Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

Shibuda apania kugombea dhidi ya JK CCM, ajitoa ghafla

Hahahahah Sheikh Yahya aliishaonya ....nani haogopi kifo?
 
nani anapenda unafiki kama huu, hivi kuwadanganya watz kwa kuwapiga changa la macho hivi haoni kama ni kujipunguzia heshima zake?
 
Jamani kwani mlitaka Shibuda aingie uwanjani ageweza mziki??Bora tu aachie ngazi
 
Isije ikawa kulipigwa mkwala mkuu au ni watu wametumwa kumwambia mzee chibuda acha ili tuonekane chama chetu kina nidhamu sasa nadhani ni nidhamu ya woga mbona Democrat ya akina obama watu walienda mpaka round ya mwisho na wakaamua wananchi weneyewe nani apewe na akaibuka Obama sasa hapa kwetu mbona hilo hawakuliweka katika sheria ya uchaguzi si wanajijua wengi wao wana CCM watyapigwa bench la kufa mtu
 
Tukiachilia mbali mkwala wa Sheikh Yahya... Shibuda kweli angeweza fitna za wana CCM hata kumpiku JK? .na hata kama angeweza cheza na hizo fitna,Watanzania wangemchagua kweli kuwa Raisi wao?

Bora tu kagundua mapema maana chances za yeye kupita hata tu huko kwenye kura za maoni sizioni.
 
To be honest nilitarajia hili.Kazi kweli kweli,cheap popularity inatafutwa kwa kila engo.
 
Mimi kwanza huyu mswahili sikumuweka akilini kama anafanya kitu kabisa...toka mwanzo nilijua kuwa ni mpiga soga za kawaida tu ili kupiga watu mchanga wa macho.

Hivi hata angegombea, Shibuda jamani ndo awe rais wetu, si bora tungempa hata Mrema kuliko Shibuda...hivi mnaona kama ametulia yule kwa upigaji domo wake na uswahili alonao?

Kitu kimoja anaweza kuongea maneno alfu moja tena ambayo si ya mtu mzima aliye serious, ni kama utani vile yaani porojo porojo...hao watu wa Maswa wana shida...na atapita kwenye ubunge wake kwasababu kwa kupiga kiswahili anajua kuliko wabunge wote wa tz na ni rahisi kuwalaghai watu wa Maswa kwa kiswahili chake..
 
Ukifuatilia kwa umakini vituko anavyofanyiwa JK na watendaji wake; mara magari, mara wamdanganye and so on, si ajabu kamati kuu ikaamua kumpitisha Shibuda. Msidharau wakuu!!
 
Leo kwenye taarifa ya saa 12 jioni nilisikia kama ametangaza kujitoa na kumwachia JK vile!
 
Nashangaa kuona wapo watu walioamini kwamba Shibuda kweli ana nia ya kugombea urais. Kwanza alishatamka kwamba Kikwete ni mtani wake kwa hiyo dhahiri ilikuwa ni harakati za kutaniana tu!

JK mwenyewe aliishasema wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kukubali kuteuliwa na CCM 2005, pamoja na wote waliojitokeza alimshukuru mtani wake Shibuda pia. Sasa watani lazima wataniane ati.
 
Shibuda: Sigombei urais, Ikulu kuna suluba


MBUNGE wa Maswa, John Shibuda (CCM), ametangaza kuondoa kusudio lake la kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Shibuda alitangaza nia yake ya kugombea kwa mara ya mwaka Oktoba mwaka jana na kurejea azma yake hiyo tena Mei 13, mwaka huu.

Lakini jana akitangaza uamuzi wake huo aliouita kuwa ameahirisha kugombea nafasi hiyo na atagombea tena mwaka 2015, alisema amefikia hivyo baada ya kuona Rais Jakaya Kikwete amefanya mambo mengi mazuri ya maendeleo.

"Napenda kutamka nina furaha kubwa ya kuongozwa na Rais Kikwete kwa sababu apendaye kuongoza lazima awe tayari kuongozwa na hisia za umma", alisema

Baada ya kutangaza uamuzi wake huo, alisema Ikulu ni sehemu ya suluba za upweke hivyo sasa ana furaha ataendelea na uhuru wake wa uraiani kwa madai siku za kuhamia Ikulu zilimnyima raha.

Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari ya takribani dakika 20, sehemu kubwa Shibuda alimuelezea Rais Kikwete kuwa katika utawala wake ameheshimu Katiba na haki za binadamu dhidi ya viburi na ukandamaizaji na ameweza kujenga demokrasia na utawala bora.

Alipoulizwa uamuzi wake huo wa kujitoa kuwania nafasi ya urais umechangiwa na utabiri wa Shehe Yahya Hussein kuwa atakayejitokeza kumpinga Rais Kikwete atakufa, alisema "nadhihirisha kuwa utabiri wa mtabiri huyo ulikuwa kwa mzimuni na haumpati kwenye heri ya peponi kama mimi ndiyo maana sijafa hadi leo".

Hata hivyo, alisema kwa muda wote aliotangaza kugombea urais hajapata vitisho vyovyote wala kuoneshwa kinyongo na Rais Kikwete na mkewe Mama Salma pamoja na CCM.

Katika Uchaguzi Mkuu ujao, atawania tena nafasi ya ubunge ingawa hajaamua atagombea jimbo lipi baada ya Maswa kugawanywa na kuwa majimbo mawili.

Source: Gazeti la Habari leo
 
nani anapenda unafiki kama huu, hivi kuwadanganya watz kwa kuwapiga changa la macho hivi haoni kama ni kujipunguzia heshima zake?
Watu wa Maswa watajuana; nilifika Maswa zamani sana mwaka 1974 muda mfupi baada ya Wilaya ya Bariadi kutenganishwa; Bariadi palikuwa ni padogo sana ukilinganisha na Maswa. Miaka ya hivi karibuni nilipofika sehemu hizo nilishangaa kuwa Bariadi inaonekana imeenedela sana kuliko Maswa, utadhani kuwa Baridi ndiyo iliyozaa Maswa. Huenda ni kwa sababu ya usanii wa watu kama huyu huko Maswa.
 
Usije ukafikia wakati wa Kuchukua fomu akasema "Baada ya kutafakari kwa kina na kutathmini mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne nimeona nimuunge mkono Mh Rais katika ngwe ya Pili". Yangu masikio and mark my word, Nina wasi wasi na dhamira halisi ya Shibuda

Hakika Unabii Umetimizwa na Shibuda
 
Back
Top Bottom