Miaka ya hamsini mpaka baada ya Uhuru mji wa Mbeya ulikuwa na shule ya kati (middle school) iliyojulikana kwa majina ya N.A. (Native Authority) na baadaye L.A. (Local Authority).
Sifa kubwa ya shule hii ni kuweza kutoa viongozi wakubwa wa mashirika ya umma, viongozi hao ni Pro. Matthew Luhanga (makamu chuo kikuu Dar es Salaam), Linford Mbona (mkurugenzi ushirika la reli Tanzania) Elijah Bharuhan(sic) Luhanga (mkurugenzi mkuu Tanesco), Diamond Mwakyembe (mkurugenzi TBS), Nicholas Mbwanji (mkurugenzi NIT) , marubani wa ATC wawili ndugu Mwambapa! na wengine ambao nimewasahau majina, wote hawa ni wale waliondoka kabla ya mwaka 1964.
Kwa orodha hii inaonesha ni jinsi gani shule hii ya L A Middle School ilivyokuwa na viwango vya huu vya msingi wa elimu kuwawezesha kuinhia kwenye vyuo vikuu na kuweza kushika nyadhifa za huu nchini.
Kwa wenye kumbukumbu zaidi ninawakaribisha.