WEMBE WENGE
Senior Member
- Mar 6, 2011
- 132
- 45
CHADEMA lazima muwe makini na uwezo wa kujuwa kwamba hii stori imetengenezwa na magazeti kutimiza matakwa ya ccm. Kwanza angalia magazeti (Jambo Leo, Uhuru) yenyewe yaliyoandika yanamilikiwa na nani. Je ni kweli kasema wapinzani hawawezi kuchukuwa nchi au kura za wanachama wa CHADEMA hazitoshi? BAVICHA wanapiga kelele kutokana na walichosoma katika magazeti na sio alichosema Shibuda. Kilichotekea ni taasisi ya utawala bora "Good Governance …" ilialikwa kwenda kutoa ripoti ya tathmini yake kwenye hicho kikao na hii taasisi inaalikwa sehemu nyingi, shibuda ni mmoja ya watu waliopo ndani ya hiyo taasisi. Baada ya maongezi rasmi kulikuwa na utani kati ya kikwete na shibuda. Katika huo utani shibuda alisema atagombea urais kwa tiketi ya mgombea binafsi na sio kwa tiketi ya CHADEMA na akamuomba kikwete amuunge mkono. Lakini magazeti kwasababu ya malengo yao binafsi au ya CCM yaliamua kupindisha kauli hii na kusema Shibuda kaamua kugombea kupitia CHADEMA, na watu hao hao ndio walioleta stori hiyo jamii forum. Baada ya Zito kutangaza kugombea uraisi na kupingwa na Mtei inaonekana CCM wameshagundua udhaifu wa CHADEMA; hawataki mgombea atoke sehemu nyingine isipokuwa kaskazini, kwahiyo kutakuwa na juhudi za kulipigia mstari swala hili mpaka nchi yote ielewe kwamba kama wewe sio mchaga au hutoki kaskazini basi uraisi huruhusiwi kugombea kupitia CHADEMA. Kwahiyo kabla haujaanza ushabiki usiokuwa na umakini kwa kupinga mtu tu kwasababu kasema atagombea uraisi, lazima uwe makini kujuwa labda unawafaidisha CCM. Huyo Shibuda anaelewa CHADEMA hawawezi kupitisha jina lake kugombea uraisi labda awe mgombea binafsi kama alivyomwambia kikwete. Kwahiyo hiyo kauli yakusema atagombea kupitia CHADEMA imetengenezwa KUGOMBANISHA WACHAGA NA WASUKUMA KAMA SIO WATANZANIA WOTE. Kwahiyo kuweni makini, wanaosoma hapa sio tu wachaga bali na kabila nyingine. Hata ukitoa comment unajiita WAMBURA au MASANJA bado tu watu watajuwa ni mchaga kwasababu ya unavyokuwa MWEPESI NA HARAKA ya kupinga watu wa kabila nyingine. Msije mkafanya CHADEMA ionekane haina Demokrasia.
Hivi ni virus vya kisiasa,
makala nzuri yenye ufafanuzi mzuri inapoingizwa kejeli za ukabila inatia shaka na maandiko ya mwandishi kama kweli lengo lake ni keulewesha wale wasiolewa ama kueneza hoja zake mgando. Nafasi ya mgombea uaraisi ni Moja, mwenzetu na kundi lako lililojikita kwenye ukabila unataka awe nani, kinyume na yule aliyegombea na wenzake wengi na kuibuka mshindi? mimi si mchaga na wala sitoki kaskazini kama ulivyojaribu kujieleza hapa, lakini uliyoyaongea yanaongelewa sana na wanamagamba katika harakati zao za kipropaganda walizojifunza pale magogoni, Isaraeli na urusi. Ni nani asiye wa kaskazini aliyeomba kugombea uraisi akashindwa kupewa nafasi kwa sababu tu yeye sio wa kaskazini ama Mchaga?
CDM ni chama cha watanzania na wanachama wake tunajua kuwa yeyote aliye mwanachama ana haki kamili ya kugombea nafasi yoyote katika chama na anao uwezo wa kushinda kama wanachama wenzake watamuona anaweza kuwaongoza. epuka hizo siasa za propaganda za kisoshalist hazikusaidii kabisa.