Shule: Wapi nimpeleke mwanangu?


Semilong,

Na mimi nimechoka akili kusikia wazazi wa JF wanashabikia kitoto cha vidudu kufanyiwa "interview" ya kujiunga na darasa la kwanza. Kama unavyosema, wengine wanachelewa kuonyesha uwezo wao. Albert Einstein hakuwa genius darasani. Alifanya dead end jobs kabla ya kutulia na kuja na Nadharia Maalum ya Uwiano. Eti unamfanyia mtoto wa vidudu "interview." "Interview" ya kutathmini kama anajua kusoma na kuandika?

Kuna kitu umesisitiza, Semilong, kuhusu kufuatilia maendeleo ya mtoto. Nilitaka nikwambie tu, usije ukamfundisha mwanao maneno "hichi kitu," "hana hakili," "embu fikiria."

Hiki, akili, hebu.
 
...
If it was me i would have recomended Muhimbili primary school mbona nishule nzuri tuu

Hapo Muhimbili Primary School wanaanzia na elementary school? Na je kwa upande wa secondary, ukiacha IST, ni shule gani nyingine zinatumia mtaala wa nje ya Tanzania ambazo zipo Dar?

...
...wanafundisha kutoka na na mtaala huo huo wa nje ila sema wao kwa kiswahili.

Je Muhimbili nao wanatumia IB curriculum isipokuwa wao wanafundisha kiswahili?

Asante.
 
Anyway mimi nashindwa hata kushangaa hapa, watu mmeombwa ushauri /information zitakazo msaidia Max kuamua wapi ampeleke mtoto wake, sasa mjadala wa kama interview kwa watoto ni sahihi au si sahihi unakujaje hapa? kama tunataka kujadili hili ianzishwe thread nyingine, ila hapa tumpe ushauri /information itakayomsaidia Max kwanza.

Mkuu max,

Zingatia ushauri wa ndugu Maane, naungana naye 100% labda tu wadau wengine wakuletee shule nyingine za namna hiyo zilizopo mikoani pia ili upate a wider choice! Nyingine hapa zitakuwa ni bla bla tu ndugu yangu!
 

Mama,
Unaweza kujaribu Dar es Independent School.Ni same standard na IST( International School of Tanganyika) ila wao fees iko kidogo chini ukilinganisha na IST.Inaanzia from KG to High School - Form VI.
Many expatriates wanapeleka watoto wao pale na ni shule nzuri.
 
Mama,
... Dar es Independent School.... wao fees iko kidogo chini ukilinganisha na IST. Inaanzia from KG to High School - Form VI.
....

Nashukuru sana kwa maelezo muafaka kabisa. Asante kwa Mwanzilishi wa thread hii, na pia Maane na wengine waliotoa mitazamo yao.
 
Mama unaweza kujaribu shule kama Laurette.

Vile vile kuna shule ambazo ziko accredited na Council of International Schools
-Aga Khan Mzizima Secondary School(IB and IGCSE/GCE)
-Haven of Peace Academy(UK) CIS Members Directory
 
Max mpeleke MANZESE PRIMARY SCHOOL aende kuchangamka then sekondari kama ni binti mpeleke MARIAN GIRLS
 
Mie natafuta shule nzuri ya kawaida ya sekondari kwa ajili ya mwanangu wa kiume ambaye kamaliza form four na nahitaji kumpatia shule nzuri kwa ajili ya masomo ya A level.
Hizo international schools siziwezi, lakini kama kuna shule zingine nzuri zinazotumia mtaala wa hapa hapa kwetu danganyika naomba nifahamishwe. Naungana na Max, nahitaji sana!
 
Shule yenye rekodi nzuri muda mrefu (boarding na day) kwa Mwanza ipo inaitwa Nyakahoja Primary (shule iko chini ya masista). Fees should be very reasonable, bei zake sio za International level. Ila wengi waliopitia hapo wanafanya vizuri sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi.
Pia kuna Isamilo International School (Mwanza). Na kama walivyosema wengine St. Constantine (Arusha - International wannabees), ISM (Moshi na Arusha Branch) na IST. Inategemea na mfuko wako.
ISM na IST wanafanya IGCSE mpaka form 4. halafu 5 and 6 ni IB (fees bonyezeni kwenye website). Kama una mfuko, bania bania halafu jipinde umweke mtoto wako asome IB. Hapo utakuwa umemonita tabia ya mtoto wako mpaka umzogeze afanye IB. By the time unamweka IB unajua ur money is worth investing. Kama zinacharge, IB is the key to any university in the word! Marekani tena unaweza hata ukaruka modules au hata 1st year of University.

