Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji

Hii ndoa kiboko...kuna mume na mke, ghafla mume asili yake imekufa japokuwa bado wanaishi pamoja. Kabaki mke ambae nae hamtaki mume, ndugu wa mume wanamkana ndugu yao kwa kisingizio "eti hajawai kuwepo"

Mfano mzuri sana . utasaidi watanganyika wasiotaka kujishughulisha kujua ujinga wa mfumo wa serekali tulio nao kwa kisingizio cha mfumo wa serikali haumsaidii raia wa kawaida katika maisha yake ya kawaida.
 
Maoni ya Shivji ni mazuri sana hata mimi ninayasapoti; ila tatizo lake ni kuwa anapenda kujenga umoja wa Tanzania kwa kutokea upande mmoja wa Muunagno huku akiwa haoni athari za sehemu moja ya Muungano kujitoa. Hataki kutoa jukumu la umoja huo kwa upande wa Zanzibar. Leo tuna serikali ya Zanzibar ambayo imekuwa inabadili katiba yake mara kwa mara bila kufuata ile katiba ya muungano; hatua zote zikiwa ni kuifanya Zanzibar iwe na autonomy zaidi nje ya Muungano. Chachu ya kuitaka Tanganyika inatokana zaidi na mabadiliko ya utawala wa Zanzibar.

Kwa mfano wakati Zanzibar walipobadili katiba yao kutaka sheria zote za Muungano zinazotungwa huko Dodoma zisifanye kazi kwao mpaka pale baraza la wawakilishi litakapozikubali, hapo ndipo Shivji alipotakiwa kusimama na kuwaambia kuwa huko mnakoenda sipo tunapotaka kwenda kama taifa. Lakini jamaa hao kimya kimya wame-sideline Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile siyo lao, na kulifanya liwe ni Bunge la Tanganyika tu. Tanzania bila Zanzibar ni Tanganyika.

Matusi ya Zanzibar nadhani yametosha sasa, iwapo hawakubaliani na Muungano basi ama tuwe na serikali tatu wakati ile ya Muungano ikiwa na limited powers au tuwe na serikali moja tu yenye nguvu. Hii kuweka weka viaraka na kupotezeana muda na resources tu. Hebu angalia Zanzibar kuna Rais na makamu wawili pamoja na waziri kiongozi wakati vile vile makamu wa Rais wa muungano anatoka Zanzibar; vibosile wote hao wa nini jamani katika nchi ndogo kuliko wilaya moja tu ya Tabora?
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?

Kwa hiyo mtu hawezi kudai Tanganyika simply because siyo Mtanganyika kama alivyokuwa Nyerere? Unadai Nyerere alikuwa Mtanganyika zaidi wakati hapo hapo umem-quote Shivji akimnukuu Nyerere akisistiza kwamba hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila. Hapo Utanganyika wa Nyerere unatoka wapi?

Hata kule Crimea, vijana walizaliwa huku wakiijua Ukraine lakini leo vijana hao ndiyo wameamua kurudi Urusi walitoka mababu zao. The people of Tanzania have the right to self-determination. Kama wakiamua kuwa na taifa lao la Tanganyika, then it does not matter kama walishawahi kuwa Watangayika before.

Otherswise, ni sawa na kusema sie tuliozaliwa na kukulia chini ya utawala wa CCM basi tuendelee kungozwa na CCM tuu. Kwamba hakuna anaeweza kujisifia kuwa yeye ni mwanamageuzi au mtaka mabadiliko. The fact kuwa Tanganyika haukuwepo wakati nilipozaliwa haina maana kuwa siwezi kupenda kuwepo kwa Tanganyika. Who knows may be kabla ya kufariki mababu zangu waliniachia wosia kuhakikisha kuwa Tanganyika inarudi?

Tuache tabia ya kuwafanyia wananchi maamuzi. Let the people decide for themselves. Let the people decide their destination wanayotaka. Kama wanataka kuwa na Tanganyika, Mwanzanyika, Mtwaranyika, Kigomanyika, Mbeyanyika, Arushanyika, n.k who are you kuwapangia? Hii ni nchi yao. Wana mamlaka juu ya nchi yao. Kama wataamua kuivunja hii nchi vipande vipande na kujigawia kama plots then it is up to them.

