Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

Ni vigumu wewe kuufikia umma kivyakovyako na ukaaminika au akapewa much attention.
 
Ninaushahidi pia niambieni nitumie njia gani umma ufahamu ukweli kwani ndugu yangu aliuwawa na hakuwepo karibu na kituo kama taarifa ya polisi inavyosema M.50 karibu na kituo jamaa alipigwa risasi na polisi tena anayemfahamu kwa sura na jina zaidi ya kilomita 2.5 kutoka kituo cha polisi.
pole sana Mangi!!

Inauma ana kuona ngudu zetu wanopotea wanachukuliwa kama mitaji ya malumbano bungeni
 
Ninaushahidi pia niambieni nitumie njia gani umma ufahamu ukweli kwani ndugu yangu aliuwawa na hakuwepo karibu na kituo kama taarifa ya polisi inavyosema M.50 karibu na kituo jamaa alipigwa risasi na polisi tena anayemfahamu kwa sura na jina zaidi ya kilomita 2.5 kutoka kituo cha polisi.
si mmuwinde au hamjui anaishi wapi? kuna mwingi nilimwona akitawanya risasi kama hana akili alikuwa amevaa kiraia ndiyo huyo....
 
huyu mama kaanza vibaya sana . Wiki mbili tu ameshaonyesha dalili za wazi za kulishindwa kuliendesha hili bunge. Sipati picha miaka mitano ijayo itakuwaje kuwaje
We ngoja tuone itakuwaje ukweli utajulikana tu. Hawa CCM wanavyofanya mambo wanafikiri bado Watanzania ni Wajinga ngoja wasubiri kitakachotokea mbele ya safari CDM kazeni kamba tupo nyuma yenu.
 
ukweli unabaki pale pale waziright mkuu hajalidanganya bunge na hawezi kudanganya kwani katika uchaguzi wa wilaya ya hai chedema imemtumia mbunge ambaye siyo mkazi wa halimashauri hiyo

Una maanisha kama Chadema wamevunja sheria Hai basi ni sawa CCM kuvunja sheria Arusha Mjini? If ur answer is yes; Hii itakuwa matope
 
Anna Makinda ..heshima kwako..... usipende kuanzisha vita ya mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo
 
Nishaurini ninao Ushahidi wote wa mauaji ya wananchi Arusha,ninataka watanzania wajue ukweli ili tujue Lema na Pinda nani Mwongo nitumie njia gani kufikia umma.Pinda amepewa ushahidi na polisi ambao walisha edit hivyo anafikiri yeye yupo sahihi wakati amejipalia makaa ya mawe kichwani.
Peleka YouTube au Megaupload...., tena ili wasijue IP address yako mtumie jamaa yako abroad UK, US Germany au France na yeye aende kwenye Internet Cafe aweze ku-upload..., hakuna mtu anayeweza kuitrack back to you
 
Mimi naona kama utetezi ndo umeegemea kwa Marry mtashindwa vibaya, Hebu tupeni defination ya neno mkazi, kabla hamjaenda mbali. Ili mtu awe mkazi inambidi awe ameishi maeneo hayo kwa kipindi kipi? je neno mkazi lilotumiwa hapo linahusiano gani na mkazi kwa maana ya mimi mtanzania na mkazi foreigner utofauti wake upo vipi?

Lema asubiri rungu la bunge tu, hizo zote ni blaaa blaaa tu
 
Hakuna kitu cha namna hiyo hapa bongo, lema kaambiwa apeleke ofsni

Hapa speaker amefanya kitu cha mbolea mana angepoteza muda wa watanzania

Duh! comments nyingine unaweza kujiuliza wagonjwa wa mirembe wamepewa internet access?
 
Mnyika kamkumbusha mama kuhusu kiporo cha Lema, Mama kamwambia Lema apeleke maelezo kwa maandishi (Sijui kama itakuwa ofisini kwake au au wapi)

Anasikitisha sana, kukurupuka kutamcost sana, mpaka kakumbushwa!!! nahisi alifikiri kila mtu bongo lala, na bado tunamgoja Lema atakapoita waandishi wa habari.
 
mkama hata kama akiwa mkazi wa manispaa ya arusha bado siyo mbunge wa kuteuliwa na raisi na wala si mmbunge wa mkoa wa arusha !
yeye ni mbnge wa mkoa wa tanga.
hapo our cry boy lazima amwage chozi tu! and of coz tunajua watachakachua lakini ukweli unabakia pale pale kuwa jamaa alilikoroga!
 
jEYKEYWAUKWELI YOU HAVE A VERY WEEK BRAIN! Suala hapa si brabra ni kuwa kosa lilifanyika na ama watendaji waliompatia PM majibu ambayo ni ya uongo hata akasema uongo bungeni ama Spika naye alikurupuka kudhani atamkomoa Lema, nimesema ktk post yangu juu kuwa busara ya jambo hili bila ushabiki, litatuliwe kiutuuzima na pengine watu wazima wamejua athari hizo ndo maana wameona si busara Lema kuwasilisha bungeni lingeleta taathira mbaya. Think as great thinker siyo shabiki. Hata kama ni Mwana CCM lazima kujua kuwa Umeya wa Arusha utatenguliwa na Mahakama kwani Mary Chatanda si diwani wa Arusha kwa mujibu wa Sheria ya serikali za mitaa na Mabaraza ya Miji. Hili lilisababishwa na uvivu wa kufikiri na kujipanga CCM uwezo wa kuchukua Umeya Arusha ungefanikiwa kama Mh Kikwete angeamua pengine kumteua Bi Batrida Burian kuwa Mbunge. Kwa Chatanda walikosea na hii ni sababu ya kutowatumia wataaalamu kwenye Chama na badala yake kukurupuka! Suala la Pinda Bungeni limeleta fedheha hata kwake, Pinda si tunayemjua asingekubali fedheha hizo, alilishwa kasa na watendaji na mi nadhani hapo anapaswa kuipitia repoer yote ya tukio la Arusha na kutaka ukweli zaidi ama atumia usalama wa Taifa wampatie taarifa za kweli. Styre hii aliitumia sana marehemu Edward Moringe Sokoine na hata Magufuli anaitumia japo pia Magufuli wakati mwingine ana mfumo wake wa kuapata na kutafuta taarifa ili kuwa na taarifa kamili bila hivo ina maana uanze kusoma wewe mwenyewe hakuna muda japo pia utamaduni wa kusoma vitu basic kama hivi hasa kwa muda mgogoro wa Arusha ulipoanza angeshakuwa na kujua ukweli upo wapi. Wtatue kiutuuzima na sisi watu wazima tutajua tu kama halijasemwa wazi basi imejulikana nani alidanganya na itajulikana kuwa kati ya hao wawili atakuwa nani ambaye amefanya suala hilo liseiwekwe wazi ni Lema ama PM ... WAKUBWA TUTAJUA na tunajua atajirekebisha kama binadamu ila si kama Spika alivosema kuwa PM hawezi kudanganya......Mi namwomba mama Makinda alinde heshima ya mwanamke.....asitekeleze matakwa ya watu..........ndoto zetu za kuwaamini wanawake zitakimbia na itakuwa amewachimbia wanawake wenzie kaburi ambalo kufukuliwa kwake ni siku ya ufufuko ama siku ya kiama. Jifunze na UGENDELAGE LUDODI, LUKAFU LULADENYEKA!

Mkuu unapoteza nguvu za bure kumjibu huyu jamaa..mpuuzie!
 
lema kaambiwa awasilishe riport yake kwa maandishi alafu spika ndio atajua jishi ya kuendesha mjadala,kama atasoma yy au watachangia haijajulikana


 
hivi kwaida si unasoma ripoti au utetezi kwa kinywa chako halafu ndio unakabidhi maandishi...? au mimi ninakosea
 
Back
Top Bottom