Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,936
Sheikh yahya hussein upo???
Watu hawataki kusikia wosia wako...
Jamaa hasipokua Shekh atakuwa mzushi na kazi yake kushinei!
Sheikh yahya hussein upo???
Watu hawataki kusikia wosia wako...
Shibuda = Mr Bean
Sheikh yahya hussein upo???
Watu hawataki kusikia wosia wako...
Du!!! Maskini Shibuda!!!! Haogopi kufa, mbona waliambiwa na mtabiri kuwa atakayempinga JK kufa ghafula bin vuuu.Natazma taarifa ya habari TBC daaaah Shibuda anatangaza live kuwa anamvaa JK kugombea u rais..haya yetu macho
Shibuda ngonjera, mashari na mipasho ndio vinamfaa! Hawezi kuwa kiongozi wa nchi inayohitaji mapinduzi ya kiuchumi! Dr Pombe, Dr Slaa ndio aina ya viongozi wanatakiwa Tanzania!
Kugombea imekuwa kama fasheni never miss, mrema, lipumba, seif type mwishowe watu wanawaona kama waigizaji tu.
Janius, utaratibu huo wa kuachiana ndio utaratibu wa CCM tena Dr. Bilal ana bahati alifika hadi NEC, Huyu Mhe. Shibuda hata wilayani havuki nadhani hata ubunge ndio bye bye, "huyu ni boya tuu kwenye maji linaelea, au ubua, unapulizwa tuu na upepo unaanguka, au kama ni mti, basi ni mpapai, tena mpapai dume, haufai kwa kivuli, kwa kuni na tena wala hauzai matunda"
Nikija kuhusu 'Kibaraka', ni afadhali ya kibaraka mleta heri, kuliko mwana Sultani mleta shari!, atakayewarudisha Wanzanzibari utumwani kwa Waarabu na kurejesha usultanini. Sio siri, 'Dr. Bilal is the best President Zanzibar can have as a nation', ila kwa vile Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ni JMT ndio inadetermine nani aiongoze ZnZ kwa maslahi ya Muungano ndio maana siku zote, Maalim anapokwa tonge mdomoni, Dr. Bilal mhafidhina, Nahodha haaminiki sana, Khatib yuko too ambitious, hivyo the next ZnZ pres ni Dr.Shein, hana makuu au Dr. Mwinyi, mtake msitake. .
Mkuu nakuambia huyu Shibuda ni mbabaishaji aliyekithiri. Ukiangalia CV zake katika tovuti ya Bunge nikuwa elimu yake ni kidato cha nne tuu. Kwani yeye hajui kuwa katiba ya CCM haiwezi kumpitisha kwa vile hana shahada? anajua sana ila anatuzuga tumwone wa maana na tusifikiri mambo mengine ya msingi ila yeye. Lakini ndivyo walivyo CCM, lao ni moja tuu.Hivi kwanini mnamdharau Shibuda? ananini cha ajabu? mimi kwangu Shibuda ni jasiri na shujaa. Shibuda amekuwa mtu muhimu katika siasa za CCM toka miaka mingi. Kipindi cha Mkapa (M/kiti wa chama) alikuwa anaamua kufanya fitina ili Shibuda asifike kwenye kikao kwa kuogopa hoja pinzani na pengine ,badala toka kwa Shibuda. Tatizo lake hana mtandao unaoaminika ndani ya chama.
Lakini hii itabakia changamoto kwa CCM na watu tunaodhani wanauwezo zaidi ya Kikwete kama Dr. Salim, Prof. Mwandosya, Jaji Bomani, Dr. Magufuli nk kuachana na utamaduni wao na kuchukua fomu.