 
😄 😄 😄 😄 😄 Kumbe hawaishii kula hela tu, kuna wanaokula wanaume kabisa😀
 
Ngono ni jambo gumu. Kadiri tafiti zinavyofanywa kuhusu ngono, ndivyo mambo ya kushangaza yanavyozidi kuja.

Jesus Rivas ni mtaalamu wa nyoka anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Mexico Highlands nchini Marekani. Hivi karibuni Jesus alijifunza jambo la ajabu kuhusu maisha ya ngono ya nyoka mkubwa anayepatikana Amerika Kusini, anakonda.

Anakonda mwanamke hula dume baada ya ngono. Hapo awali, wanasayansi waliamini kwamba nyoka dunme hutawala wakati ngono. Lakini habari hii kuhusu anakonda jike imewashtua. Kulingana na Jesus, hii ndiyo habari ya hivi punde ya kushtusha kuhusu kujamiiana ya nyoka.

Kwa viumbe wengine, wanaume ni wakubwa, wana nguvu zaidi, lakini katika kesi ya nyoka ni kinyume chake. Kwa nyoka aina ya anakonda, jike mara nyingi ni mkubwa mara tano kuliko dume. Kwa hivyo anaweza kummeza kwa urahisi.

Ukubwa wa nyoka wa kike humsaidia kutaga mayai zaidi na kuangua watoto. Kwa hiyo nyoka wadogo wa kiume hutafuta jike kama washirika wa ngono, lakini swali ni jinsi gani wanaweza kupata nyoka jike kwa ngono wakati nyoka hawaoni vizuri?

Utafiti umegundua kuwa hamu ya ngono inaonyeshwa kwanza na jike. Nyoka wa kike hutoa gamba lake anapotoka kwenye hali ya baridi kali au joto. Kisha hutoa homoni inayoitwa pheromone. Kutokana na hali hiyo, nyoka wa kiume huvutiwa kwa msaada wa homoni hiyo.

Kadiri jike anavyokuwa mkubwa wakati wa msimu wa kuzaliana, ndivyo homoni nyingi zaidi hutolewa kutoka kwa mwili wake. Kwa kumfuatilia, nyoka wa kiume humfikia nyoka wa kike kwa ajili kufanya ngono.

FRRERJJER

Nyoka jike anao uwezo wa kukaa na shahawa za nyoka dume mwili mwake kwa siku kadhaa

Kwanini nyoka jike hujamiana na madume wengi?​

Ikiwa hajaridhika na uhusiano wa kimapenzi na nyoka wa kiume, mara moja atamsukuma na kutafuta mwenzi mwingine. Sasa swali kubwa ni je, nyoka jike anaamuaje nyoka dume hafai au anafaa kufanya naye mapenzi?

Wanasayansi hawajaweza kupata jibu la wazi la swali hilo hadi leo. Inaweza kutegemea uwezo na tamaa ya nyoka wa kiume. Au jike anaweza kuwa anapata hisia ya nguvu za dume kwa uwezo wake wa kugusa.

Si lazima nyoka jike afanye ngono na nyoka mmoja tu. Nyoka wa kike wameonekana mara nyingi wakifanya mapenzi na nyoka kadhaa wa kiume. Kwa upande mwingine, nyoka wa kiume huwa waaminifu kwa jike anapokubali kufanya ngono. Hata nyoka wa kike anapolala, nyoka wa kiume huendelea kumzunguka.

Labda ni kuongezeka kwa hamu ya ngono au kwa kufanya ngono na nyoka kadhaa, nyoka wa kike huamua ni dume gani atakayezaa mtoto mwenye nguvu. La muhimu kujua ni kuwa, madhumuni ya ngono kwa nyoka ni kuzaa tu.

Jike ana uwezo wa kuhifadhi manii ya nyoka wa kiume katika mwili wake kwa siku chache. Huenda hiyo ndiyo sababu ya kufanya ngono na nyoka kadhaa wa kiume, akihifadhi mbegu za kiume ambazo zinaweza kutoa mtoto mwenye afya zaidi.

Tazama maumbile ya asili; nyoka za kike hutoa aina maalum ya homoni ya pheromone baada ya ngono mara kadhaa ili kutuma ujumbe kwa nyoka wa kiume kwamba hatafanya ngono tena. Hakuna anayeweza kumlazimisha nyoka jike.

Ndani ya njia ya uzazi ya nyoka ya kike hufungwa. Yaani hata nyoka dume akitaka hawezi kuzalisha kwa kufanya mapenzi na jike maana mbegu zake haziingii ndani.

Anakonda jike humeza dume baada ya tendo

TYUFGD

Si mara zote anakonda jike hula dume baada ya kujamiiana, lakini haijulikani ni wakati gani anakonda wa kike huamua kummeza dume baada ya kujamiiana.

Sababu ya jambo hilo haijajulikana, lakini kifo cha nyoka dume kinaweza kuwa sababu ya kumpa anakonda jike mlo wenye lishe, kwani anakonda jike mjamzito hali wala kunywa chochote kwa muda wa miezi saba.

Mitindo wa ngono katika nyoka ni migumu kama wanadamu, lakini nyoka wana tabia sawa na buibui. Ni wakubwa kwa umbo kuliko nyoka dume, na ushindani mkubwa hutokea miongoni mwa nyoka dume wakijaribu kuvutia nyoka jike. Nyoka jike ana udhibiti kamili wakati wa kujamiiana na mara nyingi hula dume baada ya ngono.

Source: BBC Swahili
Kwa upande wa nyuki , dume likishampanda jike/malikia ,linakufa muda huohuo
 
Back
Top Bottom