Shibuda ageuza bunge sehemu ya mipasho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda ageuza bunge sehemu ya mipasho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Feb 11, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Alianza kwa kushukuru kama kawaida lakini baadae ni kama alikuwa mshahiri hivi kwa jinsi alivyokuwa akiongea mpaka kengele inagonga akaomba aendelee kama wabunge wataridhia.
  Kiujumla siwezi kumquote accurate lakini alikuwa kama mahoka kwa jinsi alivyokuwa akichangia hoja bila mwelekeo. Haaaaah Shibuda ukiendelea hivi sijui kama utafika mbali?
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,027
  Likes Received: 3,220
  Trophy Points: 280
  Wadai ujana wao utawapeleka pabaya. Wakae watulie, na wajifunze kwa wazee.
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  huyu ovyooooo tu, mipasho ndo kawaida yake daima
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hata mie nimemsikia ila kweli sikuweza kuelewa anasema nini na nini ni msimamo wake kweli umenikumbusha MAHOKA
   
 5. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  sijakuelewa, what do u mean?
   
 6. c

  cray Senior Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani maneno aliyoyatoa Shibuda na makofi aliyokua anapigiwa na ccm, ni dhahiri amenunuliwa kuiua CHADEMA. Alikua akiimba mashairi aliyokua ameyandaa kwenye karatasi bila hata spika kumwambia asisome kama kananu inavyotaka. Kimakusudi alipomaliza Cheyo nae akafanya kama alivyoagizwa na ccm afanye. Hali inatisha, yaani mbunge badala ya kuchangia hoja zenye maslahi unaanza kwa kuwasema wengine kana kwamba hawajui wamo mle kufanya nini, hii maana yake ni nini?
   
 7. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Aghhh,sasa unaleta habari nusu nusu ndo nini?
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Kafulia, Fagio (Cheyo), Shibuda, Hamad Rashid ni wabunge ambao wana uhakika wa kushinda uchaguzi wowote kwenye majimbo yao hata kama watashindana na Kikwete. Hao ni rahisi sana kutumiwa maana walishawapumbaza wananchi wao.
   
 9. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hata mimi maana nikitaka kupata flow yake nashindwa maana hajamaliza hiki karukia hiki yaani vurugu tupu!
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Jamaa si kiongozi bali mtu flan muuza sura na mweny kutaka kuonekana tuu.
  si mfasihi bali mropokaji
   
 11. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Presentation yako inahitaji ufafanuzi zaidi. Kinachosekana hapa ni nini alichosema Shibuda. Hapo ndipo penye mfupa wa kujadili.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Watu wengine wapumbavu sana... Mbona ccm wanafanya mipasho ham semi acheni mambo ya kipumbavu
   
 13. c

  cray Senior Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani imewasikia nikama walipanga, Shibuda na Cheyo, huwezi amini, Katika shairi lake lina maneno kama usomi si kujaza mabuku kichwani bali hata kujifunza na kutulia. Cheyo nae anadai vijana wawe na discipline watulie wajifunze kwa wazee. Yaani hawa si wapinzania kabisa.
   
 14. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Shibuda kafanya nini hamsemi, mnaponda tu. Shibuda kageuza binge sehemu ya mipasho wakati hujaweka hata mpasho mmoja! Kama nia ni kumponda kwa vile hamuelewi alichosema basi mngeponda tu hapo mbele ya TV bila kuanzisha thread JF. Ina maana mnataka kuongeza number za thread mlizoanzisha na post mlizochangia? Kama huna cha kuandika, kinachoeleweka kaa kimya, hutakuwa umevunja sheria.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Baba mpinzani kuleta mipasho ni aibu kwani kila wakati wanatakiwa kutoa vitu vya kuumiza vichwa na si mipasho. CCM tumewazoe mbona jana Komba kalala na leo kafuka moshi balaa kwenye kikao lakini siyo habari lakini angekuwa mbunge wa CDM kalala sijui ingekuwaje? Kuwa mpinzani ni kazi siyo lelemama!
   
 16. leseiyo

  leseiyo Senior Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa ujumla Shibuda haonekani kuwa muumini wa chama cha Chadema kutokana na kile alichokisema leo bungeni. Ingawa hakuwa anataja majina anaonekana wazi kuiponda CDM na viongozi wake huku akionekana wazi kuponda Chama chake. Kwa mfano anasema kwamba CCM iwafundishe wapinzani kujitambua.

  Ametoa sifa kibao huku akisema kwamba toka ajiunge na upinzani (CDM) ameona mambo ya ajabu na kwake yeye anailaumu CCM kwa kushindwa kulea upinzani. Alikuwa akishangiliwa muda wote na Wabunge wa CCM na CUF. Kwa ufupi hafai kuwemo CDM
   
 17. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni ngumu sana kubaini mamluki. Pamoja na uruhani na mipasho hiyo ya shibuda bado ameongeza idadi ya wabunge wa cdm na hiyo ina maana pana katika jitihada za kuidondosha sisiem.
   
 18. leseiyo

  leseiyo Senior Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa Katibu wa wabunge wa CDM John Mnyika aliomba wabunge wote wakutane.Nadhani suala la Shibuda litakuwa linajadiliwa.To me Shibuda ni wa kusimamishwa ubunge na kama ikiwezekana Kamati Kuu ya CDM imtimue mara moja.Kwa kilichojitokeza leo bungeni ni fedheha kubwa.Shibuda ni makapi na hafai kuwa ndani ya CDM
   
 19. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  tuache longolongo,tuanzishe moment,serikali ing'oke madarakani.Maisha yamekuwa magumu huku bunge likiendelea kupiga soga mjengoni
   
 20. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kweli huku akijua kuwa nguzo kubwa ya CDM ni vijana amewaponda wabunge vijana kuwa wawe na busara na kuwa wazee ni hazina, yaani hata nimeshindwa kuwa specific ya yale aliongea lakini kwa tuliomuona amefuka Moshi sana.
   
Loading...