Shule hii Mbeya iko wapi?

Shule hii Mbeya iko wapi?

Ukipita uwanja wa mpira wa zamani nadhani ndipo hapo ilipokuwa hiyo shule. Miaka ya 83 kurudi nyuma na baada ya miaka unsyoitaja wewe palikuwa na shule (of course ilikuwa ya zamani sana) ilijulikana kana Mbeya Primary.
Kama sijakosea sana mwaka 1983 hiyo primary school ilifutwa na wanafunzi wakahamishiwa shule nyingine nadhani Mabatuni na Mapinduzi halafu pale pakaanzishwa shule ya Sekondari Meta.
Hapo sasa naanza kuelewa hivyo CCM iliichukua shule ya serikali! Haikubaliki.
 
Mimi nlisoma sangu form 1 miaka 90s
Tulidhuru hpo kimichezo
Ila kuna mzee mmoja alisomaga enzi hzo hpo iyunga ukicheki picha za kitambo kile shule ilikuwa kama iko mbele

Hata kibasila enzi hizo iko chini ya waghoaa ilikuwa nzuri
Ila mzee baba alipozitaifisha tu akashindwa ziendesha

Ova
Mkuu kama umesoma Sangu Sec School bila shaka utakuwa unayajua haya maeneo Msichoke Pub.. upande wa pili ukivuka barabara ya lami...kulikuwa na mishkaki na pombe za kienyeji hapo.....Savoi Bar...na Vamponji...moja kati ya maeneo ambayo tumegonga sana ulabu enzi hizo...
 
Siku hizi kuna bweni la Mkapa? Mimi kitambo nilitoka kulikuwa hamna bweni nilikuwa linaitwa mkapa kati haya ni lipi bweni limebadilishwa linaitwa mkapa? Mgabe,Lumumba,kawawa, S.Robert,Luthuli majina mawili ya bweni nimesahau moja karibu na mgabe kama unaelekea s,Robert na lingine opposite na kawawa.

Madom mengine ni Amri Abeid, Sokoine, State ya Juu na State ya Chini.... States zilikuwa bweni za wajanja ukiachilia mbali Mkapa ilipoungua.
 
Madom mengine ni Amri Abeid, Sokoine, State ya Juu na State ya Chini.... States zilikuwa bweni za wajanja ukiachilia mbali Mkapa ilipoungua.
Kati ya bweni zote Luthuli A ndio baba lao
 
Some memories from iyunga
Screenshot_20190525-143536_1558784236903.jpeg
15.jpeg
20.jpeg
11.jpeg
 
Luthuli A hiyo.... Kushoto unaweza liona bweni la mkapa au disp zamani
Screenshot_20190525-144140_1558784564548.jpeg
 
Asante kwa picha hizi, naiona main hall, haikujengwa kiswahili lilikuwa na jukwaa kubwa lenye pazia kubwa, nakumbuka kikundi kimoja cha utamaduni toka Guinea kiitwacho Djoriba kilikuja kutumbwiza hapa, ni kikundi cha serikali kama tulichokuwa nacho Tanzania, pia naona mabweni mimi nilikuwa la kushoto kuelekea madarasani nilikuwa kwenye chumba cha attachment watu watatu, kuelekea kulia dining hall na bakery.
 
Mkapa ni bweni lipo nyuma ya Luthuli. Kama unaweza kuvuta picha, kuna jengo lilikuwa kule Karibu na Luthuli.

Pia kuna jengo jipya lilijengwa mbele ya Luthuli, linatizamana na mlango wa Luthuli...Lile niliondoka lilikuwa bado halijaanza kutumika.
Lile jengo lilitumika miaka 2 kama sikosei.
Lilishaanza kuharibika.
Labda baada ya huu ukarabati mpya ndo limeanza kutumika.
 
Sasa niwape mpangilo wa mlo kwa siku.
1. Breakfast: yai, mkate uliochomwa (toast), maziwa,uji, silesia za mkate, jamu, siagi.
2. Saa nne asubuhi: chai ya maziwa, keki, cocoa, silesi za mkate na maziwa, uchag nouzi ni wako mezani.
3. Chakula mchana: viazi mviringo ( kila siku mpiko tofauti) nyama ( kilasiku mpiko tofauti) silesi ya mkate, ndizi mbivu na pudding.
4. Saa kumi: keki, maziwa, Silesi za mkate, cocoa, chai ya maziwa.
5. Chakula cha jioni: supu, wali njegere au nyama roast, au chips au mchanganyo wa kihoteli wapishi watakavyokuwa wameandaa, Silesi ya mkate, jamu, siagi,chai ya maziwa, karanga zilizokaangwa.
Kutokana na uandaaji huu lilikuwa hakuna sababu walimu kula majumbani mwao labda tu akipenda, je, tumesonga mbele kimaendeleo au tumerudi nyuma.
Tumerudi nyuma babu.
Tena hatau kumi nyuma ..daaah
 
Hahahaa...Daaah! Naomba nijibu kwanza tumerudi nyuma.

Sie ratiba ya msosi ilikuwa kama jeshini

Toka kuamka, mnafanya usafi...mnaenda Assembly, mnaenda darasani (hapo hatujala kitu).

Tunatoka Darasani Saa Tano na Nusu asubuhi...Tunapeleka vikombe kwa ajili ya kunywa uji (na hapo uji unaweza usiupate, kuna wakt uji hautoshi, wakt kikombe kinaibiwa)...Kunywa huo uji inaweza kuwa mpaka saa sita mchana ndo tunaanza kunywa)

Saa Nane mchana tunatoka Class, ila kula msosi iliweza kutukuta mpaka Saa kumi ndo tunakula....msosi full ugali maharage, sometimes wali, sometimes makande, sometimes nyama (nyama ilikuwa mara moja au mbili kwa wiki).

Jioni ugali harage.

Noma sana.
 
Ilikuwa ya wazungu ila baada ya uhuru tukawa wanafunzi wa mwanzo kusoma hapo, idadi kubwa ya walimu walikuwa ni wazungu na wanafunzi pia pamoja na wahindi wengi zaidi na waafrika.
Basi mzee wazazi wako walikuwa na uwezo wa kifedha
 
Back
Top Bottom