Shilingi Milioni 251 zatengwa kulipana posho kuondoa machinga Jiji la Mwanza,wanaolipwa CD, DC na wenzao

Hizo pesa si zinatosha kabisa kuwajengea miundombinu mizuri hao Machinga.

Waziri Ummy fuatilia Hawa na ikibainika watimue hao Wakurugenzi.
Yaani watu waache wake zao na waume zao usiku kuja kuhakiksha mnaondoka halafu mnakuja hapa na oh posho sijui nini. Kwanza hiyo posho lazima ilipwe na machinga wote walazimishwe kuifidia
 
Yaani watu waache wake zao na waume zao usiku kuja kuhakiksha mnaondoka halafu mnakuja hapa na oh posho sijui nini. Kwanza hiyo posho lazima ilipwe na machinga wote walazimishwe kuifidia
Askari wamo kwenye hiyo posho?
 
Yaani na hawa nao watapewa pesa ya kujenga madarasa.
 
Zoezi la kuwahamisha machinga jijini mwanza nahisi tathimini ya kina haikufanyika.kwanza machinga wenyewe hawako tayari kupelekwa eneo ambalo si sahihi kwa biashara zao.Eneo Ni uwanja ambao ulikuwa ukitumika Kama gulio kwa Siku ya jumanne.vimekatwa vipande vidogo vidogo vyenye ukubwa wa mita 1.5,kiasi kwamba hakuna machinga anayetaka eneo dogo kiasi hicho.

Taratibu za kuwapata machinga ili kugawiwa maeneo hayo zilikuwa ni za kihuni ,walikuwa Kila wanayemkuta sokoni siku hiyo anauza bidhaa au Kama dalali alisajiliwa Kama machinga.

Eneo Hilo limegawanywa kwa aina ya biashara mfano mitumba,vipodozi,viatu nk kiasi kwamba hakuna machinga anayekubali utaratibu huo.

Inaonekana Kuna Kila aina ya urasimu katika kugawa maeneo hayo.machinga wenye mitaji mikubwa ndiyo wamepewa namba za kuanzia 1-50 ambazo ndiyo zipo barabarani kwa mujibu wa uwanja.Inaonekana wahusika wamepewa fedha na kugawa maeneo kwa misingi ya rushwa.zoezi la ugawaji lilikuwa ijumaa kwa machinga wa makoroboi,Uhuru,kaluta lakini lilishindikana kutokana na machinga kutokukubali utaratibu wa kugawiwa maeneo.

Ushauri wa msingi kuwa Hilo zoezi la ugawaji wa maeneo usimamishwe kwani wapo waliopewa maeneo zaidi ya moja kiasi kwamba wengine wamekosa.wapo machinga ambao Siku ya kuorodheshwa hawakuwepo either walikuwa wamefiwa,wamelazwa,wanaoa,kuelewa,wagonjwa hao hawakupewa maeneo.

Eneo Hilo la uwanja limeua ndoto za wadogo zetu kimichezo.
 
Uwanja wa mchafukoga siyo wa shule usidanganye hapa. Wala hauingiliani na shule yoyote hapo. Kwa sababu Azimio Primary School iko mbali na uwanja huo. Mtoa uzi ni mmachinga amejificha nyuma ya kujiita diwani.
 
Lazima wahame tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…