Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Atakuwa anaijua India manake ndo kwao huko!!!!!!!!!!!!!
 
...Whatever form the new unity takes it ought to observe scrupulously the basic democratic principle of the right of people to self determination. This premise has two sides to it.

A) That between Zanziba and Tanganyika, as a people and nations, we would have to respect the principle of equality on the one hand, and be sensitive to the legitimate culture, history and sentiments of both parts, on the other. This means that THOSE OF US who come from the bigger nation, Tanganyika, and consider OURSELVES progressive and democrats, should be extra responsible and cautious in guiding against big nation Chauvism.
Haya ni maneno ya Prof Shivji ambaye juzi amesimama na kusema kuzinduka kwa Tanganyika kutaua uzalendo na kujenga chuki kwa wazanzibar.
Ukisoma maneno hayo hakuna mahali ametaja Tanzania. Leo anapata wapi hoja ya kulaani kuzinduka kwa Tanganyika?

Anasema, muungano mpya unapswa kuzingatia misingi ya demokrasi ya watu kuamua hatima yao.Kuna maeneo mawili
A. Kati ya znz na Tanganyika kama watu na taifa tuheshimu misingi ya usawa kwa upande mmoja,na tuwe 'makini' kuzingatia tamaduni, historia na hisia za pande zote, kwa upande wa pili.
Hii ina maana sisi tunaotoka taifa lenye demokrasia iliyombele tuwe na wajibu zaidi na tahadhari dhidi ya 'ubabe'

Tunapoangalia maneno hayo ambayo si tafsiri rasmi, tunaona kuwa Shivji alisisitiza muungano kujali hisia za pande zote.
Kilichotokea hadi kuandikwa katiba ni pamoja na hisia za pande zote.

Upande mmoja ukidai unaonewa na mwingine unatoa zaidi katika muungano.
Shivji anaposema kuzinduka kwa Tanganyika kutaua uzalendo na kujenga chuki dhidi ya wazanzibar anakana maandishi yake. Hajazingantia hisia za upande wa Tanganyika zinazodai uwepo wa fiscal autonomy.

Lakini si hivyo tu, Shivji anapokubali ZNZ ibadili katiba na kuwa juu ya katiba ya JMT anakana maneno yake.
Kama alitoa thadhari juu ya Tanganyika kuwa na Chauvism, hivi haoni kwasasa Znz ina chauvism juu ya muungano.

Na kwanini adhani malalamiko ya Watanganyika kudai fiscal autonomy itakuwa ni chauvism, waendelee kukaa kimya hata pale aliposema 'muungano uzingatie hisia za pande mbili'

Kinachotokea kwa Shivji ni suala la kuachia 'jini itoke kwenye chupa'. Shivji amekwenda znz na kuwachochea sana kuhusu kuonewa, uharamu wa katiba na uwepo wa Tanganyika. Leo amegundua kuwa uwepo wa Tanganyika utawasadia Watanganyika na utegemezi wa znz utakuwa umefikia mwisho, anageuza kibao na kusema hilo litazaa Utanganyika na chuki kwa Wazanzibar.

Kwamba, chuki kwa Watanganyika kutoka kwa wznz ni jambo jema kwa Shivji, tatizo ni pale chuki hiyo itakapokuwa dhidi ya wazanzibar. Sasa anabadili kibao na kusema anataka serikali 2.

Majuzi katika kongomano lake la CCM, Shivji alisema msingi wa muungano ni kugawana madaraka.
Katika maandishi yake anasema kuwepo na usawa. Halafu anaonya juu ya Tanganyika ku dominate.
Katika muungano wa mataifa mawili, ni lazima moja lichukue nafasi ya uongozi.
Hakuna usawa kwasababu haukuwepo kwa namna yoyote.

Hajafafanunua usawa wa jambo gani. Kama anataka usawa ni lazima kwanza Tanganyika irudi ili ikae meza moja na znz kuangalia mambo machache sana ya pamoja.