Nimepitia njia hizo, na ni kweli, kama mtoto wako hajatulia akili (hata kama ni bright), ataishia kuvuta bangi, ulevi, kubwia na kutoka kavu, na utalia investment yako. Hii haihusiani na shule, ni tabia ya mtoto tu kupapatika na freedom entrusted on them. Tabia ya kusema sijui shule inawaharibu au haiwadiscipline ni uongo. Inabidi watu tufike umri fulani tukubali responsibitilities zetu kama individuals, wazazi na familia etc. Kama mtoto anapapatika na bangi atavuta tu, nothing to do with the school.

Benefit ya IB, unakuwa multi-cultured. Unajifunza kuwa critical thinker. The freedom you are given to express yourself stays with you. Nothing phases you!! IB inakufanya uwe complete, una mix masomo yote more or less from arts to sciences, wewe unachagua masomo 3 ufanye katika higher level, na matatu katika subsid level, plus compulsory Theory of Knowledge and creatice action service (CAS - helps you be socially responsible to the society around you). Kama strength yako ni Sciences, unaweza chukua Physics, Chemistry, Biology/Maths at higher level, halafu unachukua economics, language etc at subsid level. Kama arts ni strength yako, unachukua arts at higher level, halafu sciences at subsidiary level. This is what makes IB hot katika university nyingi/anywhere in the world, maana you are a well rounded person (yaani hujafocus kwenye kusoma tu PCM au PCB etc ambayo kwakweli ina narrow ujuzi wako).

Lakini kama mfuko hautoshi, haiwezi zuia mtu yeyote kufika anakotaka. Pia unaweza usispend pesa kubwa mtoto wako akaparamia tu mabangi!! Life is about risks.

I highly recommend Nyakahoja, sijapita, ila naijua sana. Ni ya kikristo, ila waislamu kibao wamepita hapo. Nina marafiki wa kiislamu wamepita hapo, and they are the most objective Islamic people I know. Kwa waislamu, mimi na encourage upeleke mtoto wako katika shule hizi, na kama ndugu aliyeweka mfano hapo juu...wewe kama mzazi jua responsibility yako nyumbani kumfundisha dini yako, lakini jua anapata kisomo kizuri sana.
 

Asante kwa maelezo haya.
 
Yeah its damn expensive. My son wanted to join Moshi International school for Diploma 1 (that is what we call form 5) its UDS 16800 per year for borders. So if you are looking for that kind make sure ya pocket is ,,,, u know!
No EPA money please!

It is now usd-20,000+ for borders hii ni 2009/2010
 
Maane,

Mie mtoto wangu Muislam je watampokea ktk hizi shule?
Watampokea tu, dini sio kigezo cha kumregister mwanafunzi, wala usihofu kwamba ataondolewa relini. They are teaching academics subject and not religion subjects and mybe so moral stuff here and there!
 
"Interview" maana yake nini?

Kwa kiswahili maana yake ni usaili/kusaili.

Kimsingi wanataka kumhoji mtoto na kung'amua vitu (vipaji, uelewa nk) vilivyojificha ambavyo huwezi kuvijua kwa mtu kuandika au kuangalia rekodi nyingine. Kimantiki, sioni ubaya katika hili kwa sababu kwanza analinganishwa na watoo wa rika lake na sio watu wazima na pili inawapa walimu fursa ya kumfahamu mwanafunzi wanayetaka kum-enroll.

Nadhani kuna philosophical problem (si Tanzania pekee) kwa taasisi za elimu kuchagua wanafunzi wanaoonekana wana uwezo kiakili ili kujiunga na taasisi hizo.

Kama lengo la shule ni kuondoa ujinga, nilitegemea wale wanaoonekana wajinga zaidi ndio wapewe nafasi ya mwanzo ya kujifunza! Sioni mantiki ya shule kujisifu kufaulisha wanafunzi kama ilichagua wale wenye uwezo tu. Uwezo wa mwalimu/taasisi ya elimu unapaswa kupimwa kwa umahili wao wa kufaulisha wanafunzi ambao awali hawakuwa na uwezo (i.e. walikuwa wajinga)!
 
