Halmashauri ya Jiji la Arusha Yatenga Milioni 380 Kukarabati Maeneo Yaliyoharibiwa na Mvua

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga kiasi cha Sh milioni 380 ili kurudisha miundombinu ambayo imeanza kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jij la Arusha, Juma Hamsini alisema hayo juzi wakati akizungumza katika mkutano wa madiwani kwenye kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 uliofanyika katika ukumbi wa Jiji la Arusha.

Alisema ili kukabiliana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu ya barabara, na majengo ya serikali, halmashauri hiyo tayari imetenga fedha hizo ili kukabiliana na uharibifu huo.
"Ili kukabiliana na uharibifu wa El Nino tayari tumetenga kiasi cha Sh milioni 380 na hizi hela zitaenda Tarura kwa ajili ya kurudisha miundombinu ya barabara zinazoharibika kutokana na mvua," alisema.

Alisema halmashauri ya jiji hilo inaendelea kukusanya mapato zaidi kwa ajili ya kuboresha jji hilo la kitalii huku akisema kuwa tayari wameshaweka kamera 10 za majaribio za kufuatilia mienendo ya uhalifu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa alitoa onyo kwa watendaji wa halmashauri ya jiji hilo kutokwamisha ajenda za maendeleo na kusimamisha kampuni binafsi zinazojihusisha na upimaji ardhi kutopima viwanja vyenye mita za mraba 10x10 katika eneo ambalo utajengwa uwanja mkubwa wa mashindano.

"Mtu yeyote anayekwamisha ajenda za maendeleo ndani ya jiji ataondolewa nafasi yake. Lengo letu tunataka kubadilika na kila kinachoku-sanywa kiende kwenye shughuli za maendeleo. Ni marufuku kampuni binafsi kupima viwanja vya 10x10, tunataka kuweka mpangilio wa hadhi wa jiji. Hizi kampuni zimeharibu sana hadhi ya jiji.

Hivyo mtu yeyote atakayenunua kiwanja cha 10x10 hatapewa hatimiliki," alisema.

Álisema kuna haja ya kuongeza kasi ya kukusanya mapato ndani ya halmashauri ya jiji hilo kwa sababu hata Rais Samia anahimiza hivyo.
 
Halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga kiasi cha Sh milioni 380 ili kurudisha miundombinu ambayo imeanza kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jij la Arusha, Juma Hamsini alisema hayo juzi wakati akizungumza katika mkutano wa madiwani kwenye kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 uliofanyika katika ukumbi wa Jiji la Arusha.

Alisema ili kukabiliana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuharibu miundombinu ya barabara, na majengo ya serikali, halmashauri hiyo tayari imetenga fedha hizo ili kukabiliana na uharibifu huo.
"Ili kukabiliana na uharibifu wa El Nino tayari tumetenga kiasi cha Sh milioni 380 na hizi hela zitaenda Tarura kwa ajili ya kurudisha miundombinu ya barabara zinazoharibika kutokana na mvua," alisema.

Alisema halmashauri ya jiji hilo inaendelea kukusanya mapato zaidi kwa ajili ya kuboresha jji hilo la kitalii huku akisema kuwa tayari wameshaweka kamera 10 za majaribio za kufuatilia mienendo ya uhalifu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa alitoa onyo kwa watendaji wa halmashauri ya jiji hilo kutokwamisha ajenda

za maendeleo na kusimamisha kampuni binafsi zinazojihusisha na upimaji ardhi kutopima viwanja vyenye mita za mraba 10x10 katika eneo ambalo utajengwa uwanja mkubwa wa mashindano.

"Mtu yeyote anayekwamisha ajenda za maendeleo ndani ya jiji ataondolewa nafasi yake. Lengo letu tunataka kubadilika na kila kinachoku-sanywa kiende kwenye shughuli za maendeleo. Ni marufuku kampuni binafsi kupima viwanja vya 10x10, tunataka kuweka mpangilio wa hadhi wa jiji. Hizi kampuni zimeharibu sana hadhi ya jiji.

Hivyo mtu yeyote atakayenunua kiwanja cha 10x10 hatapewa hatimiliki," alisema.

Álisema kuna haja ya kuongeza kasi ya kukusanya mapato ndani ya halmashauri ya jiji hilo kwa sababu hata Rais Samia anahimiza hivyo.
"na majengo ya serikali", ni kichocheo cha upigaji.
 
Back
Top Bottom