Ndivyo Warioba alivyoshauri na tume yake.
Kumbe Shivji anakubaliana na Warioba lakini kwasababu zisizojulikana anaamua kula matapishi ya maandishi yake tena akimtanguliza Warioba kama kichefu chefu.
 
Ukweli ni kwamba wazenji walishaukataa huu muungano wa mazingaombwe cku nyingi, sioni 7bu ya kulazimishana 2takuja toana manundu bure. Tunaitaka tanganyika ye2 kama waznz walivyo na zenji yao full stop.
 
Character X
Kutoijua Tanganyika hakukufanyi uwe manamba hata kidogo. Unaposema wewe ni Mtanzania una maana ya mtu aliyezaliwa katika nchi iliyotokana na mataifa mawili, Tanganyika na Zanzibar. Hilo ndilo limkeuwepo kwa muda mrefu na hakika hakukuwa na hisia za Utanganyika.

Unapoondoa znz katika Utanzania, hubaki na utanzania unabaki na Utanganyika. Kwahiyo wewe utake usitake una 'genes' za Tanganyika. Zanz wameshakataa Utanzania kwa kusema wao ni nchi (katiba 2010). Wanatumia kifungu hicho kukubagua wewe Mtanzania kkwao. Wao wakija kwako wanasema ni Watanzania, wakipanda, wametoka nchi ya jirani.
Ndiyo walioamsha hisia za Utanganyika na kuwafanya Watanganyika wajione ni wapweke.
Nyerere alisema ' kama znz watasema sisi ni wznzn' basi Watanganyika watasononeka. Tananyika itabaki salama.

Pili, Nyerere alisema kama wznz hawataki muungano hatawapiga mabomu.
Leo wakiamua kuondoka katika muungano hatuna sababu za kuwapiga mabomu, ndivyo walivyofanya 2010.
Tunachosema hapa ni kuwa tumebaki wenyewe na hivyo tupewe nafasi ya kujiamulia mambo yetu.

Na wala Tanganyika haitaotoweka kwasababu Shivji kasema haina utaifa. Kama si utaifa sijui wale wazee waliokufa wakipiginia uhuru walikuwa wanatetea uhuru wa nchi gani. Lakini Shivji atueleza utaifa wa wznz ni upi?

Hatuwezi kubaki wenyewe katika muungano uliouawa na wazanzibar 2010,tukajidanganya tuna muungano.
Pengine kinachokuudhi ni jina Tanganyika, elewe kwasasa wewe ni Tanzania ambaye ni peke yako.
Mwenzako akitaka kukutumia anabeba bango lenye jina akisema ni Mtanzania,ukienda kwakewewe ni raia wa nchi jirani. Hakutambui.

Fikiria jambo hili, waziri mkuu ni mtu mkubwa sana katika JMT. Utashangaa nikikumabia kuwa Pinda lazima aombe kibali cha kufanya kazi znz kwasababu yeye hana kibali cha znz mkaazi. Seuse wewe! Hapo Utanzania upo wapi?

Na mwisho, hakuna anayesema Utanzania utafutika kama anavyodai Prof Shivji. Warioba na tume wanasema kuna mambo tutashikirikana kama taifa, kama uhamiaji na uraia.

Lakini kwa vile kuna mambo ambayo znz wanasema yanamneemesha Mtanganyika ni vema tukayaondoa. Kwa mfano, znz waliondoa mafuta na gesi. Iweje gesi ya Mtwara iwe yao?
Kwa mfumo uliopo utawezaje kutenga gesi ya Mtwara na ile 'ya znz' ?

Ili kuwe na usawa ambao Shivji ameueleza katika kitabu chake, ni lazima Tanganyika iwepo ili watu wakae meza moja.
Znz wakisema uvuvi si jambo la muungano, Tanganyika waliondoe katika Tanzania na kulipeleka kwa Tanganyika.
Kama Tanganyika haipo usawa utatoka wapi?

Mfano, znz wana wizara ya afya kwa ajili ya wznz. Wewe Mtanganyika ni mgeni na wala hupati huduma kama Mtanzania.
Waziri wa Afya wa Tanzania ni mzanzibar ambaye anashughulikia jambo lisilowahusu wznz. Hivi huoni kuna kituko hapo?
Kama hiyo inawezekana ni kwanini tusiruhu waziri wa fedha kutoka Uganda, waziri wa kazi kutoka Japan na waziri wa sheria kutoka Uingereza? Kwani kuna tofauti gani?

Mwisho kwani mkataba wa muungano unasemaje kama anavyochambua Mchambuzi? Kipi kigeni kilichochemekwa unachodhani kinalenga kuleta Utanganyika tu bila sababu
 
Huyu baba Natasha! !!!???#

Hivi watoto wake wana uraia wa nchi gani???!!!!

Amalizie siku zake kwa amani!!!!!
 
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.

ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.
hii ni sasa ni dharau iliyokithili na hisiyovumilika kuita taifa moja kuwa si taifa bali ni bustani ya wakoloni. kwa maana hiyo huyu "hajuza" anataka kutuambia/kutuaminisha yakua TANZANIA ni muunganiko wa BUSTANI YA WAKOLONI TANGANYIKA na ZANZIBAR???????????? Kuna kila haja yakunifanya nianze darasa la kwanza upya, kuliko kuishi kwenye kiza hiki kenene....!!!!!!
 
Hivi Wadau Naomba Kuuliza, Si Wengine Elimu Zenu Za Kayumba Hizi! Sijui Tunapotoshwa, Kwa Vile Waalimu Wenyewe Mhhhhh!! Hivi Ule Mkutano Wa Berlin 1880 -1884 Ulikuwa Na Lengo Gani?? Coz Sijaelewa Kwa Neno Tanganyika, Lilianza Wkt Wa Uingereza Au Ujerumani??
http://en.wikipedia.org/wiki/Tanganyika_Territory
The name "Tanganyika" is derived from the Swahili words tanga ("sail") and nyika ("uninhabited plain", "wilderness"). It might, therefore, be understood as a description of using Lake Tanganyika: "sail in the wilderness". Also Prof. Irfanhaider, the genius has given a very good example to how Tanzania got its name.[SUP][1][/SUP]

In the second half of the 19th century, to European explorers and colonialists penetrating the African interior from Zanzibar, Tanganyika came to mean that
Tanga = kutembea kwa kutangatanga, kwa kuzunguka eneo lote. nenda rudi
Nyika = ni uwanda, pori, msitu wa kati (Savanna)
na jina hili tulipewa na Wajerumani katika miaka kuanzia
Tanganyika Territory
Tanganyika Territory was a British League of Nations mandate between 1922 and 1946 ... the Swahili words tanga ("sail") and nyika ("uninhabited ...
Kwa hiyo Zanzibar sio Tanzania bali ni Zanzibar na hko wanakaa WaZanzibar
Kwa hiyo Bw Character X Katiba ya Zanzibar hairuhusu Mtanzania Bara (km mm Mtanganyika) kupewa ardhi ya aina au sentita yoyote kule Visiwani (eti wao tu haiwatoshi)
 
Character X
Kutoijua Tanganyika hakukufanyi uwe manamba hata kidogo. Unaposema wewe ni Mtanzania una maana ya mtu aliyezaliwa katika nchi iliyotokana na mataifa mawili, Tanganyika na Zanzibar. Hilo ndilo limkeuwepo kwa muda mrefu na hakika hakukuwa na hisia za Utanganyika.

Unapoondoa znz katika Utanzania, hubaki na utanzania unabaki na Utanganyika. Kwahiyo wewe utake usitake una 'genes' za Tanganyika. Zanz wameshakataa Utanzania kwa kusema wao ni nchi (katiba 2010). Wanatumia kifungu hicho kukubagua wewe Mtanzania kkwao. Wao wakija kwako wanasema ni Watanzania, wakipanda, wametoka nchi ya jirani.
Ndiyo walioamsha hisia za Utanganyika na kuwafanya Watanganyika wajione ni wapweke.
Nyerere alisema ' kama znz watasema sisi ni wznzn' basi Watanganyika watasononeka. Tananyika itabaki salama.

Pili, Nyerere alisema kama wznz hawataki muungano hatawapiga mabomu.
Leo wakiamua kuondoka katika muungano hatuna sababu za kuwapiga mabomu, ndivyo walivyofanya 2010.
Tunachosema hapa ni kuwa tumebaki wenyewe na hivyo tupewe nafasi ya kujiamulia mambo yetu.

Na wala Tanganyika haitaotoweka kwasababu Shivji kasema haina utaifa. Kama si utaifa sijui wale wazee waliokufa wakipiginia uhuru walikuwa wanatetea uhuru wa nchi gani. Lakini Shivji atueleza utaifa wa wznz ni upi?

Hatuwezi kubaki wenyewe katika muungano uliouawa na wazanzibar 2010,tukajidanganya tuna muungano.
Pengine kinachokuudhi ni jina Tanganyika, elewe kwasasa wewe ni Tanzania ambaye ni peke yako.
Mwenzako akitaka kukutumia anabeba bango lenye jina akisema ni Mtanzania,ukienda kwakewewe ni raia wa nchi jirani. Hakutambui.

Fikiria jambo hili, waziri mkuu ni mtu mkubwa sana katika JMT. Utashangaa nikikumabia kuwa Pinda lazima aombe kibali cha kufanya kazi znz kwasababu yeye hana kibali cha znz mkaazi. Seuse wewe! Hapo Utanzania upo wapi?

Na mwisho, hakuna anayesema Utanzania utafutika kama anavyodai Prof Shivji. Warioba na tume wanasema kuna mambo tutashikirikana kama taifa, kama uhamiaji na uraia.

Lakini kwa vile kuna mambo ambayo znz wanasema yanamneemesha Mtanganyika ni vema tukayaondoa. Kwa mfano, znz waliondoa mafuta na gesi. Iweje gesi ya Mtwara iwe yao?
Kwa mfumo uliopo utawezaje kutenga gesi ya Mtwara na ile 'ya znz' ?

Ili kuwe na usawa ambao Shivji ameueleza katika kitabu chake, ni lazima Tanganyika iwepo ili watu wakae meza moja.
Znz wakisema uvuvi si jambo la muungano, Tanganyika waliondoe katika Tanzania na kulipeleka kwa Tanganyika.
Kama Tanganyika haipo usawa utatoka wapi?

Mfano, znz wana wizara ya afya kwa ajili ya wznz. Wewe Mtanganyika ni mgeni na wala hupati huduma kama Mtanzania.
Waziri wa Afya wa Tanzania ni mzanzibar ambaye anashughulikia jambo lisilowahusu wznz. Hivi huoni kuna kituko hapo?
Kama hiyo inawezekana ni kwanini tusiruhu waziri wa fedha kutoka Uganda, waziri wa kazi kutoka Japan na waziri wa sheria kutoka Uingereza? Kwani kuna tofauti gani?

Mwisho kwani mkataba wa muungano unasemaje kama anavyochambua Mchambuzi? Kipi kigeni kilichochemekwa unachodhani kinalenga kuleta Utanganyika tu bila sababu

Kwanza ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwakuchangia kwa hoja, na kujibu kwa kunivumilia kama ambavyo demokrasia ya mawazo mbadala inavyo tuelekeza bila ya matusi wala dhihaka, niseme tu wazi sijui Una umri gani wala nafasi gani lakini wewe japo unamtazamo tofauti na wangu lakini ni mmoja Kati ya wale ambao ningetamani kukutana nao nje ya JF na kuzungumza zaidi na zaidi na kwahakika yake Mungu amekupa uwezo mkubwa ndani mwako kuwa muangalifu usipotee.

Pili niende kwenye hoja, nashukuru kwakuiona nia yangu ya dhati nakuiheshimu, kwamba natamani tu umoja wetu kama watanzania ubaki pale pale, kwakua ninaifahamu Tanzania nakuipenda katika umoja wetu tulionao sasa.

Naelewa hoja yako ya msingi kua Tanzania nimuungano wa Tanganyika na Zanzibar na hivyo ikiwa Zanzibar wamejitoa kwenye muungano tunabaki na Tanganyika,

Ninaelewa pia hoja yako ya "kujitoa" kwa Zanzibarkwenye muungano imejengwa juu ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 lakini ninaomba kujibu kama ifuatavyo;

1. Muungano wetu ni muungano wa nchi mbili lakini ni muumgano wakipekee kidogo. Si muungano wa nnchi mbili zilizo na uuwiano flani Karibu sawa,. Hapana ni muungano wa Nchi Moja Kubwa sana yenye watu Milioni 46 na nyingine Ndogo Kupindukia yenye watu Milioni 1.2, Nchi Moja yenye pato la sh Trilioni 37 na nyingine ndogo yenye pato la chini ya Trilioni 3, nchi moja kubwa ambayo inaungana na nchi nyingine ndogo kiasi ingeweza kuingia kwenye nchi hii kubwa mara 240 kwa maana ya eneo lake.

Lakini pia nchi moja kubwa kwa eneo, idadi ya watu, na pato lake lakini changa kwa maana ya utaifa wake na historia yake,. Na nchinyingine ndogo sana kwa maana ya sifa nilizotaja hapo juu lakini yenye hitoria ndefu ya zaidi ya karne mbili ya taifa la Zanzibar.

Sasa,

Unapotaka kuunganisha nnchi hizi, lazima uzinagatie hayo.!!!

Yani fanya ufanyavyo lakini hakikisha akakainchi kadogo lakini kenye historia yake ya karne nyingi pamoja na udogo wake kasipotee na historia yake kufutwa juu ya dunia tu kwakumezwa na taifa flani kubwa waliloamua kujiunga halo.- kufanya hivyo ni kufanya yaleyale waliyo ya fanya wakoloni miaka ile, ma beberu!!

Hivyo waasisi wakafikiria muundo wa serikali mbili lakini nchi moja ambao ungeitunza historia ya nzanzibar kwaipa kitu kinaitwa (spencial dispensation) utaratibu wakawaida kabisa katika hali za namna hii.,

2. Hoja kuwa Zanzibar imejitangaza kuwa nchi huru sisahihi,. Prof shivji ameeleza vizuri tu namna na mantiki ya neno "Nchi" kamalinavyosomeka kwenye katiba hiyo iliyo rekebishwa ya Zanzibar kwakusema, Zanzibar waliposema wao ninchi walimaanisha ni Dola!! Kitu ambacho siuwongo wala hakimaanishi wamejitoa kwenye muungano, isipokua wanamaanisha hasa kile ambacho waasisi walikimaanisha, kwamba Tanzania iwe nchi moja yenye dola mbili.

Note: kumbuka tofauti kati ya dola, serikali na Nchi.

3. Ninachokipinga mimi ni pale unapowasikia watu flani flani kutoka Zanzibar wakidai kitu kinaitwa "mamlaka kamili" na watu watanganyika wakidai "Dola ya Tanganyika"

Hakika yake ndugu yangu, vitu hivi kuamshwa nikuharibu taifa letu Tanzania na sikulijenga.

Mwalimu huyo uliye m quote maali flani pia aliwahi kusema " kuifufua dola ya tanganyika nikuua muungano".

NB; zingatia takwimu pale juu.

Ndugu, labda pia nikubali kwamba huenda Nina phobia na Hilo neno tanganyika, lakini phobia hii inakuja kwasababu ya ukweli kwamba huyu bwana tanganyika akifufuliwa tu, kitu kinaitwa Dola Ya Tanganyika ikawa dola hai, yenye mamlaka yake! HAKUNA TANZANIA TENA HAPO!! HAKUNA MUUNGANO TENA HAPO!!

Na mwisho kabisa nihitimishe kwakusema mimi na dhani swala hapa nikutatua changamoto za muundo wetu wa muungano, na kuujenga utaifa wetu kwakuwakemea wanaojenga misingi ya utengano. Kuidai tanganyika ATI mwasababu Zanzibar wanadai mamlaka Yao hatumkomoi mtu, tunajikomoa wenyewe tukiibomoa nchi yetu kwa midomo yetu wenyewe,

Ndugu nikualike utafakari tena.

Heshima kwako.
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?

Mimi kwani nilizaliwa Tanganyika nikaolewa Tanganyika,na watoto waliozaliwa Tanganyika ambayo ilifichwa katika Utanzania wakati wenzetu ni wazanzibari unamkumbuka Nyerer alikemea kule Mbeya walioleta Uzanzibari bila shaka alijua wasipozuia Utanganyika unakuja sasa wewe shida yako nini kutojua uhalisia wako au. Shivji aliazisha ngebe sasa aimalize kwa kufuta KATIBA YA ZANZIBAR KAMA KWELI ANATAKA MUUNGANO TUSITAFUNE MANENO PERIOD!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii ndoa kiboko...kuna mume na mke, ghafla mume asili yake imekufa japokuwa bado wanaishi pamoja. Kabaki mke ambae nae hamtaki mume, ndugu wa mume wanamkana ndugu yao kwa kisingizio "eti hajawai kuwepo"
 
Character X

Nikushukuru kwa maoni yako, hakika kupinga bila kupigana ndio uungwana.

Nina maswali machache naomba unisaidie.

Moja ya malalamiko ya wazanzibar ni kuwa Tanganyika(usioitaka) imejificha katika koti la muungano.
Wanataka kuwepo na mpaka kati ya mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Katika hali hiyo tutafanyaje? Je, tuache status quo kwa kudharau malalamiko hayo au tuyafanyie kazi?
Kama ni kuyafanyia kazi, ni kwa njia zipi labda.

Pili, kwavile znz ina dola, je hiyo inamaanisha dola ya znz ni kubwa kuliko ile ya JMT?

Tatu, kwavile znz ina fiscal autonomy na hata kufanya mambo ya kumtenga Mtanganyika kwa kutumia haki hiyo, haki ya Mtanganyika kuwa na fiscal autonomy yake ipo wapi? Je, Mtanganyika hapaswi kuamua hatima yake na kama ni ndiyo ni kwa njia na utaratibu gani.

Nne, kwavile znz ina vyombo vyake vya kiuchumi, kuna uhalali gani wa Mtanganyika kulipia gharama za sehemu yenye dola yake?

Tano, hii dola ya Tanzania ni mali ya nani? Nani mshirika wa dola hiyo
Naomba unitendee haki tafadhali, maswali hayajapata majibu
 
Mshamba mkubwa huyu mhindi aende kwao punjab! Prof sharubu tuu hana mchango wowote kwa nchi. Njaaa hizi bwana umepewa sh ngapi?
 
Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!

Kwaiyo unaona Utanganyika utawabaguwa Wazanzibari lakini Huoni Uzanzibari unavyo wabaguwa Watanganyika. Prof Shivji na MaCCM hawajatueleza kwanini Mtu wa Tanzania Bara asiwe na haki kama Mtu wa Zazibar ya kuwa na serekali yao inachunga masilai kama serekali ya zanzibari inavyochunga masilai ya wazanzibar. Swala la Tanganyika kuwepo kwa miazi 14 au nyerere na wapigania uhuru kuwa walikuwa wakija uafrika halizuii Watanzania bara kuwa na haki kama wazanzibari. Kama jina la Tanganyika au Tanganyka Territory halipendwi halizuii haki yetu ya kuwa na serekali yetu au nchi yet na hata wakiita Bongo poa tu swala ni usawa.
 
