Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Usihukumu eti "walafi wa madaraka". Sina muda wa kutosha ila nimechambua hizo hoja unazo jitanabaisha kwazo na naona hazina mashiko. Wino mwekundu ni hoja na mwanazuoni wako na bluu ni majibu yangu. Nawahi kupalila shamba, ni msimu wa kilimo-mkulima mie so pardon my lack of details as am in a hurry.

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.

Come on Prof. Why stating the obvious? This can be said to be the case for virtually all land masses occupied by black people that later on came to be counties or states as per the definition of the Montevideo Convention.


Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

What is the significance of this obvious historical account? Let me be patient a bit more but unti know you have just wasted my time.

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Three questions "Mr. Professor" 1. "Lakini mwalimu hakupata"...so are you blaming him or complementing him? What is the unstated assumption here on which your statement is based? 2. "Muda wa Kutosha" who defines muda wa kutosha? How do you measure utaifa wa Tanganyika before you come to the conclusion that it was not built? 3. "Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania." Again there is a seriously flawed assumption here, though implicit. Let me put it this way, since for generations as slaves African Americans built the US does that make them white and preclude them from claiming their black heritage?


Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka.

This regressive thinking coming from a professor of international repute is making me sick and tired. 1. What if anti-liberation struggles folks asked the same question in the 1950? Is it not a truism that all freedom fighters were born and raised under colonial yoke and consequently they had no clue of what it was to be a country free form white domination? Inashangaza.

"maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka." Without any substantiation, atypical of Professors of his level of achievements, he leaves it for us to fill the gaps. Ironically, he appears to be forgetting that the draft was writen by the likes of Judge (rtd) Warioba and Prime Minister (rtd) Dr. Salim Ahmed Salim. What other position would they want to occupy given also their honorable age? Sheer falacy!

Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

Any link with the substantive part of the draft constitution? This threat is totally misplaced. Who told you factors that lead to the disintergration of those nation states have been listed in the draft for the purposose of implementing them and consequently lead to disintergration? The draft calls for three tier union structure. Hayo yote ni yako! Kaa nayo!
- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.[/QUOTE]
 
hii nchi baada ya kuungana iliitwa "REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR" baadae tukasikia TANZANIA kwa mawazo yangu hapo ndipo makosa yalipoanza
 
Kwa wale Walio Karibu na Shivji ni vyema wamshauri mzee huyu aache kuendelea kuharibu reputation yake na sasa ajinyamazie na kupumzika katika maisha yake ya ustaafu. Kwa mfano, katika hili la kutoijua na kutoitambua Tanganyika, amedandanya tena. Tazama yafuatayo:

ISSA SHIVJI (2006): Let the people speak: Tanzania Down the road to neoliberalism, page 117, Paragraph 6:




Cc: Nguruvi3, mliberali, FJM, tpaul, Pasco, FaizaFoxy, Mtanganyika, MwanaDiwani, gambalanyoka, Ritz, zomba.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Maneno katika uzi huu yaliyo semwa na Prof. Shivji ni Yale tu yaliyo ndani ya nukuu na ndani ya inverted commas pekee., Yale yote nje ya hayo pamoja na maneno " tanganyika siijui, siihitaji" ni ya kwangu binafsi na uasihusishwe na Prof shivji.

Nimehusisha tu mawazo yake na post yangu ya hapo awali niliyo iita " Tanganyika siijui wala siihitaji"

Lakini maneno hayo hayaja tamkwa na Prof. Issa shivji hata kidogo.

Nashukuru.
 
Last edited by a moderator:
shivji ni -------- wa kutupa. mbona hawaambii waznz wasililie uznz wao?
 
shivji and his fluffy round face is a disgrace to Tanganyikans
 
Huyo kafurungwa shivji lazima watu wadai Tanganyika uyo muhindi anajuwa wapi historia kwahiyo mwaka 1964 iliungana Tanganyika na Znz au Tanzania na Znz mbona mnaleta usomi wenu uchwara apa
 
Hata Zanzibar ni jina lililoacha na waarabu waliokuja kukamata watumwa likimaanisha sehemu ya mijitu myeusi au nigger land. Zanj ni jina la kuzalilisha mtumweusi.

Asante kwa kunipa maarifa ya jina Zanjibar, kumbe hilo ni noumer kuliko wenyewe wanavyolikumbatia. Haiingii akilini huyu Baniani SiiiVuzii kuinanga Tanganyika mara baada ya kukamatishwa mpunga. Kabla ya kufanya huu mchepuko wa Kitaaluma kiukweli nilikuwa nina mkubali saaana huyu Shortie kutoka Bombay.
 
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.

ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.

Hayo ni mawazo mgando,Unauliza Tanganyika imetoka wapi unajitia kichaa kuwa huijui Tanganyika.Sababu ya kuidai Tanganyika yetu ni baada ya kuona wenzetu wanakaribia kupata uhuru kamili wakati sisi watanganyika tuko kimya tu.Kusema tunataka Tanganyika ndio imekuwa nongwa.Walipodai Zanzibar wakapewa mlikuwa wapi,?wimbo wa taifa,bendera,Baraza,vikosi vya smz(suk) na watu wawili Karume na Jakaya walivyoondoa kimya kimya sula la mafuta na gesi kimyakimya mlikuwa wapi?.Tena jakaya anatangaza kuwa mimi na karume ndio tuliondoa gesi na mafuta.Baada ya kuona balaza la mapinduzi mwamechachamaa na kuunda shirika la mafuta hata jk na karume hawajaridhia.Ni mengi mno ambayo Tanganyika tumeacha na kuwafanya Wazanzibar ambao ni nchi huru yenye mambo yake na kila kitu na katiba huku sisi watanganyika tukibaki gizani.TUNAITAKA TANGANYIKA YETU,MUUNGANO WANANCHI NDIO WAMEUNGANA TAYARI LAKINI TUNATAKA TANGANYIKA!!!.
 
ninacho Karibu kuonyesha hapa kwakuuliza swali hili ni kuwa kama kuna mtu aliamka na kuidai Tanganyika huru inayo jitegemea na kujiongoza basi ni mwalimu nyerere,. Na kama mwalimu huyo huyo aliiua Tanganyika akaizika akaunda Tanzania akaisemea na akaonya juu ya kuifufua Tanganyika sisi unaijua Tanganyika kuliko yeye? Au ndo tunajifanya tunaasili ya Tanganyika kuliko nyerere!??

Ndugu zangu Utengano sikuzote ni ugonjwa na dhambi mbaya sana. Kubaguana huku kutatumaliza kabisa!!

Nasema hatuwezi kususia muungano ATI kwasababu ya marekebisho ya katiba ya Zanzibar. Haiwezekani!!!

Kama swala ni marekebisho basi tukaetuzungumze turekebishe tusonge mbele!

Utanganyika utaua muungano.

Nakubaliana na wewe kuwa utengano ni udhaifui, lakini hilo litakuwa siyo kosa la wanaodai Tanganyika bali ni kosa la waliojiondoa kwenye muungano kupitia Katiba yao. Tanganyika hatujawahi kulalamikia upendeleo owte wanaopewa Wanzanibar na kufaidi raslimali za Tangayika wakati watangayika hawana uhuru huo huko Zanzibar, lakini hata mwaka 1993 jambo lililosababisha G55 lilikuwa ni vitendo vya Zanzibar kuhusiana na Muungano huo. Waambie kwanza waone madhara ya matendo yao kuhusu Muungano na wayarekebisha. Vinginevyo kubali kuwa Tanzania-Minus-Zanzibar=Tanganyika
 
Mzee msaada wa source ya quote ya nyerere ulio iweka kwenye signature yako.

Mwalimu Nyerere amenukuliwa hapa:

The Election Study Committee (1973), University of Dar-es-Salaam: "Socialism and Participation": Tanzania's 1970 National Elections.

Ni kitabu cha kurasa 474, nikikumbuka specific page nitakujlisha.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tanganyika haijawahi kuwa bustani ya wakoloni ila bustani za wakoloni ni zile zote zilizotengwa na Berlin Conference ya 1884, maana hizo ndo ziliandaliwa kwa lengo hilo. Baada ya Vita Kuu ya pili ya dunia sisi tulirudia utaifa wetu, tukaachana na akina Kagame na Nkurunziza tukawa sisi...tukawa TAIFA na tukawa NCHI. Haya maneno ya Shivji (mi sintamwita Prof. Shivji maana Prof maana yake ni mwalimu na hivyo sintaitendea haki tasnia ya ualimu kama yeye atakuwa mwalimu kwa kusema jina la kuundwa na sisi kama TANZANIA ndilo tu halali yetu endapo ZANZIBAR ni halali. Mi naona Tanganyika ipo na mjadala usiwe uwepo wa Tanganyika au utokuwepo wake, bali uhalali na uhakika wa kuwepo kwa Tanzania inayoundwa na Tanganyika na Zanzibar bila ya kujali historia uchwara hizo, maana hata Tanzania ikiwepo bado kulikuwa na jitihada za kuwepo kwa dola ya Kilimakyaro na akina Maleyale....Mwalimu Shivji toa uhalali wa muungano wa Zanzibar na Tanganyika kuunda Tanzania bila ya Tanganyika kuwa nchi au taifa ungetoka wapi?????? Hapo naona umetuelimisha kwa dhana dhaifu kuliko kwa uhalisia wa kujenga hoja na kutoa dhana ya nchi na taifa.
 