Mpeleke Alhassan Mwinyi Primary School, iko MIkocheni ni nzuri mwanangu anasoma pale darasa la nne.

Nenda kaone uchague
 


Mtoto wangu wa kiume alisoma St Teresa akiwa Primary, ni nzuri na alikuwa anafanya vizuri. Tatizo hawakuwa na Boarding ikawa inakuwa ngumu kuendelea kumuacha pale.

Mwaka au miezi 18 iliyopita waibadilishiwa Headmistress, sasa sijasikia iwapo ujio wa Head mpya umeboresha au umeshusha kiwango. Ni muhimu kufuatilia.
 


Walimu kumfanyia usaili sio tu kwamba wanapima uwezo wa mtoto. Mtoto wa miaka 5 akifanyiwa usaili ni kipimo kizuri kujua nyumba anayotoka ni ya namna gani. Walimu wanajua hali halisi kuwa hata kama utamfundisha vizuri namna gani, nyumbani nako lazima kuwe kumetulia katika kukuza ipaji. Tatizo ni kuwa wazazi wengi wa kitanzania tunapenda mno kukaa baa..!!
 
Kwa upande wa shule zenye mitaala ya nje ya Tanzania, International school of Tanganyika ni mojawapo.

Mwenye kujua zaidi kuhusu hii shule anaweza kusaidia.

Mimi nilifukuzwa hii shule nilipokua grade 1 for a very minor one-off offence. Nadhani I was 5 years old. Kwakweli hiyo dismissal ilikua unfair. When I look back, nadhani it had something to do with my race. Natahadharisha tu kama mtoto wako sio mzungu.
 
Unajua wengine hapa tulisoma shule za sikinde za watoto wa wakulima, lakini haidhuru tunaweza kuwa na mawili matatu.

Kuhusu hizo shule za academy kwa kweli sina idea..maana sikuwahi hata kudream kwenda huko. Kama Maane alivyosema nadhani kwa kweli sasa hivi kwa watu wa kawaida ambao uwezo ni mdogo, tegemeo kubwa ni SHULE ZA MAKANISA. Shule za mission ni nzuri sana. LAKINI inabidi ufuate masharti yao. Kama wewe ni dhehebu lingine inabidi uwe tayari mtoto wako kupewa maadili ya kikatoliki au kilutheri.

Personally nimesoma mission and I can tell you for sure. Iam who Iam today kwa sababu ya yale maisha na songombingo za mapadre NA Mabruda. Kusali kila asubuhi...kuimba nk..It was all good. So Max..sijui uwezo wako..kama uko safi unaweza kufuata ushauri wa wakubwa humu kuhusu hizi International Schools. Ila kama ndo uwezo mdogo..think shule za makanisa.

Ila kitu kimoja ambacho nimeona humu: Kwa kweli TANZANIA kadri siku zinavyokwenda thamani ya elimu inayotolewa na serikali inazidi kushuka. Maana hakuna hata mmoja aliyeshauri jamaa aende shule za serikali. Jamani wananchi we need to do something..otherwise watoto wetu watakosa elimu bora na watakuwa wapagazi wa hawa wanaoenda IST na kwingineko. I can tell, mtu wa Kigoma huo uwezo wa IST hana..sasa jamani something must be done to help this poor guy..na yeye aje kucompete na wengine.

Ushauri wangu: mpeleke mtoto shule ambayo utajua kabisa atapata maadili na elimu at the same time. Either of the two will be good for him/her
 
All in all, elimu inaanzia nyumbani.

Kama nyumbani kuna mazingira mazuri ya kumwezesha mwanafunzi kujisomea na kuelimika, mtoto atafanya vizuri shuleni. Kama mtoto analelewa na watu wanaopenda maarifa, hata shuleni atafanya vizuri.

Mazingira ya nyumbani yakikaa kielimu, mtoto atafanya vizuri hata akipelekwa kwenye shule ya kata. Lakini watoto wanaotokea nyumba za hovyo, hata apelekwe International school gani atachemsha tu.

Shule inaanzia nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…