Ni bora angesema Zanzibar ili ungana na Sii Vuzii manake hataki kukubali uwepo wa Tanganyika, pili hao wakoloni wazungu na waarabu mbona wametuachia mambo mengi kwake jina Tanganyika ndo nongwa. Huyu baniani busara yake inamatege?
Hata Zanzibar ni jina lililoacha na waarabu waliokuja kukamata watumwa likimaanisha sehemu ya mijitu myeusi au nigger land. Zanj ni jina la kuzalilisha mtumweusi.
 
Kwa wale Walio Karibu na Shivji ni vyema wamshauri mzee huyu aache kuendelea kuharibu reputation yake na sasa ajinyamazie na kupumzika katika maisha yake ya ustaafu. Kwa mfano, katika hili la kutoijua na kutoitambua Tanganyika, amedandanya tena. Tazama yafuatayo:

ISSA SHIVJI (2006): Let the people speak: Tanzania Down the road to neoliberalism, page 117, Paragraph 6:

Cc: Nguruvi3, mliberali, FJM, tpaul, Pasco, FaizaFoxy, Mtanganyika, MwanaDiwani, gambalanyoka, Ritz, zomba.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mzee msaada wa source ya quote ya nyerere ulio iweka kwenye signature yako.
 
Character X
Kutoijua Tanganyika hakukufanyi uwe manamba hata kidogo. Unaposema wewe ni Mtanzania una maana ya mtu aliyezaliwa katika nchi iliyotokana na mataifa mawili, Tanganyika na Zanzibar. Hilo ndilo limkeuwepo kwa muda mrefu na hakika hakukuwa na hisia za Utanganyika.

Unapoondoa znz katika Utanzania, hubaki na utanzania unabaki na Utanganyika. Kwahiyo wewe utake usitake una 'genes' za Tanganyika. Zanz wameshakataa Utanzania kwa kusema wao ni nchi (katiba 2010). Wanatumia kifungu hicho kukubagua wewe Mtanzania kkwao. Wao wakija kwako wanasema ni Watanzania, wakipanda, wametoka nchi ya jirani.
Ndiyo walioamsha hisia za Utanganyika na kuwafanya Watanganyika wajione ni wapweke.
Nyerere alisema ' kama znz watasema sisi ni wznzn' basi Watanganyika watasononeka. Tananyika itabaki salama.

Pili, Nyerere alisema kama wznz hawataki muungano hatawapiga mabomu.
Leo wakiamua kuondoka katika muungano hatuna sababu za kuwapiga mabomu, ndivyo walivyofanya 2010.
Tunachosema hapa ni kuwa tumebaki wenyewe na hivyo tupewe nafasi ya kujiamulia mambo yetu.

Na wala Tanganyika haitaotoweka kwasababu Shivji kasema haina utaifa. Kama si utaifa sijui wale wazee waliokufa wakipiginia uhuru walikuwa wanatetea uhuru wa nchi gani. Lakini Shivji atueleza utaifa wa wznz ni upi?

Hatuwezi kubaki wenyewe katika muungano uliouawa na wazanzibar 2010,tukajidanganya tuna muungano.
Pengine kinachokuudhi ni jina Tanganyika, elewe kwasasa wewe ni Tanzania ambaye ni peke yako.
Mwenzako akitaka kukutumia anabeba bango lenye jina akisema ni Mtanzania,ukienda kwakewewe ni raia wa nchi jirani. Hakutambui.

Fikiria jambo hili, waziri mkuu ni mtu mkubwa sana katika JMT. Utashangaa nikikumabia kuwa Pinda lazima aombe kibali cha kufanya kazi znz kwasababu yeye hana kibali cha znz mkaazi. Seuse wewe! Hapo Utanzania upo wapi?

Na mwisho, hakuna anayesema Utanzania utafutika kama anavyodai Prof Shivji. Warioba na tume wanasema kuna mambo tutashikirikana kama taifa, kama uhamiaji na uraia.

Lakini kwa vile kuna mambo ambayo znz wanasema yanamneemesha Mtanganyika ni vema tukayaondoa. Kwa mfano, znz waliondoa mafuta na gesi. Iweje gesi ya Mtwara iwe yao?
Kwa mfumo uliopo utawezaje kutenga gesi ya Mtwara na ile 'ya znz' ?

Ili kuwe na usawa ambao Shivji ameueleza katika kitabu chake, ni lazima Tanganyika iwepo ili watu wakae meza moja.
Znz wakisema uvuvi si jambo la muungano, Tanganyika waliondoe katika Tanzania na kulipeleka kwa Tanganyika.
Kama Tanganyika haipo usawa utatoka wapi?

Mfano, znz wana wizara ya afya kwa ajili ya wznz. Wewe Mtanganyika ni mgeni na wala hupati huduma kama Mtanzania.
Waziri wa Afya wa Tanzania ni mzanzibar ambaye anashughulikia jambo lisilowahusu wznz. Hivi huoni kuna kituko hapo?
Kama hiyo inawezekana ni kwanini tusiruhu waziri wa fedha kutoka Uganda, waziri wa kazi kutoka Japan na waziri wa sheria kutoka Uingereza? Kwani kuna tofauti gani?

Mwisho kwani mkataba wa muungano unasemaje kama anavyochambua Mchambuzi? Kipi kigeni kilichochemekwa unachodhani kinalenga kuleta Utanganyika tu bila sababu

Sina lakuongeza. umesema yote
 
Kuhusu Prof. Issa Gulamhussein Shivji, juzi tu tarehe 5/4/2010 kumefanyika marekebisho kwenye profile yake kama inavyopatikana ndani ya Wikipedia; cha kujiuliza labda ni kulikoni? Shivji anadaiwa kuzaliwa Kilosa,Tanganyika tarehe 15, July 1946 (mwaka huu anatimiza umri wa miaka 68) miaka miwili kabla ya kuzaliwa chama cha Tanganyika African Association, TAA mwaka 1948 baada ya Zanzibar kujiondoa kwenye ushirikiano huo. Shivji alizaliwa ndani ya tabaka lililopewa upendeleo maalum na utawala wa Kikoloni iliyowabagua na kuwakandamiza Waafrika kwa kuwaweka katika daraja la tatu; la kwanza likiwa Wazungu, la pili Waasia (jamii ya Shivji) na la mwisho Waafrika. Waasia wa wakati huo hawajatofautiana sana na Waasia wa leo miaka zaidi ya hamsini toka tupate uhuru...jinsi ile ile walivyojipendekeza kwa Wakoloni ndivyo hivyo hivyo hivi leo wanajipendekeza kwa hawa Wakoloni mamboleo, tabaka lililo madarakani.

shivji1.jpg

Wakati chama cha Tanganyika African National Union, TANU, kinazaliwa 7 Julai 1954, Shivji alikuwa na umri wa miaka minane (8) na wakati tunapata uhuru tarehe 9, Desemba 1961, Shivji alikuwa na umri wa miaka kumi na tano (15). Je yawezekana kweli kwamba Shivji haijui Tanganyika wala haihiitaji? Kwa kuamua kuitukana nchi iliyomlea, iliyowapa wazazi wake upendeleo maalum mbele ya Watanganyika, iliyoithamini na inaendelea kuithamini jamii anakotokea kuliko wazawa ni ulimbukeni usiovumilika na usioweza kusameheka. Kwa nini, Prof. Issa Gulamhusein Shivji, anakubali kutumiwa/kutumika kienyeji namna hii? Hajui kwamba juhudi ambazo ameshazifanya kuleta chokochoko na kuchochea uhasama kati ya Tanganyika na Zanzibar, zimeacha ushahidi mpana kama Freeway ya Marekani? Je kinachomsukuma Shivji ni tamaa, unafiki au woga? Hapana Profesa, you owe us an apology and a big one too.
 
Back
Top Bottom