With due respect, hiyo reasoning aliyoitoa Prof Shivj is too theoretically and does not take into account the realities za siku hizi. Ukimsoma ni kama vile alikuwa anawahadithia watoto wadogo. His argument ya mtu kutodai Tanganyika simply b'se hakukuwwa na Tanganyika alipozaliwa does not make sense. After all, we are no longer living in a Westphalia state.

It is also pity that serikali iliyo madarakani inataka muungano huu uendelee kuwepo kama ulivyo wakati juzi tuu hapo nimemwona waziri wa mambo ya nje akisaini kuitambua Kosovo kiana which speaks a lot kwa Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya nchi.

Watu wapewe uhuru wa kuambua wao wenyewe kama wanataka au hauwaitaki muungano, na kama wanautaka wanataka muungano wa aina gani. Badala ya watu wachache kujifungia ndani ya chumba na kuajiamulia aina ya muungano wanaoutaka, give the people that bit of freedom to directly decide on the matter.
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?
Nyerere aliacha nchi moja yenye serikali mbili, leo tuna nchi mbili zenye serikali mbili; Muungano uko wapi tena. Bunge la Dodoma halifanya kazi Zanzibar, je hilo ni bunge la muungano kweli au ni Bunge la Tanzania-minus-Zanzibar, i.e. Tanganyika?
 
Kwanza ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwakuchangia kwa hoja, na kujibu kwa kunivumilia kama ambavyo demokrasia ya mawazo mbadala inavyo tuelekeza bila ya matusi wala dhihaka, niseme tu wazi sijui Una umri gani wala nafasi gani lakini wewe japo unamtazamo tofauti na wangu lakini ni mmoja Kati ya wale ambao ningetamani kukutana nao nje ya JF na kuzungumza zaidi na zaidi na kwahakika yake Mungu amekupa uwezo mkubwa ndani mwako kuwa muangalifu usipotee.

Pili niende kwenye hoja, nashukuru kwakuiona nia yangu ya dhati nakuiheshimu, kwamba natamani tu umoja wetu kama watanzania ubaki pale pale, kwakua ninaifahamu Tanzania nakuipenda katika umoja wetu tulionao sasa.

Naelewa hoja yako ya msingi kua Tanzania nimuungano wa Tanganyika na Zanzibar na hivyo ikiwa Zanzibar wamejitoa kwenye muungano tunabaki na Tanganyika,

Ninaelewa pia hoja yako ya "kujitoa" kwa Zanzibarkwenye muungano imejengwa juu ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya 2010 lakini ninaomba kujibu kama ifuatavyo;

1. Muungano wetu ni muungano wa nchi mbili lakini ni muumgano wakipekee kidogo. Si muungano wa nnchi mbili zilizo na uuwiano flani Karibu sawa,. Hapana ni muungano wa Nchi Moja Kubwa sana yenye watu Milioni 46 na nyingine Ndogo Kupindukia yenye watu Milioni 1.2, Nchi Moja yenye pato la sh Trilioni 37 na nyingine ndogo yenye pato la chini ya Trilioni 3, nchi moja kubwa ambayo inaungana na nchi nyingine ndogo kiasi ingeweza kuingia kwenye nchi hii kubwa mara 240 kwa maana ya eneo lake.

Lakini pia nchi moja kubwa kwa eneo, idadi ya watu, na pato lake lakini changa kwa maana ya utaifa wake na historia yake,. Na nchinyingine ndogo sana kwa maana ya sifa nilizotaja hapo juu lakini yenye hitoria ndefu ya zaidi ya karne mbili ya taifa la Zanzibar.

Sasa,

Unapotaka kuunganisha nnchi hizi, lazima uzinagatie hayo.!!!

