SoC04 Shule za msingi za serikali zifundishe masomo yote kwa lugha ya kingereza ili kuwatengeneza watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha hiyo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius Man

Member
Apr 7, 2024
39
42
Ni wazi unakubaliana na mimi kuwa kwa asilimia kubwa watoto wengi wanaosoma shule za English medium ni watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha ya kingereza kuliko wale wanaosoma shule za msingi za serikali, kwa kweli watoto wanaosoma English medium ni watoto wanaojua sana kingereza hasa kwenye upande wa kusoma na kuandika kuliko wale wa shule za serikali.

Katika uhalisia mara nyingi watoto wanaosoma shule za msingi za serikali, kwa asilimia kubwa huwa hawajui kusoma wala kuandika lugha ya kingereza, huku baadhi yao unakuta wanajua baadhi ya maneno machache sana ya lugha hiyo tena kwa kukalili, ambapo ni tofauti na wale wanaosoma shule za English medium ambao wanajua lugha hiyo kupita kiasi. Hali hii kwa asilimia kubwa naweza kusema inachangiwa na aina ya ufundishaji uliopo katika shule hizo za serikali, ambapo kwa mara nyingi shule hizo zimekuwa zikifundisha lugha ya kiswahili katika masomo yote kasoro somo la kingereza tu, ambalo pia somo hilo hufundishwa kama kwa kugusia tu tena unakuta ni kwa mara chache sana katika shule hizo. Hali inayopelekea asilimia kubwa ya watoto wa shule hizo za msingi za serikali kutokujua kuandika wala kusoma lugha hiyo, kwasababu ya kufundishwa kwa uchache sana, tofauti na wale wa shule za English medium ambao masomo yote hufundishwa kwa kingereza hali inayopelekea kuizoea zaidi lugha hiyo na kuifahamu zaidi.

Unakuta watoto wa shule za English medium wanakuwa wapo vizuri kweli kwenye kusoma na kuandika kingereza, kwasababu shuleni kwao wanafundishwa kila kitu kwa kingereza, mfano kwenye upande wa uandishi kila somo wanaandika kwa kingereza, alafu kwenye upande wa kusoma pia wanasoma kwa kingereza hali inayopelekea kuizoea zaidi lugha hiyo na kuifahamu kwa undani kuliko wale wa shule za serikali ambao vitu vingi hufanyika kwa kiswahili, kama vile kusoma unakuta wanasoma kwa kiswahili na kwenye upande wa kuandika huwa ni kwa kiswahili, alafu kwenye upande wa somo la kingereza wenyewe wanakuwa wanagusia gusia tu, hali inayopelekea watoto hao kushindwa kuizoea na kuifahamu lugha hiyo ya kingereza kwa undani hasa kwenye upande wa kuandika na kuisoma kwasababu kila kitu wao unakuta ni kwa kiswahili.

Kwa kweli unajua lugha ya kingereza ni lugha pana sana na inahitaji ifundishwe kweli kweli ili iweze kueleweka, kwasababu lugha ni yenye maneno mengi, lakini kama ikifundishwa mara chache inakuwa ni ngumu sana kuifahamu. huwezi kuielewa lugha hiyo ya kingereza kwa miujiza ni lazima kuwe na ufundishaji wa hali ya juu wa lugha hiyo ndipo utaielewa, endapo kama itafundishwa kwa uchache basi matokeo yake yatakuwa hasi na kama ikifundishwa kwa ukubwa na undani zaidi basi ni lazima itaeleweka na matokeo yatakuwa chanya.

Naweza kusema watoto wengi wa shule za msingi za serikali wanakuwa hawanauwezo mzuri wa kusoma na kuandika kingereza, kwasababu kwanza ufundishaji wake wa lugha hiyo ni mdogo sana, yani unakuta wao aina ya ufundishaji uliopo kwenye shule hizo kila kitu ni kiswahili, mfano mtoto kuongea na mwalimu wake kila kitu anaongea kwa kiswahili, kwenye kuandika ni kiswahili na kwenye upande wa kusoma ni kiswahili alafu lugha ya kingereza unakuta inafundishwa kwa kugusiwa gusiwa tu kwa mara chache sana, kwa kweli ni mara chache hata kumkuta mwalimu wa shule hizo akiongea kwa kingereza na wanafunzi, yani wao kila kitu ni kiswahili na kama ukiwakuta wanaongea kingereza labda wakiwa kwenye somo la kingereza tu lakini nje ya hapo ni mwendo wa kiswahili. Sasa kwa hali hii ni lazima kunakuwa na uwezekano mkubwa wa watoto wa shule hizo wengi kutoijua lugha hiyo ya kingereza ukilinganisha na wale wa English medium.

Sasa hali hubadilika kabisa watoto hao wanapoingia elimu ya sekondari ambapo huko hukutana na hali ngumu kimasomo kutokana na lugha wanayoikuta huko ni tofauti na ile waliyoizoea wakiwa shule za msingi, lakini hii inakuwa ni tofauti na wale wengine waliomaliza English medium wao wanakuwa wanaona kuwa hali ya sekondari ni ya kawaida alafu unakuta wanafanya vizuri sana kwenye masomo yao. Lakini wale waliomaliza shule za msingi unakuta tatizo lao lipo kwenye lugha hali inayopelekea wafanye vibaya kwenye masomo hayo ya sekondari kwasababu lugha kwao ni changamoto sana na siyo kwamba hawana akili hapana ni kwasababu walikuwa wakifundishwa lugha hiyo kwa uchache sana. Yani wao kila kitu kwenye shule zao ni kufundishwa kwa lugha ya kiswahili.

Kwa kweli ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwenye masomo ya shule za msingi za serikali kwa namna moja ua nyingine zinachangia watoto wanapoingia elimu za sekondari kufanya vibaya kwenye masomo kwasababu ya lugha, ukilinganisha na wale wa shule za English medium.

Mapendekezo
Kila mtu hapa anakubaliana na mimi kuwa ufundishaji wa English medium umekuwa ukiwaanda watoto wanaomaliza katika shule hizo kwaajili ya kukabiliana na elimu za juu hasa kwenye upande wa lugha ya kingereza, kuliko wale wa shule za msingi. Kwa mfano watoto hao kutoka kwenye shule tofauti wanapokutana kwenye elimu za sekondari, unakuta watoto wa English medium wanafanya vizuri kuliko wale wa shule za msingi kwenye upande wa lugha ya kingereza. kwahiyo ni wazi kwamba shule za English medium wanakuwa wanamuandaa mtoto kwaajili ya kukabiliana na elimu za juu, lakini kwa upande wa shule za serikali ni kama vile wanampoteza kabisa mtoto kwasababu kile wanachomfundisha siyo kile atakachokutana nacho sekondari, alafu mwisho wa siku tunakuwa tumetengeneza watoto wasiojua kusoma wala kuandika.

Nashauri katika masomo yote ya shule za msingi za serikali yafundishwe kwa lugha ya kingereza ili kuwatengeneza watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha hiyo, ili hata watakapoingia kwenye elimu za sekondari wasipate shida, tunapaswa kurekebisha hapo kwasababu wote tunafahamu kuwa sekondari kwa asilimia kubwa inatumia lugha ya kingereza, hivyo kuna haja ya kuwaanda watoto wetu kwenye shule zetu za msingi kwaajili ya hilo. tusijekuwa tuna wafundisha watoto lugha ya kiswahili kwa asilimia kubwa, alafu tuje kutegemea labda watoto hao watakapo kutana na lugha ya kingereza kwenye elimu za sekondari kuwa labda kutatokea muujiza wakati kumbe haiko hivyo. Kwahiyo nashauri kwenye shule zote za msingi za serikali zifundishe masomo yote kwa lugha ya kingereza.

Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo itakayokuwa na elimu bora yenye matokeo chanya, sio tunakuwa na elimu yenye matokeo hasi.
 
