CHADEMA lazima muwe
makini na uwezo wa kujuwa kwamba hii stori imetengenezwa na magazeti
kutimiza matakwa ya ccm. Kwanza angalia magazeti (Jambo Leo, Uhuru)
yenyewe yaliyoandika yanamilikiwa na nani. Je ni kweli kasema wapinzani
hawawezi kuchukuwa nchi au kura za wanachama wa CHADEMA hazitoshi?
BAVICHA wanapiga kelele kutokana na walichosoma katika magazeti na sio
alichosema Shibuda. Kilichotekea ni taasisi ya utawala bora Good
Governance
ilialikwa kwenda kutoa ripoti ya tathmini yake kwenye
hicho kikao na hii taasisi inaalikwa sehemu nyingi, shibuda ni mmoja ya
watu waliopo ndani ya hiyo taasisi. Baada ya maongezi rasmi kulikuwa na
utani kati ya kikwete na shibuda. Katika huo utani shibuda alisema
atagombea urais kwa tiketi ya mgombea binafsi na sio kwa tiketi ya
CHADEMA na akamuomba kikwete amuunge mkono. Lakini magazeti kwasababu ya
malengo yao binafsi au ya CCM yaliamua kupindisha kauli hii na kusema
Shibuda kaamua kugombea kupitia CHADEMA, na watu hao hao ndio walioleta
stori hiyo jamii forum. Baada ya Zito kutangaza kugombea uraisi na
kupingwa na Mtei inaonekana CCM wameshagundua udhaifu wa CHADEMA;
hawataki mgombea atoke sehemu nyingine isipokuwa kaskazini, kwahiyo
kutakuwa na juhudi za kulipigia mstari swala hili mpaka nchi yote ielewe
kwamba kama wewe sio mchaga au hutoki kaskazini basi uraisi huruhusiwi
kugombea kupitia CHADEMA. Kwahiyo kabla haujaanza ushabiki usiokuwa na
umakini kwa kupinga mtu tu kwasababu kasema atagombea uraisi, lazima uwe
makini kujuwa labda unawafaidisha CCM. Huyo Shibuda anaelewa CHADEMA
hawawezi kupitisha jina lake kugombea uraisi labda awe mgombea binafsi
kama alivyomwambia kikwete. Kwahiyo hiyo kauli yakusema atagombea
kupitia CHADEMA imetengenezwa KUGOMBANISHA WACHAGA NA WASUKUMA KAMA SIO
WATANZANIA WOTE. Kwahiyo kuweni makini, wanaosoma hapa sio tu wachaga
bali na kabila nyingine. Hata ukitoa comment unajiita WAMBURA au MASANJA
bado tu watu watajuwa ni mchaga kwasababu ya unavyokuwa MWEPESI NA
HARAKA ya kupinga watu wa kabila nyingine. Msije mkafanya CHADEMA
ionekane haina Demokrasia.