Shonza: Kwa Mara ya Kwanza Tutampitisha Rais Mwanamke kwa Kishindo Mwaka 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946

MHE. JULIANA SHONZA - "KWA MARA YA KWANZA TUTAMPITISHA RAIS MWANAMKE KWA KISHINDO MWAKA 2025"

"Tutampitisha Rais Mwanamke Madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2025 kwa kumpigia kura za kutosha, kura za heshima. Hatutamchagua kwa sababu ni Mwanamke, hatutamchagua kwa sababu ni takwa la Serikali, siyo kwa sababu ya utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi wa miaka 10, Hapana!" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tutamchagua kwasababu ya uthubutu, tumeona Rais wetu alivyothubutu. Zilitolewa fedha za UVIKO-19 Duniani kote na kazi yake ilikuwa kununua Gloves, Barakoa, Sanitizers. Rais akasema hapana!" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Rais akaangalia, Tanzania pekee yake ndiyo fedha za UVIKO-19 ziliruhusiwa zikafanye kazi zingine zikajenga madarasa nchi nzima na wanufaika ni sisi na watoto wetu" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Haya yote ni uthubutu ambao Rais Samia anao. Sisi tutamchagua kwa sababu ya uthubutu wake alionao na wala siyo kwa sababu nyingine. Ili tumuweke Madarakani ni lazima sisi wanawake tuwe mstari wa mbele kwa kusemea mazuri aliyoyafanya na kuwaunga mkono wasaidizi wake, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na watendaji wote" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tutumie fursa ambayo Rais ameitoa ya kuruhusu Mikutano ya hadhara, sisi kwetu ni faida maana tunatekeleza Ilani ya CCM na tuna mambo mengi ya kuongea. Wenzetu hawana cha kuongea, wakija kwenye mikutano ni matusi tu kwasababu hawana cha kuongea" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Tumekutana kwasababu tuna jambo sisi wanawake tupeane joto, tayari tuna Rais wetu ambaye ni Mwanamke. Sisi huku chini ndiyo jeshi lake. Jeshi la Mama ni wewe, Jeshi la Mama ni mimi. Akikaa kule anajua Tunduma nina wanawake. Tuhamasishane maana inasaidia kukijenga Chama na inasaidia viongozi kuielezea Ilani ya CCM" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe.


 
Uthubutu pekee hautoshi, ila ni pamoja na umakini na umahiri.
 
Weka akiba ya maneno wewe usijitoe ufahamu njoo huku ground ndo utajua ukweli wa mama kwa watoto anakubalika kiasi gani
 
Mtaani pagumu sana aiseee, ameona njaa inazidi katafuta venue ya kuongea pumba ili akumbukwe. Most politicians ni empty headed aiseeee.
 
Sifa zinakaribia kuzidi utendaji, mjini kote mabango yamejaa yote yakielezea sifa, bado mawaziri wabunge, wanachama wa ccm na chadema watendaji wote wa serikali, hakika sifa na zivume .
 
Back
Top Bottom