Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

Nakwambia hapo wanatuzuga tu, wanataka watu waelekeze macho kwa shibuda na wengine watakaojitokeza, kwasababu watu wenyewe hawana hata upinzani kwa JK, so JK atachukua kiulaini, wanataka kuelekeza current issues za watz kwa shibuda na wengine watakaokuja,

Watasahau kum-criticise mkuu wa nchi kama watu walivyosahau Richmond na Mkapa baada ya ufisadi wa bank kuu na kuanza kuburuzwa mahakamani kwa kina mramba, hii nayo ni njama ya kufunika kinachoendelea,...

Siasa ni kitu kilaini sana aisee, unaweza kuwachezea watu akili hivihivi vile upendavyo.
 
Ni haki yake kikatiba. Tusimhukumu kwa kujitimizia haja ya nafsi yake.
Na hakuna aliye na ushahidi kati yetu kuwa katumwa.
Hakuna mpumbavu anaekubali kutumwa na mtu wakati tayari ameshaambiwa atakaepambana
nae kifo kinamsubiri. Sidhani kama mtu anaakili timamu anaweza kutumwa kwa staili hiyo.
Tumuache shibuda. Maisha yanautamu wake kwa watu kama hawa wanapokuwepo ktk
ulimwengu huu. Haijalishi mtazamo wake uko jamani.
 
Hapa tutaka kuona je ule utamaduni wa 'kuachiana' kwa rais kumaliza kipindi chake utafatwa?
Maana Dr. Bilal alipotaka kumtoa "kibaraka" wao, aliambiwa hakuna demokrasia hiyo ndani ya CCM, kuna utaratibu wa chama wa "kuachiana" mpaka rais amalize vipindi vyote viwili, je na Shibuda naye atafanyiwa kama hivyo au wakati ule CCM bara walikuwa na lao kuifisidi Zanzibar kupitia kibaraka wao Karume?
 
Pole pole mkuu asije kusikia Karume na kuhairisha huruma yake ya kushirikiana nanyi kafu huko zenji mkuu wangu.
 
Kuna mambo mengine inabidi kuyaangalia kwa umakini kabla ya kukubaliana nayo.Hili la Shibuda nalo ni mojawapo kwangu. Does he mean what he says au anataka kutuchanganya akili maana hii ni moja ya majukumu ya "kazi za kudumu" za watu wa aina ya Mheshimiwa Mrema. To save the master by any means.
 
Hapa tutaka kuona je ule utamaduni wa 'kuachiana' kwa rais kumaliza kipindi chake utafatwa?
Maana Dr. Bilal alipotaka kumtoa "kibaraka" wao, aliambiwa hakuna demokrasia hiyo ndani ya CCM, kuna utaratibu wa chama wa "kuachiana" mpaka rais amalize vipindi vyote viwili, je na Shibuda naye atafanyiwa kama hivyo au wakati ule CCM bara walikuwa na lao kuifisidi Zanzibar kupitia kibaraka wao Karume?
Janius, utaratibu huo wa kuachiana ndio utaratibu wa CCM tena Dr. Bilal ana bahati alifika hadi NEC, Huyu Mhe. Shibuda hata wilayani havuki nadhani hata ubunge ndio bye bye, "huyu ni boya tuu kwenye maji linaelea, au ubua, unapulizwa tuu na upepo unaanguka, au kama ni mti, basi ni mpapai, tena mpapai dume, haufai kwa kivuli, kwa kuni na tena wala hauzai matunda"

Nikija kuhusu 'Kibaraka', ni afadhali ya kibaraka mleta heri, kuliko mwana Sultani mleta shari!, atakayewarudisha Wanzanzibari utumwani kwa Waarabu na kurejesha usultanini. Sio siri, 'Dr. Bilal is the best President Zanzibar can have as a nation', ila kwa vile Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ni JMT ndio inadetermine nani aiongoze ZnZ kwa maslahi ya Muungano ndio maana siku zote, Maalim anapokwa tonge mdomoni, Dr. Bilal mhafidhina, Nahodha haaminiki sana, Khatib yuko too ambitious, hivyo the next ZnZ pres ni Dr.Shein, hana makuu au Dr. Mwinyi, mtake msitake. .
 
nakwambia hapo anataka kutupoteza mwelekeo, tutakapokuja kugundua, jamaa ameshakalia kiti tena kule ikulu...hao ni hao hao tu, wana akili za kulaghai kama nini. hadanganywi mtu hapa. si alianza muda tu kuongea hili....
 
Kugombea imekuwa kama fasheni never miss, mrema, lipumba, seif type mwishowe watu wanawaona kama waigizaji tu.
 
...Dr. Bilal mhafidhina, Nahodha haaminiki sana, Khatib yuko too ambitious, hivyo the next ZnZ pres ni Dr.Shein, hana makuu au Dr. Mwinyi, mtake msitake.

Ngoja tuamue aina ya ligi tunayotaka kucheza...halafu SMT waone kama wao na wakoloni wepi walikuwa majabari?
 
Shibuda ogopa politics zinazotegemea unajimu kama njia mojawapo ya campaign! Si uhamie tuu CCJ!
 
Shishangai na wengi hawatashangaa kusikia jina na Shibuda likihusishwa na kuchukua fomu za urais kwa tiketi ya CCM - hizo ni propaganda tu hakuna jipya.
 
Janius, utaratibu huo wa kuachiana ndio utaratibu wa CCM tena Dr. Bilal ana bahati alifika hadi NEC, Huyu Mhe. Shibuda hata wilayani havuki nadhani hata ubunge ndio bye bye, "huyu ni boya tuu kwenye maji linaelea, au ubua, unapulizwa tuu na upepo unaanguka, au kama ni mti, basi ni mpapai, tena mpapai dume, haufai kwa kivuli, kwa kuni na tena wala hauzai matunda"

Nikija kuhusu 'Kibaraka', ni afadhali ya kibaraka mleta heri, kuliko mwana Sultani mleta shari!, atakayewarudisha Wanzanzibari utumwani kwa Waarabu na kurejesha usultanini. Sio siri, 'Dr. Bilal is the best President Zanzibar can have as a nation', ila kwa vile Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ni JMT ndio inadetermine nani aiongoze ZnZ kwa maslahi ya Muungano ndio maana siku zote, Maalim anapokwa tonge mdomoni, Dr. Bilal mhafidhina, Nahodha haaminiki sana, Khatib yuko too ambitious, hivyo the next ZnZ pres ni Dr.Shein, hana makuu au Dr. Mwinyi, mtake msitake. .

PASCO,
huo mfananisho wa shibuda na mpapai dume umenifanya nicheke sana.
 
Shibuda,Shehe Yahaya nk ndani ya CCM ni wasanii tu na wanataka mambo muhimu kwa chi yetu tuyachukulie kiutani utani. Ni wa hatari sana hawa.
 
Back
Top Bottom