Yani fanya ufanyavyo lakini hakikisha akakainchi kadogo lakini kenye historia yake ya karne nyingi pamoja na udogo wake kasipotee na historia yake kufutwa juu ya dunia tu kwakumezwa na taifa flani kubwa waliloamua kujiunga halo.- kufanya hivyo ni kufanya yaleyale waliyo ya fanya wakoloni miaka ile, ma beberu!!

Hivyo waasisi wakafikiria muundo wa serikali mbili lakini nchi moja ambao ungeitunza historia ya nzanzibar kwaipa kitu kinaitwa (spencial dispensation) utaratibu wakawaida kabisa katika hali za namna hii.,

2. Hoja kuwa Zanzibar imejitangaza kuwa nchi huru sisahihi,. Prof shivji ameeleza vizuri tu namna na mantiki ya neno "Nchi" kamalinavyosomeka kwenye katiba hiyo iliyo rekebishwa ya Zanzibar kwakusema, Zanzibar waliposema wao ninchi walimaanisha ni Dola!! Kitu ambacho siuwongo wala hakimaanishi wamejitoa kwenye muungano, isipokua wanamaanisha hasa kile ambacho waasisi walikimaanisha, kwamba Tanzania iwe nchi moja yenye dola mbili.

Note: kumbuka tofauti kati ya dola, serikali na Nchi.

3. Ninachokipinga mimi ni pale unapowasikia watu flani flani kutoka Zanzibar wakidai kitu kinaitwa "mamlaka kamili" na watu watanganyika wakidai "Dola ya Tanganyika"

Hakika yake ndugu yangu, vitu hivi kuamshwa nikuharibu taifa letu Tanzania na sikulijenga.

Mwalimu huyo uliye m quote maali flani pia aliwahi kusema " kuifufua dola ya tanganyika nikuua muungano".

NB; zingatia takwimu pale juu.

Ndugu, labda pia nikubali kwamba huenda Nina phobia na Hilo neno tanganyika, lakini phobia hii inakuja kwasababu ya ukweli kwamba huyu bwana tanganyika akifufuliwa tu, kitu kinaitwa Dola Ya Tanganyika ikawa dola hai, yenye mamlaka yake! HAKUNA TANZANIA TENA HAPO!! HAKUNA MUUNGANO TENA HAPO!!

Na mwisho kabisa nihitimishe kwakusema mimi na dhani swala hapa nikutatua changamoto za muundo wetu wa muungano, na kuujenga utaifa wetu kwakuwakemea wanaojenga misingi ya utengano. Kuidai tanganyika ATI mwasababu Zanzibar wanadai mamlaka Yao hatumkomoi mtu, tunajikomoa wenyewe tukiibomoa nchi yetu kwa midomo yetu wenyewe,

Ndugu nikualike utafakari tena.

Heshima kwako.

Kwakifupi ulichosema ni kama Zanzibar inaitaji "Prenuptial Agreement" yakulinda mali za Zanzibar kwasababu inaumri mkubwa na watoto wachache wakati haina mali. Ila Tanganyika haiitaji kulindwa malizake kwenye "Prenuptial Agreement" kwasababu ina umri mdogo, mali nyingi na watoto wengi. Hii Sio doa bali chuna buzi
 
Usihukumu eti "walafi wa madaraka". Sina muda wa kutosha ila nimechambua hizo hoja unazo jitanabaisha kwazo na naona hazina mashiko. Wino mwekundu ni hoja na mwanazuoni wako na bluu ni majibu yangu. Nawahi kupalila shamba, ni msimu wa kilimo-mkulima mie so pardon my lack of details as am in a hurry.

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.

Come on Prof. Why stating the obvious? This can be said to be the case for virtually all land masses occupied by black people that later on came to be counties or states as per the definition of the Montevideo Convention.

Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

What is the significance of this obvious historical account? Let me be patient a bit more but unti know you have just wasted my time.

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Three questions "Mr. Professor" 1. "Lakini mwalimu hakupata"...so are you blaming him or complementing him? What is the unstated assumption here on which your statement is based? 2. "Muda wa Kutosha" who defines muda wa kutosha? How do you measure utaifa wa Tanganyika before you come to the conclusion that it was not built? 3. "Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania." Again there is a seriously flawed assumption here, though implicit. Let me put it this way, since for generations as slaves African Americans built the US does that make them white and preclude them from claiming their black heritage?

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka.

This regressive thinking coming from a professor of international repute is making me sick and tired. 1. What if anti-liberation struggles folks asked the same question in the 1950? Is it not a truism that all freedom fighters were born and raised under colonial yoke and consequently they had no clue of what it was to be a country free form white domination? Inashangaza.

"maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka." Without any substantiation, atypical of Professors of his level of achievements, he leaves it for us to fill the gaps. Ironically, he appears to be forgetting that the draft was writen by the likes of Judge (rtd) Warioba and Prime Minister (rtd) Dr. Salim Ahmed Salim. What other position would they want to occupy given also their honorable age? Sheer falacy!

Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

Any link with the substantive part of the draft constitution? This threat is totally misplaced. Who told you factors that lead to the disintergration of those nation states have been listed in the draft for the purposose of implementing them and consequently lead to disintergration? The draft calls for three tier union structure. Hayo yote ni yako! Kaa nayo!
- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.[/QUOTE]
 
Maoni ya Shivji ni mazuri sana hata mimi ninayasapoti; ila tatizo lake ni kuwa anapenda kujenga umoja wa Tanzania kwa kutokea upande mmoja wa Muunagno huku akiwa haoni athari za sehemu moja ya Muungano kujitoa. Hataki kutoa jukumu la umoja huo kwa upande wa Zanzibar. Leo tuna serikali ya Zanzibar ambayo imekuwa inabadili katiba yake mara kwa mara bila kufuata ile katiba ya muungano; hatua zote zikiwa ni kuifanya Zanzibar iwe na autonomy zaidi nje ya Muungano. Chachu ya kuitaka Tanganyika inatokana zaidi na mabadiliko ya utawala wa Zanzibar.
Kwa mfano wakati Zanzibar walipobadili katiba yao kutaka sheria zote za Muungano zinazotungwa huko Dodoma zisifanye kazi kwao mpaka pale baraza la wawakilishi litakapozikubali, hapo ndipo Shivji alipotakiwa kusimama na kuwaambia kuwa huko mnakoenda sipo tunapotaka kwenda kama taifa. Lakini jamaa hao kimya kimya wame-sideline Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile siyo lao, na kulifanya liwe ni Bunge la Tanganyika tu. Tanzania bila Zanzibar ni Tanganyika.

Matusi ya Zanzibar nadhani yametosha sasa, iwapo hawakubaliani na Muungano basi ama tuwe na serikali tatu wakati ile ya Muungano ikiwa na limited powers au tuwe na serikali moja tu yenye nguvu. Hii kuweka weka viaraka na kupotezeana muda na resources tu. Hebu angalia Zanzibar kuna Rais na makamu wawili pamoja na waziri kiongozi wakati vile vile makamu wa Rais wa muungano anatoka Zanzibar; vibosile wote hao wa nini jamani katika nchi ndogo kuliko wilaya moja tu ya Tabora?
Kichuguu , nianzie hapo ulipomalizia. Zanzibar inayosemwa haiwezi kuchangia muungano ndiyo yenye mlolongo wa viongozi uliowataja.

Kuhusu Shivji tatizo la maoni yake lipo sehemu hizi
1. U-turn, amegeuza kibao na kukana maandishi yake ya siku nyingi
2. Uchochezi, ndiye aliyepita znz na kuwaeleza wamoporwa utaifa wao. Leo anasema ni dola
3. Anahoji utaifa wa Tanganyika kana kwamba muungano usingekuwepo utaifa huo usingetokea.
4. Kuegemea znz, kwa utetezi huku akifumbia macho madhila ya Watanganyika.

Kama umesoma huko nyuma, Shivji alitetea uwepo wa serikali 3, mara zote akisema Tanganyika na Zanzibar.

Leo anasema eti kurudi kwa Tanganyika kutachochea kuvunja muungano. Mwaka 2010 hadi sasa amekaa kimya dola ya znz ikichukua madaraka ya dola ya Tanzania.

Kwamba, ni lazima tuombe idhini ya BLW kutenda mambo kwa wananchi wetu. Shivji anasema hilo ni ku table tu mswada kama formality. Sasa kama ni formality kwanini isiondolewe.

Shivji amesahau kuna 2/3 ya wabunge wa znz katika bunge la JMT ambao ni 81.
Nguvu yao inaweza kuzuia jambo la watu milioni 43 tena kwa gharama za watu hao 43M.
Shivji hakUliona hilo kama dispensation, anachokiona ni kurudi kwa Tanganyika.

Shivji yupo katika video akitetea znz kuporwa madaraka na kwamba katiba ya JMT ni haramu kutokana na asili yake.

Ghafla anatumia katiba hiyo haramu kuhalalisha uharamu mwingine ambao anauita uhalali (katiba ya znz 2010)

Katika serikali 3 Shivji hajaeleza mambo yasiyo ya muungano yabebwe na nani.
Akiwa znz anasema lazima kuwepo na mgawanyo wa madaraka na shughuli ili kuleta uwiano.

Uwiano anaoongelea ni ule wa kugawana madaraka. Shivji amesahau kuwa tatizo si madaraka bali mabadiliko ya kiuchumi.

ZNZ inapozuia soko lake la ajira, biashara na ardhi inalenga kulinda uchumi wake.
Kwa shivji hiyo ni sawa, Tanganyika inayobeba lawama za manufaa huku ikiwa imebeba mzigo wa muungano anainyooshea kidole.

Shivji anadai znz lazima ipewe dispensation (upendeleo maalum).
Kwa miaka 50 imepewa dispensation. Tanganyika ikaua utanganyika kwa manufaa ya Tanzania. Ikabeba zigo zito la muungano linalopaswa kuchangiwa pamoja.
Kwa takribani miaka 30 znz haina mchango. Hakuna aliyekuwa analalamika.

Kitendo cha znz kujiita nchi kilikuwa kuvunja muungano. Kitendo cha znz kutojitambua kama Tanzania kilikuwa kuvunja muungano na kitendo cha znz kujitambulisha kama nchi kwa tafsiri yoyote kilikuwa kuvunja muungano.

Kitendo cha znz kuchukua jukumu la bunge la JMT na kuwa juu ni kuvunja katiba na muungano.

Kitendo cha waziri mkuu wa Tanzania ambayo ndiyo nchi kwa mujibu wa Shivji, kwenda znz na kuomba kibali cha kazi na ukaazi ili atekeleze majukumu ya JMT ni kuvunja muungano na kuidharau katiba.

Haya yote Shivji ameyafumbia macho ili kuunga mkono kile alichokikataa miaka nenda miaka rudi. Ameshindwa kutetea uchichezi wake kuhusu muungano, leo anasema kutakuwa na chuki ya Watanganyika dhidi ya wazanzibar.

Angalia, Shivji haoni chuki ya wznz kwa Watanganyika iliyo dhahiri shahiri.
Mtanganyika ni raia wa kigeni znz na hutendewa kila baya pengine kuliko raia wa nchi nyingine.

Hukumu ya Mtanganyika aishie znz inatolewa kwa reference ya Nyerere ambaye ni adui mkubwa wa wznz . Hilo Shivji halioni anachokiona ni chuki watakayopambana nayo wznz.
Kwamba mkuki kwa nguruwe..........

Kwakweli kama kuna siku nilizo wahi kuwa disappointed mojawapo ni ile ya Shivji.
Ameni disappoint pengine kuliko Kinana.

Kinana pamoja na mambo yote at least amenyanyua ulimi na kusema walichokifanya wznz ndicho kilichochea haya licha ya ukweli kuwa serikali 3 ni burning issue kwa muda mrefu.

