Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

Show ya Lema vs Pinda featuring Makinda

.
Utashangaa mama kuja na jibu la kupiga chenga ya mwili.
Atasema busara ya bunge imeona kuwa suala la Arusha lipo mahakamani hivyo kuweka ushahidi hadharani ni kuingilia mamlaka ya mahakama.
.
Kama ulikuwepo vile!
 
Sorry wakuu, kuna anayeweza kunisaidia, aniwekee point to point alichodanganya Pinda na "ukweli" wa Lema. maana nimepita post na thread nyingi watu hawasemi wanadai Pinda na Makinda wataumbuka tuu. Sikusikiliza bunge siku hiyo tafadhali help
 
lema atawasilisha ofisini kwa speaker:coffee::coffee::laugh::laugh:

Kama Mh. Spika angetaka ushahidi wa maandishi basi angemwandikia barua Mb. Lema awasilishe ushahidi huo ofisini na kusingekuwa na haja ya kumuamuru ndani ya bunge. Sasa kwa kuwa amri yake aliitoa hadharani tena mbele ya luninga na kila mtu aliyetazama kipindi kile alishuhudia busara ya kawaida inataka Mb. Lema awasilishe kwa njia ileile ya hadharani ili wote tushuhudie.
 
Leo Anne Makinda ameanza kwa stahili ya kujidai kuwaelewa CDM kwa kuanzia kutetea uamuzi wa Mbowe kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri vivuli ambalo halikuhusisha chama kingine kama CUF, UDP, NSSR na TLP. Leo amejidai kuwaelewa sana CDM kwamba kufanya hivyo kanuni zinaruhusu.

Kufanya hivi nimehisi ni style nyingine ya kuwaambia CHADEMA jamani yaishe bwana hasa lile suala la Lema msijaribu kuleta ushahidi jamani mtatuua mwe mwe.!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kumbe na wewe ulimuona alivyokuwa anatoa uteteze wakati hakukuwepo na mashitaka ee? Nilitarajia aseme labda alipokea kimeseji kwamba Mbowe amekiuka taratibu lakini wapi. Kamfagilia weeee na kaifagilia chadema weee na akawapongeza mawaziri vivuli weee. Tena akato maagizo wasimame wapigiwe makofi. alipoona makofi hayatoshi tena akauliza mbona hamshangilii.

Nilijua tu kwamba hapo nguvu ya umma itakuwa imemkamata pabaya. Na huyo John Mnyika naye bana. Ndiyo maana kweli Shibuda alisema vijana hawana busara. Mama wa watu alishaomba msamaha kiutu uzima na kufunika taarifa ya Lema lakini yeye akajifanya kuja na kanuni. Sasa kamsuta mama wa watu bure. We Mnyika kwani kule kwenu hakuna wamama?
 
Tulitegemea kama alivyosema Spika kwamba Lema atawasilisha utetezi wake leo asubuhi. Baada ya kuonekana hataki kutoa nafasi kwa Lema , Mh. mnyika alimwuuliza swali la kumpa mwongozo wa kwa nini hajamtaka Lema atoe ushahidi. Anna Makinda alimemjibu kwamba ataleta kwa maandishi na yeye Makinda anajua jinsi ya kuongoza bunge anavyojua. Inaonyesha Makinda ametuliza mpira kusoma ramani kwani ameshaambiwa alikurupuka na asipokuwa makini itakula kwake. Hivyo ameonyesha kugwaya kwanza kwani nani asiyejua Mkuu alidanganya na CDM wana evidence nzuri zaidi kuliko Mzee pinda.

Do I smell arrogance from the answers given by Madam Speaker?.
 
Wlijua wakipiga biti jamaa watarudi nyuma kudadadek,

Wanadhan watanzania wanawachagua wabunge masoro kama zamani, Haina kufuta kauli mpaka mtoto wa peasant arudi kwao namanyele akasumbe wanga wake wa maneno huko!,

Makinda - Kinda = Kinda na kinda maanake ni Mtoto! (aache utoto asikurupuke hapo wnaongelea maisha ya watanzania)

Kama vipi arudi kwao Makete
Kwao njombe
 
Kwa kawaida hoja inayowasilishwa Bungeni na kujadiliwa inaamriwa kwa kura. Na kwa sababu wabunge wa CCM ndo wengi Bungeni ni dhahiri kuwa wangekuwa na uwezo kuwamua nani mwongo, na kwa vyovyote vile Lema angeibuka mwongo. Hata hivyo, uamuzi wa ccm siyo uamuzi wa wananchi, ccm wanajua wanamwakilisha nani Bungeni. Kama Lema angepata nafasi ya kulielezea Bunge na umma upande wa pili wa kauli ya PM pengine ingezidi kuongeza kina cha kaburi lao. LAKINI HATA KIMYA NI MAJIBU, wenye akili watajua tu.
 
the submission is tight. I hope they wont set it for voting coz they will be making a big mistake.
 