Character X

Nikushukuru kwa maoni yako, hakika kupinga bila kupigana ndio uungwana.

Nina maswali machache naomba unisaidie.

Moja ya malalamiko ya wazanzibar ni kuwa Tanganyika(usioitaka) imejificha katika koti la muungano.
Wanataka kuwepo na mpaka kati ya mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Katika hali hiyo tutafanyaje? Je, tuache status quo kwa kudharau malalamiko hayo au tuyafanyie kazi?
Kama ni kuyafanyia kazi, ni kwa njia zipi labda.

Pili, kwavile znz ina dola, je hiyo inamaanisha dola ya znz ni kubwa kuliko ile ya JMT?

Tatu, kwavile znz ina fiscal autonomy na hata kufanya mambo ya kumtenga Mtanganyika kwa kutumia haki hiyo, haki ya Mtanganyika kuwa na fiscal autonomy yake ipo wapi? Je, Mtanganyika hapaswi kuamua hatima yake na kama ni ndiyo ni kwa njia na utaratibu gani.

Nne, kwavile znz ina vyombo vyake vya kiuchumi, kuna uhalali gani wa Mtanganyika kulipia gharama za sehemu yenye dola yake?

Tano, hii dola ya Tanzania ni mali ya nani? Nani mshirika wa dola hiyo
Nitendee haki kwa majibu ya maswali.
 
Asante kwa kunipa maarifa ya jina Zanjibar, kumbe hilo ni noumer kuliko wenyewe wanavyolikumbatia. Haiingii akilini huyu Baniani SiiiVuzii kuinanga Tanganyika mara baada ya kukamatishwa mpunga. Kabla ya kufanya huu mchepuko wa Kitaaluma kiukweli nilikuwa nina mkubali saaana huyu Shortie kutoka Bombay.

Nikweli kabisa. mimi nilipokuwa shule nilikuwa napenda kuwaita wazanzibar wazenji. kukawa na professor wa anthropology ambae ni mmarekani mweusi aliekuwa anafundisha kenya akabidi aniambia kuwa waarabu waliwaita watuweusi Zenji kama wazungu walivyo waita watu weusi nigger. yote ni majina ya kuwazalilisha watu weusi. Nakuna mtu alishasema ndio asili ya tusi la kiswahili la mshenzi na jina la Zanzibar vile vile.
 
Nikweli kabisa. mimi nilipokuwa shule nilikuwa napenda kuwaita wazanzibar wazenji. kukawa na professor wa anthropology ambae ni mmarekani mweusi aliekuwa anafundisha kenya akabidi aniambia kuwa waarabu waliwaita watuweusi Zenji kama wazungu walivyo waita watu weusi nigger. yote ni majina ya kuwazalilisha watu weusi. Nakuna mtu alishasema ndio asili ya tusi la kiswahili la mshenzi na jina la Zanzibar vile vile.

hahahah duh sasa wewe umeenda mbali zaidi kusema tusi "mshenzi" ina maana kuna siku tutasikia "mshenzibaaa"
 
Kwa wale Walio Karibu na Shivji ni vyema wamshauri mzee huyu aache kuendelea kuharibu reputation yake na sasa ajinyamazie na kupumzika katika maisha yake ya ustaafu. Kwa mfano, katika hili la kutoijua na kutoitambua Tanganyika, amedandanya tena. Tazama yafuatayo:

ISSA SHIVJI (2006): Let the people speak: Tanzania Down the road to neoliberalism, page 117, Paragraph 6:




Cc: Nguruvi3, mliberali, FJM, tpaul, Pasco, FaizaFoxy, Mtanganyika, MwanaDiwani, gambalanyoka, Ritz, zomba.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Wakati Sadam Hussein anakamatwa na askari wa marekani, alionekana kuwa mpole kama kondoo, tofauti na dunia ilivyomfahamu. Inasemekana kwamba askari wa marekani walimchoma sindano ya kumpumbaza na kumzezetesha ilki iwe rahisi kumkamata na hatimaye kumuuua. Inavyooneka hata huyu profesa atakuwa amechomwa sindano ya uzezeta na maCCM iliyomtoa akili na kumfanya akubali kueneza propaganda hizi, kama zinavyopikwa na CCM. Inawezekana tukawe tunamlaumu bure, huenda hatumii akili zake za kawaida kutamka uharo huu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom