BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,379
- 8,123
Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Rashid Mfaume amebaini ukiukwaji wa manunuzi ya vifaa ikiwamo jokofu za kuhifadhia damu katika kituo cha afya Mwalugulu, katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Dkt. Mfaume amebaini hayo wakati wa kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa afya katika kituo hicho akiwa ameambatana na timu ya afya, ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo majokofu mawili yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwa ajili ya kuhifadhi damu yakabainika kuwa ya matumizi ya nyumbani.
“Ni majokofu kwa ajili ya kufungia nyanya,karoti na parachichi na wataalamu wametuthibitishia kuwa haya sio majokofu ya damu, huyu mzabuni tumemlipa bila kukagua tumeagiza majokofu ya kutunzia damu tumeletewa majokofu ya matunda” Amesema Dkt. Mfaume.
Kufuatia hatua hiyo Dkt. Mfaume ameelekeza mfamasia wa halmashauri kuondolewa kwenye nafasi yake kwa kutoa taarifa ya uongo wakati wa ukaguzi wa vifaa huku akielekeza kuonywa kwa maandishi kwa wajumbe wa timu ya usimamizi wa shughuli za Afya ya Halmashauri (CHMT) ya Msalala.
JAMBO TV