Shule hii Mbeya iko wapi?

Shule hii Mbeya iko wapi?

Sasa hizi zinazojengwa miaka hii ni shule au maboma ya kukusanyia watoto maana hazina hata robo ya huduma kama shule za zamani,
Nilisoma pale Karatu shule iko powa hadi university uchwara za miaka hii hazifui dafu
 
hapo kwenye swiming pool alidondoka jamaa usiku alikuwa anakimbizwa kutokea uwanjani alipaa kama NINJA (mwanafunzi aligombana na raia kwenye chips,hatare)
 
Iyunga ndo ilikuwa ipi kati ya hizi?
Iyunga ni sekondari na bado ipo karibu na stesheni ya Tazara, hizi mbili hazikuwahi kuwa sekondari zilikuwa za kati (middle school) darasa la tano mpaka la nane.
Mpaka sasa L.A. (N.A.) Middle School haijulikani ilipotelea wapi! Shule lilikuwa nzuri ina madarasa, nyumba za walimu nzuri, bwalo kubwa la chakula, mabweni, karakana ya useremala, jiko, sickbay (chumba cha kulala wagonjwa),shamba la kahawa na kiwanja cha michezo.
 
hapo kwenye swiming pool alidondoka jamaa usiku alikuwa anakimbizwa kutokea uwanjani alipaa kama NINJA (mwanafunzi aligombana na raia kwenye chips,hatare)
Hahahaha..
Mkuu huyo mwanafunzi itakuwa aligombana na raia kule kwa big kama unaenda Must mana ndo zilikuwa chimbo zetu za kula kiepe.
 
Niliwahi kuona kwenye luninga mabweni yaliyoungua, nilisikitika na sikuelewa kwa vipi!
Babu shikamoo.
Ni kweli 2016 shule iliungua hata sisi wanafunzi hatukujua chanzo ni nni.Kipindi inaungua tulikuwa tumebakiza kama mwezi hizi kuingia nectar ya form six.
Nakumbuka matukio yote mawili yalitokea ndani ya mwezi mmoja mwezi wa 4 .
Kama jumatatu ya wiki hii bweni moja limeungua afu jumatatu ijayo pia bweni lingine liungue tena .
Ndo mambo yalikuwa ivo na mda ni ule ule saa 3/4 asubuhi.
Mwaka jana niliona picha shule imekarabatiwa imekuwa kama private sasa majengo yanavutia mno.
 
Nlisoma sangu sec ila nlitimuliwa
Sikumaliza miezi 3 wanapiga bakora balaa
Kulikuwa na mwl anaitwa kabigi na ndimbo
Wao utafikiri walinikamia

Ova
Mwalm ndimbo ticha wa biology RIP
 
Iyunga ilikuwa bonge la shule
Ila ilikuwa haimilikiwi na serikali kabla
Badaye ndy serikali nyerere wakaja itaifisha....
Shule mwanzoni ilikuwa na mpk swimming pool wabongo walipoichkua sehemu hyo wakaigeuza dampo ya kuweka uchafu

Ova
Hahahahahah daaah we Iyunga unaijua vizuri umesoma pale nini mkuu .

Shule ile wazungu waliiplan vizuri sana saivi imebakia gofu

Nasikia juzi kati wamekarabati na wamezungusha ukuta

Iyunga shamba la One
 
Nmesoma iyunga

Na swimming pool haijageuzwa dampo
Unesoma iyunga ya mwaka gani .

Mimi pia ninepita pale ile swiming pool ilijaa takataka na maganda ya miwa .

Wamafunzi wanakula sana miwa kwa babu kule.

Pia kuna maji yaliyotwama hadi vyura vimezaliana mule .

Sijui siku hizi kama wamepabadilisha
 
Wakati ninaondoka swimming pool, gymnasium, laundry, dispensary, dining hall na hot water heaters kila bweni pamoja na wanafunzi na walimu mnakula chakula pamoja kuanzia breakfast mpaka super. Enzi hizo tulikuwa tunalipa ada shs. 2,000/= (elfu mbili) sawa na kununua gari!
Hadi sasa Iyunga ni ya vipaji maalumu wale wenye ufaulu mzuri tu ndio hujiunga kidato cha kwanza hapo.
 
Hahaha mipata raha sana asee...hahha...hizo hot water heaters sijawahi kuziona hata mabaki yake nilipoenda kusoma pale...Swimming pool ilibaki shimo tu.

Laundry hii inaweza kuwa yale mabaki niliyaona kule nyuma karibu na jiko, karibu na mashine.

Chakula kula na walimu, hiyo haikuwepi kabisa,Msosi mbaya kabisa

Gymnasium, ilibaki jengo...tulikuwa tunaitumia tumia kidogo kama ukumbi (wa mtihani na viParty vidogo dogo) kiujumla ilikuwa imechoka, zile mbao chini zilikuwa ktk hatua zake za mwisho mwisho.

Dispensary...Sikumbuki ilikuwa upande gani,hahhaa...ila walikuwa kutengeneza ya kigumu tu pale bweni la Shaban Robert.

Dinning ilikuwepo, ila ilikuwa ndogo...tunakula tumesimama, wengine wanatoka kula nje kweny viunga vya maua.

Hahhaha, Najivunia kusoma pale.

Ila ikirudishwa siku nyuma niambiwe nikasome SIENDI.
Mkuu dispensary ilikuwa bweni LA Benjamin mkapa

Lile lenye vyemba vizuri liko kati ya shaban Robert na Luthuli
 
Ile swimming pool bora wangeifukia tu, kuna mwaka alikufa mtoto wa mwalimu pale kwa kuzama mule.... nakumbuka ilinivurugia plan za kung’oa mtoto wa Mung’ong’o.
Aisee kumbe wewe ulisoma enzi za mng'ong'o head master .

Nilikuwa pale enzi za KISUSANGE
 
Back
Top Bottom