Uko sahihi sana,

Na pia, hata hizo shule za english medium hazifundishi kiingereza vizuri, wanafunzi wanaohitimu wakijua kiingereza ni wachache.
Nimepita huko, nimeona.

Ukizingatia kwenye nchi maskini kama yetu, kujua kiingereza kunaweza kukuongezea kipato kwa kiasi kikubwa na kukufunulia milango mingi ya fursa, sijui kwanini serikali haichukulii kiingereza kwa uzito....
 
Wajue kuandika kiingereza Ili iweje, fafanua vzr
 
Japokuwa una hoja na unatakiwa kusikilizwa ila maneno yamekuwa meeengi wakati lengo ni lilelile, asante kwa bandiko japo sio english medium zote watoto wanatoka wakiwa vzuri kwenye lvgha ya malkia, nyingine tia maji tia maji tu. Ntakupa vote yangu.
 
Thanks mkuu vote
 
Kwanza nimevote kwa roho safi kwakuwa sina baya hata ephen_ anajua

Pili kuna maoni kidogo ningependa kutoa,,umezungumzia umuhimu wa kujua lugha ya kiingereza ni sahihi kabisa lkn ningetegemea useme vitu kama maarifa mengi yanapatikana kupitia lugha hii mfano machapisho mbali mbali yapo kwa lugha ya kiingereza,vitabu vimeandikwa kwa lugha hiyo,,,kukua kwa sayansi na tekinolojia kunachagizwa sana na matumizi ya lugha ya kiingereza na mambo kama hayo hivyo kujua lugha hiyo ingekuwa ni chachu ya kuongeza ufahamu zaidi na kuongeza maarifa pia

Kwahiyo ungepitia humo ingekuwa bora zaidi

Lakini hongera sana kwa kuja na andiko lako hili,,kila la kheri
 
Asante sana kwa maoni yako,
 
Asante
 
Serikali imeshageuka kuwa wafanya biashara,,
Hawawezi kuweka mfumo wa kufundishia kwa english kwenye shule za serikali sababu utaua shule za private.

99% ya wazazi wanaowapeleka watoto kwenye shule za english medium ni sababu ya english,,
Sasa shule za serikali zikiwa kwenye mfumo wa english ni nani atakubali kutoa mamilioni kwenye shule za private?

Maana yake shule za private zitakosa soko.
 
Ni kweli kabisa Kiingereza haiepukiki,NDIO KiSWAHILI cha DUNIA...tunakihitaji kuliko kinavyotuhitaji..
Ni NYENZO muhimu katika kuhimili mikiki mikiki ya hii dunia

Kuwepo na waalimu wazuri,vitabu na kifundishwe ingali watoto bado wadogo,ikipendeza hata vidudu,kwa kuwa muda mzuri wa binadamu kujifunza lugha yoyote ni UTOTONi
 
Ni kweli kabisa Kiingereza haiepukiki,NDIO KiSWAHILI cha DUNIA...tunakihitaji kuliko kinavyotuhitaji..
NYENZO muhimu katika kuihimili mikiki ya hii dunia

Kuwepo na waalimu wazuri,vitabu na kifundishwe ingali watoto bado wadogo,ikipendeza hata vidudu,kwa kuwa muda mzuri wa binadamu kujifunza lugha yoyote ni UTOTONi
Kweli mkuu kingereza ni muhimu sana katika dunia ya sasa kila mmoja kukifahamu.
 
Serikali imeshageuka kuwa wafanya biashara,,
Hawawezi kuweka mfumo wa kufundishia kwa english kwenye shule za serikali sababu utaua shule za private.

99% ya wazazi wanaowapeleka watoto kwenye shule za english medium ni sababu ya english,,
Sasa shule za serikali zikiwa kwenye mfumo wa english ni nani atakubali kutoa mamilioni kwenye shule za private?

Maana yake shule za private zitakosa soko.
Kila mtoto anayohaki ya kupata elimu bora, kama tukiwa tunatanguliza tu biashara tutakuja kuzalisha watoto wengi wasiojua kusoma wala kuandika
 
Back
Top Bottom