Shule bora za Serikali, enzi hizo

Shule bora za Serikali, enzi hizo

Hizi ni shule ngumu..
Ukitoka hapo ww ni jembe.
 
Aisee mbona mademu wetu wa Ashira Hawapo...?
 
Lakini kuanzia miaka ya 2010, yaani uchakachuaji era, kuna vishule vingi modern vimekuja juu ambavyo tunaweza kusema viliondokana na u-conservative wa shule tajwa hapo juu. Hizi shule kuiba mitihani ni jambo la kawaida, maadili sio ya kitanzania tena, ni western. Eg wanafunzi wa kike kuvaa wig na akatinga class ni suala la kawaida tu.
 
Katika hizo shule ulizotaja kuna hata moja ada inazidi milioni? Unaipima akili kwa kusoma shule za bei rahisi. Badilisha title ya thread yako IWE KAMA UMESOMA KATIKA SHULE HIZI BASI WEWE NI MASKINI.

Wajanja waliosoma Loyola, Cambridge , St. Marrys, Makongo, Jite ya enzi hizo, St. Anthony ya miaka hiyo, FEZA boys na nyinginezo nyingi.

Hizo shule ulizotaja hakuna chochote cha maana zaidi ya kujifunza kunywa MATAPUTAPU katika umri mdogo.

KIPIMO HALISI: Angalia tuu mlivyojazana humu JF lazima mtakuwa na kasoro tuu. Au MAPIMBI SQUARE
 
Nashangaa cjui anaiachaje NJOSS. Ilikua maarufu sn mkoa wa iringa, Tosa na ifunda zilkua haziifikii Njoss. Km nauona ivi msitu wa ndovu apo nalala dom3 gorofan kabsaa

...hahahaa Njoss ya lini ? nawakumbuka akina dengeya mwanyigu and team. Msitu wa ndovu, golani, Dom six.....
 
Mkuu...
Kweli wewe hukufaa kuingia kwenye hii list,unaleta hoja kwa mbwembwe bila kufikiria kuwa shule zoote tajwa hapo juu ni kutoka TZ...uganda inaingiaje hasa....!!???
Kweli ww ni k.l.z!!!!

Heading inasema "Kama hukupita katika moja ya shule hizi jua wewe ni Kilaza", alipaswa aanze na " kama ulisoma shule za Tz na hukupita katika shule hizi jua wewe ni Kilaza ".
 
Mleta uzi alipata Div III. Hana lolote!
 
Asee umenikumbusha enzi zile ukifaulu kwenda sekondari inakuwa ni sifa kubwa kwako,familia mpaka mkuu wa shule. Kila ukikutana na mtu mzima ni ushauli wakusoma tu.
 
Je ni sisi ambao maisha yetu yote tumesomea shule za nje ya nchi, bara la Asia na bara la ulaya tupo kwenye kundi gani?
 
Unaijua Geita Sec(GESECO) au unaisikia tu!? hapo kama ni mtoto wa mama ulikuwa unakaa siku moja na kuacha shule.
 
...kaangalie kwenye matokeo ya form six ya mwaka jana au juzi nadhani hakuna hata moja ya hizo kwenye 50 bora. Ilboru ni ya hamsini na tatu na ndo inawaongoza Wa serikalini. Ingawa Mimi nimo katiyazo, hamnamo kitu anymore....

Ila Kibaha na Mzumbe still zinafanya vema
 
Nashangaa cjui anaiachaje NJOSS. Ilikua maarufu sn mkoa wa iringa, Tosa na ifunda zilkua haziifikii Njoss. Km nauona ivi msitu wa ndovu apo nalala dom3 gorofan kabsaa

Njoss ilikuwa inaipita kidugara seminary?
 
Duh! umenikumbusha Kigoma Secondary miaka ya 1980. Mwl Lwinga, Mutobesya, Mngodo chini ya uongozi wa Mazigo (rip) na Chaka. Wakati huo Tabora yupo Msemakweli. Ilikuwa raha sana.
 
Hizo shule ni kwa zaman siku hizi zimechoka ukipeleka mtoto huko tarajia ataondoka na zero,kwamfano;kwiro secondary mwaka huu kwamatokeo ya advance imekuwa ya mwisho kitaifa.Peleka mtoto wako private schools kama unataka apate elimu bora kwasasa,hiyo Azania secondary nayo iko hoi sasa kwani niliwahi kufanya field ya kufundisha pale yaan wanafunz wa pale sasa ni wakawaida sana hawana tofaut na wanafunz wa shule zingine za kat
 
Mimi nilisoma miaka ya tisini kilimanjaro na nilibahatika kuzifahamu shule nyingi tu. Nachokiona hapa wewe umeamua kutaja tu majina ya shule unazozikumbuka lkn si kweli kwamba hizo shule tajwa hapo ndio zilikuwa bora.
 
Embu acha izo mwanawane unanikumbusha mkuu mmoja anaitwa Mbanga, nyie acheni bana. Embu lowassa aingie mdarakani aturejeshee mashule dezaini hii maana naskia jamaa kapania kweli..

Kuanza kufikiria kurudi nyuma kwenye enzi za wilaya nzima kuwa na shule moja ya sekondari au hakuna ni mawazo ya kimaskini sana!!

Shule hizo chache nchini zisizozidi hata 50 ndo tumefanya watanzania wengi kukosa fursa za kusoma na sasa ni maskini!!

Hebu angalia walau katka hii miaka 15 iliyopita ambayo shule za sekondari na vyuo vimeongezeka, utaona kabisa vijana wengi walau wamepata maisha mazuri, wanaweza hata kujenga na kununua usafiri kuliko enzi za shule chache mnazoziabudu hapo juu!!!

Eti Lowassa aje azirejeshee heshima!! Heshima gani mnayotaka azipe!! Tunataka usawa na fursa sawa za elimu sio ubaguzi uliotupatia majizi machache yanayoitafuna hii nchi kwa sasa!!!

We need more schools and universities! Sio ujingaujinga wa vishule hata havifiki 50 nchi nzima.
 
Back
Top Bottom