Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Kwani posho inaweza kuwa sera? wewe umesoma wapi shule?

Posho ni sera ya CHADEMA?! Watakuwa wameishiwa sera kwa kweli. Ukumbuke suala la Posho lilikuwa la Zitto mwenyewe kabla hajaliuza kwa taabu kwa chama chake.
 
Posho ni sera ya CHADEMA?! Watakuwa wameishiwa sera kwa kweli. Ukumbuke suala la Posho lilikuwa la Zitto mwenyewe kabla hajaliuza kwa taabu kwa chama chake.
Hv unaelewa maana ya sera?? chochote kitakachozungumzwa katika ilani ya uchaguzi wa chaa ni sera na hili la posho lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya cdm hata mnyika alisema bungeni serikali ndio imeiba sera hiyo kwao kwa sababu ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya cdm.
 
zitto anajipendekeza kwa mbowe baada ya kuona siraha za mbowe kwenye magazeti eg mjinga/mnafiki kubenea na wengine wanampiga mikuki ya kweli, na ndiyo maana anaamua kunyoosha mikono.
muone huyu muongo mbowe mnafiki mkubwa anawatesa wabunge wadogo masikini yeye akiwa atajiri jizi na fisadi wewe mbowe hutakiwi, na siku watu wakikuchoka kwa kuwaandama watu hodari utajuta, landa uwaue kama chacha wangwe.
huyu zitto ni kigeugeu alikuwa akimuandama wangwe sana kabla hajapewa za uso na mbowe,akamtumia kafulila kuwaandika wanaharakati wa kweli wa cdm ili apate kura, watu wa aina hizi ni uchafu kabisa
 
Huyu lengo lake anataka kukivuruga chama ili kionekane hakina maana na wananchi wapoteze imani na upinzani kwa ujumla,sema lililo jema tu ni kwamba viongozi wote wako pamoja dhidi yake.

this was his motive we need to be veeery and extra careful
 
Hv unaelewa maana ya sera?? chochote kitakachozungumzwa katika ilani ya uchaguzi wa chaa ni sera na hili la posho lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya cdm hata mnyika alisema bungeni serikali ndio imeiba sera hiyo kwao kwa sababu ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya cdm.
Dah! Ngoja niisome tena ilani yao. Hata hivyo, sidhani kama kila kilichomo ndani ya ilani ni sera. Ilani inabeba vitu vingi zikiwemo ahadi na jinsi ya kuzitekeleza kwa muda maalum tu. Zipo sera za Elimu, Uchumi, uwekezaji,....., posho haiwezi kuwa sera.
 
Mie kwa upande wangu nilimshangaa sana huyu bwana wakati akichangia. Sasa asianze kuleta habari ambazo hazipo na kuanza kuzushia watu. Kwa maoni yake yeye mbunge anapaswa apate kipoozeo hata kama posho hizo sio halali? Wabunge wa aina hii ni hatari kabisa kwenye nchi yetu. Yeye anadhani ubunge ni ajira yake!

Lakini kwa upande mwingine naona ni vizuri kwa chama kufikia kwenye hali kama hii. Katika mazingira kama haya ndo tutaona ukomavu wa chama kwenye kushughulikia mitafaruku kama hii. Ukomavu wa viongozi na oganaizeshen nzima utaonekana pale chama kinapokuwa kwenye wakati mgumu.

Huyu bwana baada ya kuona amekosea anaanza kutishia watu kwenye vyombo vya habari. Kikubwa ni hatua zichukuliwe kwa kufuata utaratibu wa chama. Kama ni kufukuzwa na afukuzwe tu. Ninaamin kuwa CDM watalifanya hili kwa uangalifu mkubwa sana.
 
*Avaa viatu vya marehemu Chacha
*Asema CHADEMA inanuka ubinafsi
*Ajipanga kueleza maovu ya Mbowe, Zitto
*Asema hatishiki, yupo tayari kufukuzwa.

*Awashutumu Mbowe Zitto wameigeuza Chadema kampuni
*Ajiandaa kuzunguka nchi nzima kuueleza umma ukweli
*Mbowe ajibu, asema hapendi malumbano, wakati utafika


HALI ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si shwari, baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, kuwatolea uvivu viongozi wa juu wa chama hicho, akisema hatishiki na vitisho vinavyofanywa na viongozi hao.

Alisema kutokana na hali hiyo, yuko tayari kufukuzwa katika chama kwa kosa la kusema ukweli siku zote.

Hivi karibuni, Shibuda amedaiwa kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake, kuhusiana na suala la posho za wabunge, kitendo ambacho kimemfanya aonekane muasi ndani ya chama na hivyo kuundiwa tume ya kumchunguza.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mjini Dodoma jana, Shibuda alibeza shutuma hizo zilizoelekezwa kwake na kuwataka viongozi wa juu wa chama hicho kumwomba radhi kutokana na kumchafua.

Shibuda aliwataja viongozi hao ambao alidai wanamchafua kupitia vyombo vya habari kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto.

Hata hivyo Shibuda alisema mbali ya kuombwa radhi, pia atalazimika kuandaa mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwaeleza wananchi tabia za viongozi hao.

“Natarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli za kibunge, nitakaporudi, nitaitisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi juu ya Zitto na Mbowe, ambao tayari wameshanishutumu kupitia vyombo vya habari.

“Mikutano hiyo nitaianzia jimboni kwangu mwishoni mwa mwezi huu, nitaweka wazi kila kitu kwa sababu wananchi ndio wenye chama na wana haki ya kujua nani anasema ukweli na nani anasema uongo.

“Hata hivyo, kabla mimi sijaenda kwa wananchi nawaruhusu wao waende kwa wananchi wakanishitaki, wakaeleze ubaya wangu ili mimi nitakapowaeleza wananchi basi wao ndio wapime wenyewe.

“Mimi nayajua mengi sana ya CHADEMA, kwa muda mfupi niliokaa katika chama hicho nimejionea mengi sana na nalazimika kusema kuwa alichokuwa akikisema Chacha Wangwe (marehemu) ni sawa kabisa na hakukosea kitu.

“Nakwambia sura ya CHADEMA ukiwa nje ya chama ni tofauti na sura ya CHADEMA ya ndani, ni tofauti kabisa kwa sababu yanayofanyika humo ni mambo ya ajabu sana.

“Mbowe anaendesha chama kibabe na anaungwa mkono na Zitto ambaye anaonekana kuwa na tabia ya ukuwadi na unafiki, mimi siwezi kunyamaza, siwezi kufumbia ukweli katika jambo ambalo naamini ni sahihi. Niliyosema nimeyasema na kama hayakuwafurahisha sitawaomba radhi na sina tabia ya kuomba radhi, kwani hata nilipokuwa CCM sikuwahi kuomba radhi.

“Lakini kwa kuwa wao ndio wamenikosea kwa kunichafua kupitia vyombo vya habari, basi nawataka waniombe radhi kwa waliyonizushia na pia nawataka wawaombe radhi Watanzania kwa kutowaambia ukweli,” alisema Shibuda.

Katika maelezo yake, Shibuda, ambaye alihamia CHADEMA mwaka jana akitokea CCM, baada ya kushindwa katika kura za Mahon, alisema pamoja na kwamba Mbowe na Zitto wanaamini wako sahihi, ukweli utabaki pale pale kwamba wanasiasa hao wanahatarisha demokrasia katika chama hicho.

“Hili suala la posho ambalo ndilo chanzo cha haya, nakwambia siyo msimamo wa chama kama wanavyowaambia Watanzania, huo ni uamuzi wao wawili tu kwa sababu katika vikao walikuwa wanawatisha wabunge na kuwatishia kwamba watawafukuza kama hawatakubali kukataa posho.

“Huwezi kuendesha chama kwa nguvu kwa sababu hizo posho ndicho kipozeo cha mbunge, kwani kama ng’ombe anayekamuliwa akikosa malisho ukimkamua ujue atatoa damu.

“Sasa kama ndivyo hivyo, wabunge wasipolipwa posho kazi zao watafanyaje, katika hili siwezi kunyamaza, nitaendelea kuheshimu uongozi kwa ajili ya kujenga ufanisi wa maslahi ya chama ya kutajirisha masikini dhidi ya vatu, cheo ni dhamana.

“Sitoona haya kukosoa tabia ya umimi na uyeye kwa mtu yeyote, sitahama CHADEMA kwa sababu sikutofautiana na chama bali nimetofautiana na watu wachache kutokana na kutoridhishwa na uongozi wao,” alisema.

Akimchambua Zitto, alisema anajifanya mzalendo machoni pa watu wakati tabia na matendo yake ni tofauti na anavyowaambia Watanzania.

“Zitto siyo mzalendo, namtaka aache tabia ya ukuwadi na kuunda uzandiki wa kufunika uwazi na ukweli kwa dhamira ya ubinafsi wa kujikweza kisirisiri ili apendwe na uongozi na kuidanganya jamii kwamba yeye ni mwadilifu.

“Zitto asigandamize haki za watu, wanaojua stahili zao kwa sababu yeye anajipamba ili asihitilafiane na kiongozi wake kwa masilahi yake binafsi, aache tabia ya kujifanya mzalendo wakati ni mnafiki anayetaka kujenga matarajio yake binafsi huku akificha ajenda ya siri ya umimi na uyeye.

“Ili kutambua tabia yake na mwenzake huyo ni sawa na mwenye kiatu ambaye ndiye anayejua jinsi kinavyomuumiza badala ya mtazamaji ambaye anafurahishwa na rangi ya kiatu, aache kabisa tabia hiyo awe wazi na asitafute umaarufu,” alisema.

Alisema kinachomgombanisha na wenzake ndani ya chama hicho ni tabia yake ya kupenda uwazi, wakati baadhi ya wenzake wanataka ukweli usielezwe kwa wananchi.

“Chuki iliyopo ni kwamba mimi Shibuda napinga chama kuwa kama kampuni ya kuingiza wanachama wa kutekeleza masilahi binafsi ili kudumisha ukabila, uyeye, umimi, uwao, umajimbo ambao umefichwa na msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata.

“Binafsi sitarudi nyuma, naahidi kulinda maslahi na kutetea shabaha ya CHADEMA kwa maslahi ya wananchi, nitaendelea kupingana na tabia ya kuwaonea watu kwa sababu wabunge maskini kama mimi tunapata fedha za kuwahudumia wananchi kwa kudunduliza fedha za mishahara na posho.

“Wabunge matajiri wao wana mapokeo ya hisa kutoka katika biashara zao binafsi, kwa hiyo ndondondo za mapato kutoka bungeni hawazihitaji, ndiyo maana wanawalazimisha wenzao wasiokuwa na kitu wafuate nyayo zao hata kama wanawaumiza,” alisema.


Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema atahutubia mikutano ya hadhara wakati wowote mwishoni mwa mwezi huu baada ya kurejea nchini, ili kuweka wazi tabia za badhi ya viongozi wa chama hicho.

Juni 28 mwaka huu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka wa fedha 2011/2012, Shibuda aliitaka serikali iongeze posho za wabunge kutoka Sh 150,000 hadi Sh 500,000 kwa siku, kwa kuwa kiwango cha sasa hakitoshi.

Akijibu shutuma hizo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, alisema hapendi malumbano kupitia biombo vya habari.

“Kamanda sipendi malumbano kwenye vyombo vya habari, tusubiri muda ukifika ukweli utajulikana tu,” alisema Mbowe
Wabunge waliopo bungeni kwa masilahi ya binafsi wanaonekana kwa matamshi na matendo yao .Baada ya kutemwa CCM na kwenda CHADEMA imedhihilisha ya wazi kwa mtu huyu kwake muhimu ni posho na marupurupu ya ubunge si kinginecho.USHAURI WANGU KWAKO SHIBUNDA,CCM WABAYA HAWAKUKUPA KULA CHADEMA WABAYA WANATAKA KUKUZUIA KULA!​"UNDA CHAMA CHAKO"!
 
MAMBO yanazidi kuwa magumu kwa mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda kufuatia Kambi ya Upinzani Bungeni kuanza rasmi mchakato wa kuchukulia hatua mbunge huyo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kuisaliti kambi hiyo.Shibuda ambaye alijiunga na Chadema akitokea CCM wakati wa harakati za uchaguzi mkuu uliopita, leo atakabidhiwa barua rasmi inayomtaka ajieleze kwanini aliwasaliti wakati akichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni, kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Tuhuma zinazomkabili Shibuda ni kutoa matamshi yanayopinga na msimamo wa kambi yake inayoongozwa na Chadema pale alipowapiga vijembe wabunge wanaopinga posho zinazotolewa kwa wabunge na watumishi wengine wa umma nchini.

Akizungumza na Mwananchi, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kitendo Shibuda kupingana msimamo wa kambi ya upinzani ambao ni kukataa kulipwa posho za vikao, kimewadhalilisha na kwamba lazima muhusika (Shibuda) atoe maelezo kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yake.

"Kutokana na tukio la kudhalilisha uamuzi ya vikao vya kambi, kuna aina mbili za kumchukulia hatua Shibuda, kwanza ni kwa upande wa kambi ya upinzani na pili kumshitaki Chadema,”alisema Lissu na kuongeza:

“Mbunge anapokiuka uamuzi ya kambi anastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kupewa adhabu, na adhabu kubwa anayoweza kupewa na kambi hii kwa kanuni zetu ni kumtenga katika kambi na kumtangaza hadharani kuwa huyu ametengwa na kambi kwasababu amefanya makosa kadhaa".

"Mimi kama kiongozi wa nidhamu katika kambi hii kesho (leo) nitamuandikia barua ya kumtaka ajieleze ni kwanini amekaidi msimamo wa kambi katika suala la posho alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu, bungeni, ambalo sisi kama kambi ya upinzani tulikubaliana wote kukataa posho hizo,"alifafanua Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Shibuda mbali na kosa hilo, pia amekuwa akitoa matamshi ya kudhalilisha kambi ya upinzani na Chadema, pamoja na kuwadhalilisha viongozi wao.

Kushtakiwa Kamati Kuu
Lissu alisema baada ya kumuita Shibuda na kumuadhibu, kambi ya upinzani itawasilisha malalamiko katika vikao vikuu vya chama hicho, ili kuvipa ya nafasi ya kujadili suala hilo na kuchukua hatua.

"Katiba ya Chadema imeweka miongozo ya viongozi na wanachama na kwa yoyote atakayeivunja anastahili kuadhibiwa, sisi kama kambi ya upinzani bungeni, tutapeleka malalamiko yetu katika mkutano wa kamati kuu ya Chadema ili chama kione kama haya matamshi aliyoyatoa Shibuda hayakiuki hiyo miiko ya chama chetu,"alisema na kuongeza:

"Tukumbuke kwamba hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Shibuda kushtakiwa katika kamati hiyo, alishaadhibiwa kwa kutoshiriki kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia Bunge mjini Dodoma, ambapo yeye na wenzake ambao hawakushiriki walipewa onyo kali na kutakiwa kuwaomba radhi wabunge wenzao walioshiliki katika tukio hilo, wenzake walifanya hivyo, lakini Shibuda hadi leo hajawahi kuomba radhi".

"Tutaiomba Kamati Kuu suala hili lilishughulikie kwa umakini sana na waangalie matukio yake ya nyuma hili adhabu watakayotoa hiwe staiki na kubwa, na adhabu kubwa ya chama ni kufukuzwa tu,"alifafanua Lissu.

Lissu alisema madai kwamba Kiongozi wa Kambi hiyo, Freeman Mbowe na Naibu wake, Zitto Kabwe waliwalazimisha wabunge wa Chadema kukataa posho kwa kuwatisha kufukuzwa ubunge ikiwa watapingana, siyo ya kweli na kwamba ni ya kupikwa.

"Si kweli kwamba wabunge wa Chadema wametishwa, kufukuzwa iwapo hawataunga mkono kukataa posho, suala hili lilizua mjadala mrefu kwenye vikao vyetu na ilikuwa lazima iwe hivyo, lakini baadaye wote tulikubaliana kwasababu ulikuwa ni msimamo wa chama na tukasema ndio utakuwa msimamo wetu bungeni," alisema Lissu.

Alisema wanataka kuondoa utamaduni wa posho katika malipo ya utumishi wa umma nchini kwasababu unaangamiza uchumi wa taifa na kufanya watumishi wa umma kutowajibika ipasavyo kwani wanafanya kazi ya kukimbilia vikao kila mahala ili walipwe posho.

Kauli ya Zitto
Naye Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto alisema msimamo wa kumfukuza Shibuda upo pale pale kwani kambi hiyo wala Chadema hawawezi kumuacha mbunge anayekiuka sera na kuwadhalilisha viongozi hadharani.

"Shibuda hatafukuzwa kinyemela, lazima taratibu zifuatwe kwa Mnadhimu Mkuu wa kambi yetu kumuandikia barua ya kumueleza makosa yake na yeye kupata fursa yakujibu shutuma hizo, pili ataitwa katika Kamati Kuu ya chama chetu (Chadema) nao watatoa uamuzi wao,"alisema Zitto na kuongeza:

“ Chadema si chama cha kihuni kwamba tutakurupuka ni lazima haki itendeke na mimi sipendi mtu aonewe, Shibuda atapata haki zake zote kama mwananchama. Mbunge yeyote wa Chadema anapaswa kujua akienda kinyume na sera ya chama atafukuzwa”.

Alisema suala la posho lipo kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2010 kwahiyo ni sera, na kwamba anayepinga atafukuzwa tu na kwamba Chadema wataanza na Shibuda.

Zitto alisema "Shibuda anajua mie humtetea sana, lakini anapokwenda kinyume na sera ya chama tutamfukuza, aniite majina yoyote tu akienda kinyume na sera nitakuwa wa kwanza kumfukuza".

"Kuna masuala ya nidhamu kwenye bunge na wabunge wa chama fulani inaitwa’ three line whip, masuala ya msimamo wa kitendaji mfano tulipokaidi kwenda bungeni kutoka nje ya ukumbi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia bunge (walk out), haya ni ya kawaida na hayana adhabu kali, lakini likiwa la sera adhabu ni kufukuzwa, Shibuda asipapalike," alisema Zitto.

Wabunge Chadema wanena

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliwaomba wananchi wampuuze Shibuda kwa kauli zake kuwa wabunge wa Chadema wamelazimishwa na viongozi wao kukataa posho za vikao.

"Shibuda anataka umarufu mrahisi tu, Mbowe na Zitto hawezi kutuburuza wote 46 wa Chadema kwenye suala la posho, kwa kauli moja wabunge tulikubaliana swala hili na yeye hakuwepo kwenye vikao, nadhani ana tatizo".

Naye Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema hakuna hoja hata moja waliyowahii kulazimishwa na viongozi wa kambi ya upinzani bali wabunge wote hujadiliana jambo kwa pamoja kwa kushindana kwa hoja.

"Huyu mwenzetu Shibuda amekuwa akikiuka maagizo mengi ya vikao na kujitetea kuwa hakuwepo katika vikao, sisi hatuitani katika vikao kwa barua bwana, tunatumiana ujumbe mfupi wa maandishi wa simu au kumuomba Spika, Naibu Spika au Mwenyekiti wa Bunge yoyote kati yao anayeongoza bunge siku hiyo kututangazia bungeni," alisema.

Msimamo wa Shibuda
Wakati hayo yakiendelea, jana Shibuda amenukuliwa na gazeti moja litolewalo kila siku (siyo Mwananchi) akisema kwamba haogopi kufukuzwa katika Chadema na kwamba ataendelea kusimamia ukweli siku zote.

Shibuda alinukuliwa na gazeti hilo akiwataka viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Mbowe na Zitto kumwomba radhi kwa kile alichodai kwamba ni kumchafulia jina, huku akiahidi kwamba ataanika maovu ya viongozi hao.

Shibuda ni mwanasiasa ambaye alipokuwa CCM aliwahi kuzua mtafaruku ndani ya chama hicho na hata kuzuiwa kwake kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana kunatokana na kutofautina na waliokuwa viongozi wake wa chama mkoani na Taifani.
 
Imefika muda sasa Wasukuma kutoka kanda ya ziwa kuachana na CDM chama cha kikanda na kikabila, Shibuda ananyanyashwa kutoka na Usukuma wake angekuwa ametoka kaskazini wala usingesikia maneno yoyote ya kashfa! Shibuda nakushauri ili swala kawashitakie wazee wa Kisukuma kama ulivyomshitaki Wenje, kwa wazee wa Mwanza na wazee wakakuelewa kama Wenje ni Mkenya hawana tena shida nae amalize kipindi chake aende zake kwao Kenya, Wasukuma mnaona mnavyodharauliwa na CDM.Mbona kina Selasini wanaipongeza CCM kila siku ata siku moja hawajaguswa au kwa sababu ni Wachagga!.

Good comment,,,,,,, lakini ipeleke magambani great thinker haiendekezi ukabila unaouhubiri hapa
 
eti mkakati hafifu wa kuibomoa CDM ndiyo huu --- hata mimi nauweza. fukuza hii kitu, fanya uchaguzi mpya na nina uhakika atakayesimama hata kama ni mimi nitapita tu.

Shombo ya umagamba magamba hatuitaki CDM. Shibuda John - Your days are numbered my friend, better go back to CCM or CCM "D" aka UPD akugawie posho ya safari ya juzi U.K kudai chenge ya RADA.
 
ukiwa na mawazo kama shibuda ni sawa na kuambiwa una mtindio wa ubongo. yeye bado wa ccm siku zote kuja cdm ni unafiki wa mawazo yake. ila sijui elimu yake lakini ILLISH anasema unaposoma ndipo unakuwa mjiga na unapotibiwa ndo unaugua zaidi, hii yote hatuoni mchango wa wasomi wanaojiita maprofessa walio acha nafasi zao za kuweza kuongoza nchi na kuwaachia waheshimiwa tu, msomi gani mwoga tena anakiogopa chama cha ccm
 
MIONGONI mwa habari za kuchekesha zilizopamba vyombo vya habari jana ni pamoja na ile ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), kutangaza kugombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, lakini akimwomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, awe meneja kampeni wake.

Tunaiona kama habari ya kuchekesha kwani Shibuda alitangaza azima yake hiyo mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwenye semina iliyofanyika Dodoma, akisema kuwa Rais Kikwete awe mpiga debe wake, maana kwa kazi nzuri aliyofanya nchini kwa kipindi cha miaka aliyokaa madarakani, atafanikiwa.

Bila woga wala kujali kama alikuwa anajichafua mwenyewe na kukidhalilisha chama pamoja na viongozi wake, Shibuda aliisifu CCM kuwa imejijenga kimfumo kuanzia ngazi ya juu mpaka mashinani, jambo ambalo linarahisisha utoaji haki kuanzia chini mpaka juu.

Kwa maono yake ni kwamba licha ya makandokando na madhaifu yote ya CCM, bado chama hicho kina nafasi kubwa ya kuendelea kuongoza dola, eti mpaka sasa vyama vya siasa vya upinzani bado havijawa na uwezo wa kutekeleza chochote zaidi ya CCM.

Tunaheshimu mawazo ya Shibuda, kwani anayo haki kikatiba kufanya hivyo, lakini kauli yake tunaitafsiri kama ni matusi makubwa kwa chama chake, viongozi wake na hata yeye mwenyewe kama mwanachama wa upinzani.

Kwanza, Shibuda kama mwanachama na kiongozi ndani ya CHADEMA, anafahamu wazi kuwa upo utaratibu wa kutangaza nia ndani ya chama chake, sasa kwanini afanye hivyo kupitia mkutano wa CCM?

Lakini pia tunachelea kuamini kama kweli Shibuda ni muumini na mwanachama hai wa CHADEMA, ikiwa anaamini hakuna chama mbadala wa CCM mpaka sasa halafu akaendelea kuuhadaa umma kwamba naye ni mpinzani.

Pili, kitendo chake cha kumwomba mwenyekiti wa CCM awe meneja kampeni wake, ni matusi makubwa kwa viongozi wa CHADEMA, yanayomaanisha kwamba safu yao inayumba, hivyo haina uwezo wa kumwombea kura, lakini wakati akielewa wazi kuwa hao hao ndio walimwombea ubunge.

Tunaamini kuwa kwa kauli hizo za Shibuda hata kama alikuwa anafanya mzaha, inatosha kuthibitisha mkanganyiko wa uanachama wake CHADEMA, kuwa alikimbilia huko kupata uongozi, ila moyo wake bado uko CCM.

Maana haiingii akilini hata kidogo kwa mwanasiasa kuendelea kupoteza muda kwenye chama anachokiona hakikidhi matakwa yake, halafu akakichukia chama kingine, wakati huo akikimwagia sifa lukuki.

Ni imani yetu kwamba wakati umefika sasa kwa CHADEMA, kufanya uamuzi mgumu kwa Shibuda kama walivyokuwa wakitahadharishwa tangu mapema mara tu baada ya kumpokea kada huyo na kumteua kuwania ubunge.

Kwa mwenendo wa matendo na misimamo ya Shibuda muda mfupi aliokaa CHADEMA, unatosha kuueleza ulimwengu kuwa hayuko safari moja na wenzake, hivyo njia nyepesi ni kumwacha arejee huko CCM anakodhani ni bora zaidi.
 
Mbunge wa Maswa Magharibi-CDM John Magale Shibuda ametangaza rasmi nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 kupitia chama chake cha CDM.

Shibuda alitangaza nia hiyo mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ambao walikuwa kwenye semina maalum. Shibuda alihudhuria semina hiyo kama mwakilishi anayewakilisha vyama vya upinzani.

Katika hali ya kushangaza Shibuda alimuomba Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete kuwa Meneja wake wa kampeni na kusema itakuwa rahisi zaidi kwake kushinda atakapoungwa mkono na Rais Kikwete kutokana na mambo makubwa aliyofanyia taifa hili tangu awe Rais.

Pia katika hotuba yake hiyo Shibuda alikishutumu vikali chama chake cha CDM na upinzani kwa ujumla kwamba hawajakomaa na viongozi wake wengi ni wanaharakati.

Shibuda alisema kwa hali ilivyo CCM itatawala hata miaka zaidi ya 50 ijayo kutoka na ubovu wa vyama vya upinzani.

Alisema CCM imekomaa na inatekeleza vema ilani yake ya uchaguzi huku ikipendwa na wananchi kote vijijini Tanzania.

Katika hotuba hiyo Shibuda alikuwa anashangiliwa kwa Mayowe na wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM.
 
Mmeshawahi kuona mtu anaenda kutangaza kugombea kwenye kambi nyingine zaidi ya ya kwake na kuomba mshhenga wake awe "adui yake"? Huyo mtu anapaswa ashughulikiwe kabla hajachafua zaidi. Kuna somo kubwa kwa CDM kupokea magamba kwa tahadhari
 
Chadema nyang'anya kadi huyu jijamaa...huyu bado gamba ,ila hatupi tabu maana anaonekana hamnazo.
 
Back
Top Bottom