Should CHADEMA Fire Zitto?

Should Zitto get FIRED from CHADEMA?

  • YES

    Votes: 137 65.9%
  • NO

    Votes: 57 27.4%
  • May be

    Votes: 10 4.8%
  • I don't know

    Votes: 4 1.9%

  • Total voters
    208
Status
Not open for further replies.
Zitto, acha kupiga watu mkwara hapa, kusema ukweli, siku zote huwa napenda iwepo chadema bila zitto, mbona hauaminiki? Gorofa lile la mbezi umepata wapi pesa, justify it hapahapa ili watu wakuamini, na je, hummer hiyo ulinunua kwa pesa gani? eleza hapa, au ndo zile za mfuko wa bunge ambazo ulijifanya kukataa?

Hapo bungeni unapata shilingi ngapi? Weka wazi biashara zako unazozifanya ili watu tusiwe na wasiwasi na wewe, halafu, tunaomba usiwe kirusi kwa chadema, kwasababu wewe si muhimu kwetu kuliko chadema...please and please!
 

Zitto hawezi kuwa makini na suala lolote la kuivuruga CHADEMA...nahisi anafanya makusudi kwa malengo anayoyajua mwenyewe na wanaomtuma kama wapo....refer kauli zake za kugombea urais katikati ya kampeni za 2010 na zile za Arumeru...yeye badala ya kuunga mkono juhudi za wanachama wengine yeye anakimbilia kwenye ubinafsi......

Sina tatizo na yeye kugombea urais lakini kwa nini asisubiri wakati muafaka na akafuata taratibu za chama ili kama akipita tumuunge mkono kwa pamoja kuliko hii divide and rule anayo implement sasa.
 
Zitto ni sawa na kindama kilichotoroka kwenye zizi kwenda kula na mafahali kikajiona na chenyewe ni fahali sasa madume yameaanza kupambana ndo kinajua kuwa kina baba na mama kinataka kurudi zizini CDM MPENI HAKI YAKE KAMA MLUNGULA KALA ACHINGIWE BAHARINI KWANZA VUA UNAIBU KATIBU THEN PELEKA PCCB AKAFIE HUKO DONT SPILL HIS BLOOD INSIDE THE PARTY.
 
Jmushi1, mkuu tafadhali... Hivi nikikwambia wewe kwamba Dr.Slaa, Mbowe na Lissu walishachukua Hongo utanijibu nini? Je, nao tutawaweka kwa Kaizali, misumari na msalaba ikiwa pembeni? au...Labda nikuulize wewe Zitto ata prove vipi kesho ikiwa hajachukua. I mean wewe kama ungekuwa nafasi ya Zitto na hujachukua hongo utaweza vipi ku prove hujachukua? kwa kuonyesha bank account, warrant ya house search ama ungefanya nini. Kwa nini tunakuwa wepesi sana kuhukumu watu wengine wakati hatufahamu hata yenyewe ni yapi..

Kesho, ni just press conference, kukana hizi tuhuma ambazo Maswi mwenyewe anazikana hajamtaja mtu kwa jina isipokuwa alisema Wanaomtetea Mhando ni kwa sababu wanafanya bishara na Tanesco. Kina nani hao hataki kuwataja!. Na tunajua ukweli alitaja lakini anaruka baada ya kubanwa.. Maswi sii mkweili hata kidogo.

Sasa kama hakusema yeye ni nani alowalitaja jina la Zitto kuhusika na hata kuongezea sababu ya kwmaba ndio maana hapokei posho..Haya madudu yote, haya ring something fishy is goin' on!..
 

Haswaaaa Mkuu wangu. Huo mfano wako umegonga pale pale. Kwa sisi tunaoishi katika mazingira ya mifugo iko hivi: kwa kawaida madume/mafahali yakishakula yakashiba na hasa wakati wa jioni vita inayofuata ni kugombea majike na kama ujuavyo huwa hadharani bila kificho. Wakati mchezo huu unaendelea, vindama ndivyo huumia zaidi kwani havipati hata nafasi ya kunyonya na badala yake hukimbia hovyo.

Na hiki ndicho kinachotokea huko CCM, mafisadi (mafahali) walishakula wakavimbiwa kilichobaki ni "kupanda" - yaani kutafuta rushwa kubwa kubwa kwa ajili ya kujistarehesha kwa anasa zaidi; hapa ndipo vindama vidogo vilivyoasi makao (akina Zitto) vinapopata tabu.
 
