BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Msekwa: Shibuda hamuwezi Kikwete
Na Yusuph Katimba
Majira
17 October 2009
MIZENGWE ya kurudisha nyuma juhudi za Mbunge wa Maswa, John Shibuda kutaka kukamilisha nia yake ya kumng'oa Rais Kikwete katika uchaguzi wa kiti cha urais mwakani inazidi kutokota baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pius Msekwa kusema kuwa hana ubavu wa kumpiku Rais Kikwete.
Alisema kuwa licha ya katiba ya CCM kuruhusu kila mwanachama aliye na sifa kugombea, lakini bado mbunge huyo hawezi kumtetemesha Rais Kikwete katika nafasi hivyo.
Bw. Msekwa alitoa kauli hiyo alipozungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC jana. Bw. Msemkwa pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa kila mwanachama anayo sifa, na kuongeza kuwa baada ya mwanachama kuchukua fomu na kurejesha, mchakato hupita na kuwa yule aliye na sifa ndio hushika hatamu huku akimtaja Rais Kikwete kuwa ndiye aliye na sifa kwa sasa.
Bw. Shibuda amekuwa akikumbwa na misukosuko mbalimbali ndani ya chama chake. Julai mwaka jana, alijikuta akitimuliwa nje ya kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Maswa.
Ilidaiwa kuwa hakuwa mjumbe halali wa kamati ya siasa. Alitimuliwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Bw. Peter Bunyongoli na Katibu Mwenezi na Itikadi, Bw. Jeremiah Makondeko.
Baada ya kutangaza nia yake ya kumng'oa Rais Kikwete kwa kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani, alipingwa huku akisema ana uwezo wa kumung'oa na kuongoza nchi.
Pia alionesha kushangazwa na uamuzi wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) kuondoa jina lake katika kinyanganyiro cha nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.
Kipindi hicho, alikaririwa na vyombo vya habari akisema, Potelea mbali, liwalo na liwe, nimechoka kuwa mfungwa wa kisiasa ndani ya CCM wakati nina uwezo wa kuwaongoza Watanzania.
Akizunguimzia suala la rushwa jinsi inavyohusishwa katika uchaguzi, Bw. Msekwa alisema suala la fedha kuhusishwa katika uchaguzi ni suala la kawaida kwa kuwa hakuna uchaguzi unaofanyika bila kutumia fedha. Aliongeza kuwa rushwa na matumizi ya fedha lazima vitenganishwe.