Dkt. Dugange aagiza uchunguzi ufanyike ujenzi wa Kituo cha Afya Malengamakali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

DKT. DUGANGE AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE UJENZI WA KITUO CHA AFYA MALENGAMAKALI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya mhe. Dkt. Festo Dugange ameielekeza ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuunda timu ya uchunguzi kukagua matumizi ya fedha nza usimamizi wa ujenzi wa kituo cha Afya Malengamakali kilichopo Mkulula kata ua Malengamakali halmashauri ya Iringa Vijijini.

Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo baada ya kutilia shaka usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho ikiwemo majibu yasiyoridhisha kutoka kwa mkurugenzi mtendaji, mganga mkuu na mhandisi wa halmashauri hiyo tarehe 19.12.2023

“Sijaridhiwa na utekekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Malengamakali na itoshe kusema utekelezaji ni mbaya thamani ya fedha hapa sujaiona kwasababu hakuna jingo lililokamilika kwa asilimia 100,hakuna tathimini ya fedha zilizotumika kwa kila jengo haijulikani kila kitu kimekwenda holelaholela haijulikani kiasi gani watendaji hawako ‘serious’ hakuna ‘commitment’ mhe. Rais ameleta milioni 500 mwaka 2021 /22 leo tunsongea mwaka 2024 bado wiki moja watendaji hawana majibu kituo cha Afya hakijakamilika na wananchi wanahitaji huduma na umbali hap ani kilomita 34 kutoka vijiji vingine kuja kupata matibabu hapa leo mkurugenzi anaongelea kituo kitakamilika Octoba 2024”. Amesema Dkt. Festo Dugange

Aidha,amemwekeza Tawala mkoa huo hufanya uchunguzi huo mapema iwezekanavyo na kuwasilisha taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI na taarifa isiporidhisha timu nyingine ya uchunguzi itetumwa kutoka Ofisi ya Rais

“Tmu hiyo tunataka iwe na wataalamu ikiwemo wakaguzi wa ndani wa mkoa,TAKUKURU mkiwapata na watu wa CAG waje wachunguze thamani ya fedha iliyoletwa, kazi iliyofanyika na tusiporidhishwa na taarifa hiyo tutaleta timu nyingine na tutachunguza kama DMO pamoja na DED kama mnatusaidia au lah na hatutawavumilia watendaji ambao hawatimizi majukumu yao” Dkt. Festo Dugange

Hata hivyo wananchi wa Kijiji cha Mkulula akiwemo Asia Makambi,Lupumuko Chungu na Magreth Sigila wamesema kukamilika kwa kituo hicho kitasaidia akina mama wajawazito na wazee wanaosumbuliwa na magonjwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
 

Attachments

  • GBy94ImWAAAUAzu.jpg
    GBy94ImWAAAUAzu.jpg
    412.8 KB · Views: 4
  • GBy94ImWwAIH0xH.jpg
    GBy94ImWwAIH0xH.jpg
    265.7 KB · Views: 4
  • GBy94IvW0AAimSh.jpg
    GBy94IvW0AAimSh.jpg
    268.4 KB · Views: 3
  • GBy94IoXgAAJ7o8.jpg
    GBy94IoXgAAJ7o8.jpg
    211 KB · Views: 4
  • GBy95ovXsAAoHYN.jpg
    GBy95ovXsAAoHYN.jpg
    203.7 KB · Views: 1
  • GBy95o5WkAE0tlI.jpg
    GBy95o5WkAE0tlI.jpg
    146.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom