Mkuu wewe kama unakunywa pombe utakuwa umejifunzia ukubwani.Kama si pombe kuna kitu huwa kinakulevya na unakuja na mabandiko ya ajabu ajabu.
Unajuwa nilipo hadi useme kuna mbege kama si kauli ya kijinga na yenye kuonyesha ubaguzi?Kama Zitto anaamini yale unayoyaamini wewe kuwa chama ni cha kikanda,kikabila na kidini.Kwanini sasa asije huko kwenye chama chenu kisicho na hayo matatizo?
Wananchi wengi wanaochukizwa na hizo kauli ni wale ambao wanaona kwamba chadema ni chama cha kitaifa.Wale wasio na hila na chama hawaoni hayo.
Tofauti na wale wa ccm,chauma na cuf ambao wanatumia propaganda sawa na Zitto za kuihujumu chadema.
Huwa sijui kwanini huwa kama unawashwa flani hivi na baadhi ya viongozi wa chadema.Huwezi kuficha chuki zako hata siku moja.
Nimeanzisha thread yenye swali unaloliona na nimeweka sababu za kuijenga hoja yangu.Wewe unataka kubadili mjadala sijui kuhusu aliyeombwa kugombea urais,as if hakuna asiyejuwa kuwa ni kina nani mnaomwomba ama wenye kuombea agombee kwa kutumia mgongo wa chuki,makundi na kauli za kuvuruga chama kwa kuleta udini,ukabila na ukanda sijui wa Lutigite.
CHADEMA kilikuwa kinajinasibisha na kupinga ufisadi na kumkomboa mwananchi pamoja na kuwa mbali mbali na ufisadi na mafisadi pale inapokuja kwenye kupata credibility ya wananchi. Na siyo style anayoitumia Zitto yenye uharibifu na kuleta makundi ndani ya chama.
Mambo ya kurudisha ukombozi wa Mtanzania nyuma.
Id agree with you, but then wed both be wrong.
Umeishiwa na hoja tangu lini mbege imegeuka tusi kwa mchaga? Ni ukombozi upi ambao Chadema mnataka kumkomboa mtanzania? Watanzania tupu huru siku nyingi sana nadhani kabla hujazaliwa hizo propaganda zenu za ukombozi tafuteni kwa kuzipeleka; wewe ndio mshabiki mkubwa makundi leo unamtuhumu Zitto kwa makundi ama kweli "Nyani haoni kundule"
Chama
Gongo la mboto DSM
Last edited by a moderator: