Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

..................juzi waziri mkuu wa zamani edward lowasa aliiambia serikali na ccm kuwa wanapaswa kuchukua maamuzi magumu japo yatakuwa na maumivu makali dhidi yao................mimi naomba uongozi wa chadema uchukue maamuzi magumu kumtimua shibuda katika chama,kwa kuonyesha dharau dhidi ya chama na kuwa kibaraka wa ccm ndani ya cdm. Hata kama maamuzi hayo yawe na madhara kwa chama chetu kwa kiasi gani..........nawasilisha!!!


true bora tupoteze hilo jimbo kuliko kuendelea kuwa na mtu kama shibuda
 
naomba ushauli juu ya suala la shibuda, sababu jumanne tutakuwa na kikao cha kamati tendaji ya jimbo la maswa magharibi ni kikao cha dharura hata agenda hatujaambiwa ikitokea kuna agenda ya kujadil sakata la shibuda naomba ushauli, kwa maana nalo ni suala zito na gumu la kimaamuzi.
 
Dr. yupo online, bahati mbaya ameshindwa kulijibu hilo.
 
Sio shubuda peke yake bali na madiwani wa Arusha nao inabidi maamuzi magumu yachukuliwe.
 
Hata wakati zitto anaandamwa na mbowe na wajinga fulani humo, tuliambiwa huwa haitwi kwenye vikao halali vya watendaji wa chama, badala yake wanakaa slaa na watu wake vipenzi.
Hata sasa shibuda hakuitwa kisa mbowe anaogopa shibuda akipewa nafasi ya kuonekana kwa watanzania, atamfunika na kugombea urais ambao mbowe anataka amuondoe dr slaa.
Ila mbowe ushauri wa bure huwezi kuwa rais wa nchi hii.
 
Naunga mkono hoja asilimia mia hatuwez kuendelea kuwa na kibalaka wa wazwaz ndan ya chama, maamuz magumu muhimu.
 
Chama makini hutumia rasilimali zake za ndani kurekebisha mara mambo yanapokwenda mrama, hivi huyo Shibuda mmoja tu mnataka kumfukuza??? wakiwa kumi kama yeye mtafukuza wangapi? anapaswa awekwe sawa? kama ndani ya chama mnapata tabu hiyo!! mkichukua nchi si mtafukuza watu wote watakao kua na hsisa tofauti, nadhani mtafukuza mpaka itafikia time mtaenda burundi kuchkua watu waje kufanya kazi za wazawa. tuache uvivu wa kufikiri, ongeeni nae
 
CHADEMA: hivi mnafahamu kua nguvu ni matumizi ya mwisho kabisa ya akili???? sasa mtafukuza wangapi? mtu akitofautiana na nyie mawazo basi hafai???? hichi ni chama cha siasa au " International criminal gang of Bust.......ds". umwamba haufai bana. shibuda apewe muda na arekebishwe.
 
naomba ushauli juu ya suala la shibuda, sababu jumanne tutakuwa na kikao cha kamati tendaji ya jimbo la maswa magharibi ni kikao cha dharura hata agenda hatujaambiwa ikitokea kuna agenda ya kujadil sakata la shibuda naomba ushauli, kwa maana nalo ni suala zito na gumu la kimaamuzi.

mwambie awape kadi yetu ya cdm aende zake. Pia mwambie aache kuota sharubu!
 
Yes, na mimi naunga hoja hii kwa 100 pc.

Kwa kweli siyo siri tena kuwa Shibuda ni agent wa Chama Cha Magamba=CCM na ametumwa kuja kuivuruga CHADEMA.
Huyu jamaa anaonekana hafai na ni wakuogopwa kama ukoma. Simwelewi hata kidogo anaposema anaishangaa Demokrasia ya CDM!!! Inaonekana hajui hata maana ya demokrasia! Hili sukuma hovyo kabisa!!
Kuna uhuru wa kutoa maoni/mawazo nje au ndani ya chama kuhusiana na issues ambazo ni too general lakini siyo kwa case sensitive kama hii ya Posho za Wabunge ambayo ni UFISADI wa moja kwa moja.

Shibuda kupingana na sera ya CHAMA ambayo imo kwenye ILANI ya Uchaguzi ni UHAINI perce. Sijui huyu jamaa wakti wa Kampeni mwaka jana alikuwa anaeleza nini kwa wapiga kura wake kama kwa sasa anaonekana KUPINGA SERA ZA CHAMA WAZIWAZI!

Shibuda habebeki hata kwa mbeleko lazima atimuliwe akachunge ng'ombe usukumani.
Uongozi wa Chama kitaifa fanyeni kweli ili kuondoa vibaraka wanaotumwa kuja kuvuruga chama chetu ambacho kinaendelea kukua na kuimarika siku hadi siku. Lazima Shibuda atimuliwe atuachie chama chetu. Hana adabu!
 
Shibuda ameshika mpini, CDM hawawezi kumfukuza uanachama sasa hivi kwani matokeo yake ni kupoteza viti maalum. Unless wawe wana uhakika wa kyshinda uchaguzi mdogo.
 
Nimefuatilia harakati za chama cha cdm tangu 1992 chini ya uongozi wa Edwin mtei, nimeshindwa kushawishika kabisa kujiunga na chama hiki, kila mwanachama anapolalamikia uongozi wa chama shutuma anazotoa utasikia chama kina ukabila, ukaskazini leo tena ameibuka shibuda anasema viongozi hawana demokrasia bali wamejaa umimi na uyeye kila siku ni migogoro, kwanza chama kilipasuka wakatoka watu wakaenda kuunda SAU, kisha ikafuatiwa kuondoka KABOUROU akafuata Akwilombe wote hawa wanalalamikia ukabila, marehemu chacha naye alipita humo humo kwenye ukabila

Sijajua wewe ni chama na malengo yako ni yapi, na ninajadili hapa nikiwa freelance bila chama, lakini, hoja yako ingekuwa na mashiko ungetuleleza chama kingine cha upinzani unachokilinganisha na CHADEMA kwa mafanikio. Na kama hakuna, tuambie ni kwa nini. Kwa analysis yangu ya haraka haraka tu, ni kuwa CHADEMA ni chama pekee Tanzania ambacho trend yake yamafanikio inapanda regime hadi regime, tofauti kabisa na chama kingine chochote. Hii ni kwa sababu ya mbinu zao za kiongozi ikiwemo kutambua mamluki tofauti na vyama vingine vingi. Hilo unalotaka kutuaminisha, ni propaganda ambazo tumezizoea kila kukicha. Labda tu nikuambie kitu kimoja, kuwa, hakuna kitu kigumu kama kuendesha chama cha upinzani Tanzania, pengine hata Africa. Hii ni kwa kuwa, kwanza chama ambacho kinakuwa kiko madarakani, kinakuwa hakipendi hata kidogo kuona ustawi wa chama ambacho kitatishia mustakabali wake hapo baadaye. Kwa hiyo kitatumia kila kitu ikiwemo kuweka mamluki, media, sheria, polisi, mahakama na kila kitu ili tu kuonyesha uovu uliopo kwenye chama cha upinzani. Ndio maana hata wanavyofanyiwa wabunge wa upinzani hasa CHADEMA ni tofauti kabisa na wanakuwa treated wabunge wa CCM. Hebu tulia kidogo ufikirie enzi zile za chama cha NCCR mageuzi (mkumbuke Masumbuko Lamwai-alifutiwa mpaka uwakili), ikaja UDP, pale Cheo alipokuja kufukuza wabunge wake wote na kubaki yeye na Teddy Kaselabantu. Fikiria pia CUF ilivyokuwa ikifanyiwa propaganda, mara kufananishwa na ugaidi, udini na fujo, unashangaa yule yule aliyekuwa katibu mwenezi wa CUF leo ndio yuko propaganda CCM, lakini pia utaona kuwa Zanzibar wameingia mseto. Sasa kama hawa watu walikuwa wabaya kiasi hicho, wanakubalianaje kuwa nao leo kwenye serikali. Pia wale wote unaosema walitendewa vibaya CHADEMA leo wako CCM akiwemo Kaborou, Akwilombe, Shitambala nk. Nilitegemea basi kama wao walikuwa wapiganaji wa kweli wangeanzisha chama chao au basi kuhamia chama kingine wanachoona kizuri cha upinzani wakahamia halafu tuone maendeleo. ? Haya fikiria TLP, CCJ kote fitina nk.Mwangalie Mrema? wapi amefanikiwa?

Mwisho nakutakia kila la heri katika kazi yako
 
Hakuna haja ya maamuzi magumu, yule nguvu ya umma itamchomoa!
 
Shibuda ni Picha hailisi ya CCM. Mawazo mabovu ya shibuda na Roho ya Upumbavu vimemjaa hata hawezi tena kufikiri. Tunachotaka HERI KUKATAA POSHO HATA KAMA NI KWA UNAFIKI. SISI HATUHITAJI UTAKATIFU WA WA CHAMA BALI KUIONDOA CCM. CHAMA CHOCHOTE CHA UPINZANI KISHIKE NCHI HATA KAMA NI KIPINDI KIMOJA KINATOSHA. CHADEMA KUWENI MAKINI NA VIBARAKA WA CCM: WAKINYIMWA KURA ZA MAONI MJUE HAO KWELI NI TAKATAKA WANANUUKA. SHIBUDA ANATAKIWA KUOGOPWA KAMA GONJWA LA UKIMWI.
 
*Avaa viatu vya marehemu Chacha
*Asema CHADEMA inanuka ubinafsi
*Ajipanga kueleza maovu ya Mbowe, Zitto
*Asema hatishiki, yupo tayari kufukuzwa.

*Awashutumu Mbowe Zitto wameigeuza Chadema kampuni
*Ajiandaa kuzunguka nchi nzima kuueleza umma ukweli
*Mbowe ajibu, asema hapendi malumbano, wakati utafika


HALI ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si shwari, baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao.

Alisema kutokana na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.

Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mjini Dodoma jana, Shibuda alibeza shutuma hizo zilizoelekezwa kwake na kuwataka viongozi wa juu wa chama hicho kumwomba radhi kutokana na kumchafua.

Shibuda aliwataja viongozi hao ambao alidai wanamchafua kupitia vyombo vya habari kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto.

Hata hivyo Shibuda alisema mbali ya kuombwa radhi, pia atalazimika kuandaa mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwaeleza wananchi tabia za viongozi hao.

"Natarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli za kibunge, nitakaporudi, nitaitisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi juu ya Zitto na Mbowe, ambao tayari wameshanishutumu kupitia vyombo vya habari.

"Mikutano hiyo nitaianzia jimboni kwangu mwishoni mwa mwezi huu, nitaweka wazi kila kitu kwa sababu wananchi ndio wenye chama na wana haki ya kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo.

"Hata hivyo, kabla mimi sijaenda kwa wananchi nawaruhusu wao waende kwa wananchi wakanishitaki, wakaeleze ubaya wangu ili mimi nitakapowaeleza wananchi basi wao ndio wapime wenyewe.

"Mimi nayajua mengi sana ya CHADEMA, kwa muda mfupi niliokaa katika chama hicho nimejionea mengi sana na nalazimika kusema kuwa alichokuwa akikisema Chacha Wangwe (marehemu) ni sawa kabisa na hakukosea kitu.

"Nakwambia sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu sana.

"Mbowe anaendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki, mimi siwezi kunyamaza, siwezi kufumbia ukweli katika jambo ambalo naamini ni sahihi. Niliyosema nimeyasema na kama hayakuwafurahisha sitawaomba radhi na sina tabia ya kuomba radhi, kwani hata nilipokuwa CCM sikuwahi kuomba radhi.

"Lakini kwa kuwa wao ndio wamenikosea kwa kunichafua kupitia vyombo vya habari, basi nawataka waniombe radhi kwa waliyonizushia na pia nawataka wawaombe radhi Watanzania kwa kutowaambia ukweli," alisema Shibuda.

Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za Mahon, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.

"Hili suala la posho ambalo ndilo chanzo cha haya, nakwambia siyo msimamo wa chama kama wanavyowaambia Watanzania, huo ni uamuzi wao wawili tu kwa sababu katika vikao walikuwa wanawatisha wabunge na kuwatishia kwamba watawafukuza kama hawatakubali kukataa posho.

"Huwezi kuendesha chama kwa nguvu kwa sababu hizo posho ndicho kipozeo cha mbunge, kwani kama ng'ombe anayekamuliwa akikosa malisho ukimkamua ujue atatoa damu.

"Sasa kama ndivyo hivyo, wabunge wasipolipwa posho kazi zao watafanyaje, katika hili siwezi kunyamaza, nitaendelea kuheshimu uongozi kwa ajili ya kujenga ufanisi wa maslahi ya chama ya kutajirisha masikini dhidi ya vatu, cheo ni dhamana.

"Sitoona haya kukosoa tabia ya umimi na uyeye kwa mtu yeyote, sitahama CHADEMA kwa sababu sikutofautiana na chama bali nimetofautiana na watu wachache kutokana na kutoridhishwa na uongozi wao," alisema.

Akimchambua Zitto, alisema anajifanya mzalendo machoni pa watu wakati tabia na matendo yake ni tofauti na anavyowaambia Watanzania.

"Zitto siyo mzalendo, namtaka aache tabia ya ukuwadi na kuunda uzandiki wa kufunika uwazi na ukweli kwa dhamira ya ubinafsi wa kujikweza kisirisiri ili apendwe na uongozi na kuidanganya jamii kwamba yeye ni mwadilifu.

"Zitto asigandamize haki za watu, wanaojua stahili zao kwa sababu yeye anajipamba ili asihitilafiane na kiongozi wake kwa masilahi yake binafsi, aache tabia ya kujifanya mzalendo wakati ni mnafiki anayetaka kujenga matarajio yake binafsi huku akificha ajenda ya siri ya umimi na uyeye.

"Ili kutambua tabia yake na mwenzake huyo ni sawa na mwenye kiatu ambaye ndiye anayejua jinsi kinavyomuumiza badala ya mtazamaji ambaye anafurahishwa na rangi ya kiatu, aache kabisa tabia hiyo awe wazi na asitafute umaarufu," alisema.

Alisema kinachomgombanisha na wenzake ndani ya chama hicho ni tabia yake ya kupenda uwazi, wakati baadhi ya wenzake wanataka ukweli usielezwe kwa wananchi.

"Chuki iliyopo ni kwamba mimi Shibuda napinga chama kuwa kama kampuni ya kuingiza wanachama wa kutekeleza masilahi binafsi ili kudumisha ukabila, uyeye, umimi, uwao, umajimbo ambao umefichwa na msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata.

"Binafsi sitarudi nyuma, naahidi kulinda maslahi na kutetea shabaha ya CHADEMA kwa maslahi ya wananchi, nitaendelea kupingana na tabia ya kuwaonea watu kwa sababu wabunge maskini kama mimi tunapata fedha za kuwahudumia wananchi kwa kudunduliza fedha za mishahara na posho.

"Wabunge matajiri wao wana mapokeo ya hisa kutoka katika biashara zao binafsi, kwa hiyo ndondondo za mapato kutoka bungeni hawazihitaji, ndiyo maana wanawalazimisha wenzao wasiokuwa na kitu wafuate nyayo zao hata kama wanawaumiza," alisema.

Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema atahutubia mikutano ya hadhara wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu baada ya kurejea nchini, ili kuweka wazi tabia za badhi ya viongozi wa chama hicho.

Juni 28 mwaka huu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Sh 150,000 hadi Sh 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi.

Akijibu shutuma hizo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, alisema hapendi malumbano kupitia biombo vya habari.

"Kamanda sipendi malumbano kwenye vyombo vya habari, tusubiri muda ukifika ukweli utajulikana tu," alisema Mbowe
 
Kosa lilifanyika kumchukua huyu mropokaji, tangu akiwa CCM alikuwa akijulikana kwa uzezeta wake sijui kwa nini CDM hawakulifikiria hili. CDM waendenaye taratibu, wamweke pembeni. Anazungumzia ya marehemu Chacha Wangwe, kweli kwa hulka na uwezo wa kiakili wanafanana....magarasha tu!
 
Kosa lilifanyika kumchukua huyu mropokaji, tangu akiwa CCM alikuwa akijulikana kwa uzezeta wake sijui kwa nini CDM hawakulifikiria hili. CDM waendenaye taratibu, wamweke pembeni. Anazungumzia ya marehemu Chacha Wangwe, kweli kwa hulka na uwezo wa kiakili wanafanana....magarasha tu!

chacha ni kichwa mkuu, huwezi kumlinganisha na huyu kiazi hata mara moja, chacha alikuwa na kasoro zake lakini sio km za shibuda.
 
Huyu lengo lake anataka kukivuruga chama ili kionekane hakina maana na wananchi wapoteze imani na upinzani kwa ujumla,sema lililo jema tu ni kwamba viongozi wote wako pamoja dhidi yake.
 
sasa atakuwa anahitaji nini, maana alishatwambia ubaya wa 'magamba' na sasa anakiponda chama ambacho kimemfavour kumuingiza bungeni! Kweli Perfection doesn't exist na hapa cdm wakubali kosa kuteam up na huyu jamaa. ...basi ahamie TLP!!!
Kosa lilifanyika kumchukua huyu mropokaji, tangu akiwa CCM alikuwa akijulikana kwa uzezeta wake sijui kwa nini CDM hawakulifikiria hili. CDM waendenaye taratibu, wamweke pembeni. Anazungumzia ya marehemu Chacha Wangwe, kweli kwa hulka na uwezo wa kiakili wanafanana....magarasha tu!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom