SERIKALI imesema ugonjwa wa malaria kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano umepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 10 kwa mwaka huu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaama kabla ya uzinduzi wa taarifa ya awali ya hali ya malaria nchini kupitia utafiti wa viashiria vya ugonjwa wa ukimwi na malaria, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi, alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 44.
Serikali imechukua hatua madhubuti katika kudhibiti kwa kuandaa sera sambamba na mikakati itakayolenga kupunguza maambukizi hayo, alisema Dk. Mwinyi.
Aidha, alifafanua lengo la utafiti huo mbali na kupata idadi ya kushuka kwa kiwango cha maambukizi kutoka kwa watoto wadogo, vilevile ni kufahamu takwimu sahihi juu ya ufahamu na tabia kuhusiana na ukimwi na malaria.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Mayasa Mwinyi, alitabanaisha kuwa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kimepungua kwa asilimia moja kutoka mwaka 2008 hadi sasa.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Kiranga and co naomba kujua hapo juu kama ethics zimevunjwa. Kwani mleta mada ametoa takwimu, na ukienda wizarani pia watakupa takwimu ya wilaya gani Tanzania inaongoza kwa maambukizi ya ukimwi sasa.
|