Soma hii ya Deus, Tanzania Daima, nimeipenda;

FEBRUARI 10 mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari, kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Jambo hili lilitokea baada ya Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (CHADEMA), kuomba apewe mwongozo wa spika “kuhusu utaratibu” aliohisi unakiukwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, wakati akitoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha Januari 5, mwaka huu.

Pinda alizungumzia vurugu hizo za Arusha wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua serikali ina msimamo gani kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi wakati wa vurugu hizo.

Akijibu swali la Mbowe, Pinda alilieleza Bunge kwamba chanzo asilia cha vurugu hizo ni uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa umeya mjini Arusha, wakati “utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

Kufuatia kauli hiyo na zingine zinazofanana nayo, Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika “kuhusu utaratibu” wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mbunge wa kawaida endapo kiongozi mkubwa wa nchi kama Waziri Mkuu amelidanganya Bunge.

Baada ya kuombwa mwongozo huo, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, Spika Makinda alisema: “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; waziri mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?”

Kisha, Spika alimpa siku tatu Lema ili awasilishe kwa maandishi utetezi wake wa kuthibitisha kwamba waziri mkuu alisema “uongo” bungeni siku hiyo.

Katika muktadha huu, tunakusudia kufanya mambo mawili. Kwanza ni kuonyesha kwamba ni kweli kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo bungeni ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Na pili tunataka kuonyesha kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema.

Waziri Mkuu alisema uongo: Meya wa Arusha si halali
Kwa lengo la kuonyesha kwamba Waziri Mkuu alisema uongo bungeni, inatosha kutoa ushahidi utakaokanusha usemi ufuatao kama ulivyotolewa naye bungeni: Kwamba, “Utaratibu uliofuatwa katika kumpata meya na naibu wake ni sahihi kabisa”, kwa maana kwamba “Meya wa Arusha yupo kihalali.”

Hapa inatosha kabisa kuonyesha kwamba miongoni mwa wajumbe waliompigia kura ya ndiyo “Meya wa Arusha”, yupo angalau mjumbe mmoja ambaye hakuwa na haki ya kisheria ya kuingia na kupiga kura hiyo. Na huyo si mwingine, bali ni Mary Pius Chatanda, ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Mkoa wa Tanga. Utetezi unafuata.

Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) ” (Local Governments (Urban Authorities) Act) ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda atakuwa ni mjumbe mwenye sifa ya kisheria ya kupiga kura katika vikao vya Manispaa ya Arusha kama atatimiza sifa mojawapo kati ya sifa tano zifuatazo:

Kwanza, lazima awe ni miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(a)). Chatanda hakuwa miongoni mwa madiwani ambao ni “wajumbe waliochaguliwa katika kata zilizomo katika Manispaa [ya Arusha]”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa meya wa Arusha.

Pili, lazima awe ni “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana” (Tazama ibara ya 19(2)(b)). Chatanda hakuwa “mbunge anayeliwakilisha jimbo la uchaguzi ambamo manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Tatu, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(c)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyechaguliwa (na chama) kutoka katika mkoa ambamo Manispaa [ya Arusha] inapatikana”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Nne, lazima awe ni “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais” na kwa mpigo awe “ni mkazi ndani ya eneo la manispaa [ya Arusha]” (Tazama ibara ya 19(2)(d)). Chatanda hakuwa “Mbunge wa Taifa aliyeteuliwa na Rais”. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Na tano, lazima awe ni miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI ambaye katika uteuzi wake [amezingatia] makundi maalumu kama vile watu wenye ujuzi maalum, watu waliotelekezwa na watu walio katika mazingira magumu.” (Tazama ibara ya 19(2)(e)). Chatanda hakuwa miongoni mwa “wajumbe wasiozidi watatu [waliochaguliwa] na Waziri wa TAMISEMI. Kwa hiyo hakuwa na sifa hii wakati wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

Hivyo basi, Kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya “Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji)” ya mwaka 1982, kama ilivyofanyiwa marekebisho bungeni mwaka 2006, Mary Pius Chatanda hakuwa na sifa yoyote ya kisheria ya kuingia katika kikao cha Manispaa ya Arusha na kupiga kura kama alivyofanya. Baraka za chama chake haziwezi na hazipaswi kubatilisha sheria za nchi.

Tena tusifananishe uwepo wa Mary Pius Chatanda na uwepo wa Rebecca Mngodo katika kikao kilichofanya uchaguzi wa Meya wa Arusha. Kufanya hivyo ni kufananisha maembe na machungwa. Mngodo ni mbunge viti maalumu aliyepatikana kupitia mkoa wa Arusha kupitia CHADEMA. Na hatimaye alipangiwa kazi na chama chake kufanyia kazi katika Mkoa wa Arusha. Kwa hiyo alikuwa na sifa zote za kisheria za kuwemo katika kikao kile.

Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema
Na sasa, tuone ni kwa nini Spika Makinda hakumtendea haki Godbless Lema. Kabla ya spika kumnyima mwongozo “kuhusu utaratibu” wa kikanuni, spika alipaswa kufanya tafakari kadhaa kuhusu Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi yetu.

Kwanza, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(1) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za siku hadi siku zinazofanywa na vyombo vya dola katika Jamhuri nzima. Pili, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 52(2) ya Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni “Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni”.

Tatu, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 62(2) na 66(1) za Katiba ya nchi, Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) ni mjumbe halali katika vikao vya bunge kupitia kofia yake kama mbunge wa kuchaguliwa.

Nne, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Waziri Mkuu (Mizengo Pinda), kama ilivyo kwa Mbunge mwingine yeyote, anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha tu.

Tano, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(3) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema) anaweza kusimama mahali pake na kuomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni; na kwamba baada ya kuruhusiwa na Spika, anaaweza kudai kwamba, Mbunge aliyekuwa anasema kabla yake (kama vile Mizengo Pinda) ametoa maelezo ya uwongo kuhusu jambo au suala alilokuwa analisema bungeni.

Sita, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), mbunge anayeomba mwongozo “kuhusu utaratibu” uliokiukwa bungeni (kama vile Godbless Lema alivyofanywa), atakuwa na wajibu wa kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.

Saba, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(5) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika au Mbunge mwingine yeyote (kama vile Godbless Lema), baada ya kutoa maelezo mafupi ya ushahidi unaotilia mashaka ya dhahiri kuhusu ukweli wa kauli juu ya jambo ambalo mbunge mwingine (kama vile Mizengo Pinda) amelisema Bungeni, anaweza kumdai Mbunge huyo (Mizengo Pinda), ambaye kauli yake inatiliwa shaka, atoe uthibitisho wa ukweli wa kauli yake na kama atashindwa kufanya hivyo, afute maelezo yake hayo.

Nane, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(6) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha ukweli wa kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda), atawajibika kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, papo hapo au katika muda atakaopewa na Spika kwa ajili ya kufanya hivyo.

Tisa, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(7) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo Mbunge aliyetakiwa kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake aliyoyatoa Bungeni (Mizengo Pinda) atashindwa kufanya hivyo, anaweza kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake hayo, papo hapo au katika muda atakaokuwa amepewa na Spika kwa ajili ya kuthibitisha kauli au usemi au maelezo yake.

Na kumi, spika alipaswa kujiridhisha kwamba, kwa mujibu wa kifungu cha 63(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), endapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, Mbunge aliyetakiwa kutoa uthibitisho wa ukweli wa kauli yake aliyoitoa bungeni (Mizengo Pinda) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge, na kama atakataa kujirekebisha kwa kufuta kauli au usemi au maelezo yake, basi Spika atamwadhibu kwa kumsimamisha Mbunge huyo (Mizengo Pinda) asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.

Hivyo ndivyo Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) zinavyosomeka. Na huu ndio mwongozo aliopaswa kuutoa Spika Makinda. Lakini, baada ya kuombwa mwongozo husika, Spika Makinda hakuutoa. Badala yake, akaona kwamba ombi hilo ni utovu wa “adabu” wa “hali ya juu”. Kwa maneno yake mwenyewe, Spika alisema, “Bunge letu hili lazima liwe na adabu ya hali ya juu; Waziri Mkuu na ahadi yake aliyoiweka ndani ya Bunge hili anaweza kulidanganya?”

Kwa hakika, lazima hapa tukubaliane kwamba spika alipindisha Kanuni za Kudumu za Bunge (2007) kwa lengo la kubembeleza urafiki wa Kaizari kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Aliombe radhi Bunge na taifa kwa ujumla.

Simu: 0758341483/0684175182
Email: deus.jovin@gmail.com

Huyu mama Anna Makinda aka 'alikwina' ndiye chanzo cha matatizo Tanzania kwa sasa...!
Na nchi bila bunge lenye uongozi makini, ni nchi iliyokwishakufa...., Hapa anatekeleza maagizo ya CCM na siyo kanuni za bunge - maana yaelekea kabisa kuwa anapanic, hazijui au hazikumbuki na analazimishia aonekane ni mkali au anakomaa kumbe ni ukosefu wa busara, akili na uongozi.

Tanzania yote inahitaji kuundwa upya, na hii bila shaka dalili zote zinaonyesha kuwa kuna mianya mingi ya nguvu ya umma kuchukua uongozi, ikiwa ni pamoja na kutokea ktk anguko la mhimili huu, Bunge! Wananchi wanapoteza imani haraka sana, na hatima yake haitabiriki..
 
Back
Top Bottom