Mtoa mada, mimi nadhani issue ya msingi hapa sio kumfukuza Zitto au kumuacha. Cha msingi hapa ni kwanza kupatikana kwa ushahidi pasi shaka kuwa Mh. Zitto alipokea rushwa au hakupokea.

Tukumbuke kuwa siasa za nchi yetu kupakana matope siyo kitu cha ajabu. CCM walimuadhibu kikatili mh. Lowasa leo hii wanajuta. Ikishathibitishwa pasi shaka kuwa Mh. Zitto alipokea rushwa nadhani CDM kama chama wanataratibu za kinidhamu kwa viongozi wanaokosa hivyo basi ni busara kuwa taratibu hizo zichukue mkondo wake na hata kama ni kufukuzwa basi afukuzwe kwa mjibu wa sheria na taratibu za chama na si kukurupuka kama CUF na NCCR mageuzi ambazo zimefukuza watu, na mpaka leo wanadunda na ubunge wao.

Na ikithibishwa pasi shaka kuwa mheshimiwa Zitto hakupokea rushwa basi sheria napo ichukue mkondo wake kama inavyositahili, kama ni kumuomba radhi au kumulipa fidia kutokana na kumchafua na iwe hivyo. Kwahiyo basi mimi ningependa mjadala ujikite ni namna gani ukweli utapatikana? Ili tutoe maoni from facts na sio here say.
 
When it comes to serious issues kama hizi ni vizuri tukatulia na kusubiri kinachoendelea, itakuwa bora sana. Sipendi kusema kwa jazba kama wewe lakini this is sensitive. Na chama chochote kinahitaji wanachama siyo Zitto tu, kama unajua what a political party is supposed to be bas utaona Zitto hata wewe unatakiwa CDM. Hizi ni tuhuma lets wait and see kama zina mashiko! Jana nilisema hapa kujenga ghorofa si lazima uibe, Hammer unaweza nunua pia ya mtumba ni vipaumbele tu vya mtu. It is too early for now!
 
Mkuu swali lako kuhusu kina Slaa kuchukuwa rushwa ni rhetoric?

Unamaanisha kunijulisha kuwa wamechukuwa rushwa?
 
Ni wakati muafaka sasa wa kukata hiki kiungo chenye kansa ndani ya CDM.Sisi wanachama wa kawaida huku vijijini tumechoka!kila siku ana sarakasi mpya
 
Mkuu swali lako kuhusu kina Slaa kuchukuwa rushwa ni rhetoric?

Unamaanisha kunijulisha kuwa wamechukuwa rushwa?
Vipi umeshtuka?...ebu nambie kwanza majibu yako wewe utawasulubu kwa tuhuma zangu?
 
Zitto alisema akipatikana na hatia atawajibika. Nina wasiwasi na hii kauli. Ni tata sana
 

Is Zitto too smart boy? Or smart enough? Nafikiri uamini kama amekamata mlungula kwa sababu ni 'too smart boy' sasa mimi naamini inawezekana ni kweli kwa sababu ni 'too smart boy'!!
 
Zitto asipotangaza kujiuzulu UENYEKITI wa POAC sitamwelewa leo. Sambamba na hilo ni kujiuzulu pia unaibu KUB. Vinginevyo atuambie ni kwanini alikusanya sahihi za kumtaka WM Pinda ajiuzulu.
 
Vipi umeshtuka?...ebu nambie kwanza majibu yako wewe utawasulubu kwa tuhuma zangu?

Hapana mkuu,ntawasubiri kwanza kuwasikia wanachosema halafu pia nitasubiri uchunguzi,hata ukirejea bandiko langu la mwanzo,ndivyo nilivyomaanisha.
Nimesoma taarifa ya mh Zitto,kuna pahala maneno yake yamefanana sana na hayo maswali uloniuliza lol!.Kumbuka simjamsulubu Zitto.
Pia nilishangazwa pale aliposema eti wajumbe wengine wa kamati wasiguswe,eti kama ikibidi ajiuzulu,hapo si kuingilia uchunguzi?Ama wajumbe wa POAC si part of the investigation of POAC?
 
aisee mbona maneno machache hivi,hii ni ajabu. Hebu tupe mawazo yako juu ya hili swala maana tangu Regia kafariki hakuna hata mmoja wenu amekuja kuziba pengo lake.

Kuziba pengo lake katuika nini hasa?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…