CUF walikuwa na sera ya serikali 3, Shivji hakuwahi kukemea. Wznz wanataka serikali 3 na wengine kuvunja kabisa muungano ili tuwe na MoU inayoitwa mkataba. Hayo madai ameyasikia katika mikutano yake znz. Hakuwahi kukemea bali kuchochea kuni. Leo kuni zina moto anageuka na kusema Warioba ni mbaya. Kwanini si Maalimu aliyeanza miaka zaidi ya 20.

Anamshambulia Warioba ili iwe njia ya kuwashambulia Watanganyika. Hakumbuki tena kuwa madai yake ya siku za nyuma na mikutano yake znz ilianza kabla ya tume ya Warioba.
Shivji hawasemi wznz kwasababu wana dispensation, kwamba hata wakivurunda historia na utamaduni wao ulindwe. Hata wakivunja katiba anasema dispensation.

Eti tukieleza jinsi Mtanganyika anavyopinda mgongo kwa ajili ya mznz tunaambiwa hiyo ni chuki. Kwamba, raha ni Mtanganyika kulipa bill za mznz.

Shivji anatetea kwa kupulizia uvundo marashi. Yupo bize na perfume akitaraji siku moja lundo la uchafu litageuga kuwa mlima wa dhahabu. Shivji amesahau mbegu za chuki alizonyunyiza znz, anaona ukakasi wa Tanganyika kuwepo.
 
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?

Kwahiyo wamarekani wa Leo hawawezi kujisifia wao ni wamarekani kuliko Abraham Lincoln? Hiyo zaidi ya kitu gani?! Kwan kwenye utaifa kuna aliye zaidi?
 
Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!
Acha kujifanya wewe ni Nyerere gamba mkubwa wewe
 
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.

ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.
Ndugu maneno aliyo yasema Prof. Yameishia pale nilipo weka inverted comas za mwisho, na kuweka citation, - Prof. Issa Shivji 2014

Maneno yaliyo endelea baada ya hapo yakiwemo maneno " Tanganyika siijui wala siihitaji nimaneno YANGU BINAFSI na yasihusishwe kwa namna yoyote ile na Prof. Issa Shivji.

Ni maneno ambayo nimeyasema Mara myingi katika posts zangu hapa, na hivyo maelezo hasa juu ya utanganyika aliyo yatoa Prof. Shivji yalinipa nafasi ya kuyarudia tena maneno hayo "Tanganyika siijui wala siihitaji"

Narudia tena, maneno hayo si ya shivji Bali yangu binfsi na yasihusishwe na shivji.

Maneno yake kama nilivyo mnukuu yanaishia kwenye inverted commas.

Asante
 
Nyerere aliacha nchi moja yenye serikali mbili, leo tuna nchi mbili zenye serikali mbili; Muungano uko wapi tena. Bunge la Dodoma halifanya kazi Zanzibar, je hilo ni bunge la muungano kweli au ni Bunge la Tanzania-minus-Zanzibar, i.e. Tanganyika?

ninacho Karibu kuonyesha hapa kwakuuliza swali hili ni kuwa kama kuna mtu aliamka na kuidai Tanganyika huru inayo jitegemea na kujiongoza basi ni mwalimu nyerere,. Na kama mwalimu huyo huyo aliiua Tanganyika akaizika akaunda Tanzania akaisemea na akaonya juu ya kuifufua Tanganyika sisi unaijua Tanganyika kuliko yeye? Au ndo tunajifanya tunaasili ya Tanganyika kuliko nyerere!??

Ndugu zangu Utengano sikuzote ni ugonjwa na dhambi mbaya sana. Kubaguana huku kutatumaliza kabisa!!

Nasema hatuwezi kususia muungano ATI kwasababu ya marekebisho ya katiba ya Zanzibar. Haiwezekani!!!

Kama swala ni marekebisho basi tukaetuzungumze turekebishe tusonge mbele!

Utanganyika utaua muungano.
 
Kwahiyo wamarekani wa Leo hawawezi kujisifia wao ni wamarekani kuliko Abraham Lincoln? Hiyo zaidi ya kitu gani?! Kwan kwenye utaifa kuna aliye zaidi?

ninasema hivi, kama nyerere ndiye aliye pigania uwo uhuru wa iyo Tanganyika na baadae akaiua Tanganyika na kuunda Tanzania!!

Naakatuusia akisema " kuifufua dola ya Tanganyika ni kuuwa muungano"

nikusema nyerere yeye hakuwa mtanganyika kama tulivyo sisi? Au hakua na uzalendo??
 
Kisa jina walitoa wazungu ndo hatuwezi kuwa taifa, huyu profffesa bogas kabisa, basi tunabadili jina kuanzia leo taifa letu litaitwa Tanganyusi haya tupeni uhuru wetu,
 
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.

ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!

Nanukuu,

"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa ‘Utaifa wa Tanganyika’ bila kudadisi kihistoria ‘Utaifa wa Tanganyika’.

Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa’ ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika’ chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika’ na iliitwa ‘Tanganyika Territory’, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African’, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.

Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"

- Prof. Issa Shivji 2014.

Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!

Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!

Comrades ninashukuru sana.

Kukata mzizi wa fitina: Nchi moja, Serikali moja
 
We need our country back,nimechoka kunyanyaswa nikienda zanzibar
 
Ninakumbuka ya Amil Jamal. Hawa wenzetu wana uraia pacha. Jamal alikuwa Waziri wakati wa Nyerere na pia Mbunge wa Morogoro. Baada ya kufariki amezikwa Canada kama sijakosea! Hivyo hivyo kwa huyu Bwana unaweza kukuta naye ni raia wa Canada! Kila kitu kinawezekana katika nchi hii.

Hawea ni wasanii wa Kihindi....na huyo Amir Jamal aliaminika kweli na Nyerere...unajua Familia yake inavitega uchumi kibao hapa Bongo wamekuja kwa style nyingine wanajifanya wametoka Kenya wana makampuni yako chini ya AJ Group (Amir Jamal Group of Companies)....imo New Africa Hotel and Casinno, SCI Tanzania Limited, Tanganyika Motors, Twiga Chemicals wana Apartsments.....ila watu wanasema oooh huyu Amir Jamal hajaiba kitu chochote hapa bongo.
 
Proffesor mmoja pale UDSM siku moja wakati anafundisha mambo ya Adult Education akatoa akaelezea hii kitu kuwa ukimuona Professor sio kuwa ndio the most learned person but viceversa is true, yaani anaacha kusoma mambo mengiiii halafu mtu unayeweza kumuona leop ana akili kesho unaweza kumuona ni empty headed hata kwa mambo ambayo ni simple tu....Shivji pumzika
Kwa wale Walio Karibu na Shivji ni vyema wamshauri mzee huyu aache kuendelea kuharibu reputation yake na sasa ajinyamazie na kupumzika katika maisha yake ya ustaafu. Kwa mfano, katika hili la kutoijua na kutoitambua Tanganyika, amedandanya tena. Tazama yafuatayo:

ISSA SHIVJI (2006): Let the people speak: Tanzania Down the road to neoliberalism, page 117, Paragraph 6:

Cc: Nguruvi3, mliberali, FJM, tpaul, Pasco, FaizaFoxy, Mtanganyika, MwanaDiwani, gambalanyoka, Ritz, zomba.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Anatambua kuwa siku Tanganyika ikirudi, as Kanjubay hana chake hap!
 
Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na ‘German East Africa' ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la ‘Tanganyika' chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili ‘Tanganyika' na iliitwa ‘Tanganyika Territory', yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye ‘African', Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).

Unajaribu kufuta neno Tanganyika lakini halifutiki na halitafutika kamweeeee!!!! kama unatambua uwepo wa Rwanda na Burundi katika GEA , unashindwa vipi kutambua uwepo wa Tanganyika hata kama imeundwa na waingereza???? kama ni naming hata Kenya & Uganda ziliitwa British East Africa, je leo hatuna Kenya na Uganda??
 
Back
Top Bottom