Nianze kwa kusema kuwa misingi ya demokrasia imejengwa tangu enzi na enzi katika principle ya demokrasia na uwajibikaji. KWa maana nyingine, demokrasia kamwe haiondoi uwajibikaji wa watu husika. Hii ndio maana pamoja na kushinda kwa kishindo, Hitler aliondolewa madarakani kwanguvu ya majeshi ya kimataifa katika vita kuu na sasa tunaona hata baada ya kushinda uchaguzi Mubarak ameondolewa kwa sababu ya kushindwa kuwajibika baada ya demokrasia kumpa ukuu wa nchi.
Tukirudi nyumbani CCM iliwahi kuwa chama nguli kisicho na mpinzani. Naam, ni unguli wa CCM uliofanya hata kura ya maoni kuona kwamba Tanzania ipo tayari na vyama vingi ilileta matokeo kuwa watanzania zaidi ya asilimia 90% waliona CCM inafaa kuongoza pekee. KWanini CCM ilikuwa bora? Ni kwasababu Nyerere alihakikisha misingi ya demokrasia na uwajibikaji inatunzwa wakati wote akiwa hai. Nitakupa mfano hai wa marehemu Horace Kolimba Katibu Mkuu wa Zamani wa CCM. Huyu kwa kutumia "demokrasia" aliongea waziwazi kuwa CCM imepoteza dira. Tukumbuke kuwa Kolimba hakuwa fisadi na wala hakuwa na kashfa yoyote ile wakati huo. LAkini Nyerere alimkanya na baadae kiumtungia kitabu (na Kolimba alitimuliwa CCM badae) kwa sababu ya msimamo wake huo. Sio kwamba alionewa ila aliadabishwa kwa kutumia uhuru wa kuongea (DEMOKRASIA) vibaya. Kolimba kama kada mwandamizi alitakiwa ajue kuwa ALIWAJIBIKA kuionya CCM lakini katika platform (eneo) maalum kwa kufanya ivyo. Kolimba angeweza kuionya CCM katika vikao vya chama na huko angesikika vyema. Lakini kwa yeye kutumia platforms zisizo sahihi, aliitumia Demokrasia vibaya.
Miaka imepita na Nyerere hayupo tena. KWanini nasema CCM ni mfu. CCM imekufa kwasababu uwezo wa chama kuruhusu demokrasia huku ikihakikisha uwajibikaji haupo tena. Leo hii Lowassa anaweza kujiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa ya ufisadi lakini bado anapewa uhuru wa kuwa mjumbe wa kamati mkuu na sasa mwenyekiti wa kamati ya bunge. Ni ufu huu huu unaomwezesha Rostam kuonyoya Tanzania kwa Richmond, DOWANS lakini bado ni muheshimiwa CCM. Uhuru wanaopewa akina Makamba na Tambwe Hiza kutukana hata marehemu wa Arusha bila kuwajibishwa kutokana na matamshi yake ndio ulioiua na unaondelea kuiua CCM paka sasa hakuna mtu mwenye haki na akili sawasawa anataka kuwasikia.
Nirudi kwa Cancer ya CHADEMA niliyoiita SHIBUDA. Ikumbukwe kuwa cancer hii iliingia CHADEMA pale tu iliposhindwa kura za maoni CCM. KWaiyo CANCER SHIBUDA hakuwa na nia ya ndani ya ila tamaa ya kuukwaa ubunge ndio uliompeleka CHADEMA. Angesamehewa na kukubalika ikiwa tu ana adabu na kufuata principle ya uwajibikaji. Kinyume chake, CAncer SHIBUDA amekuwa mstari wa mbele kusambaza sumu CHADEMA. KWa mfano:
1. Aligoma kuingia na kutoka wakati wa hotuba ya mkwere kinyume na uamuzi wa CHADEMA uliotokana na kura halali za wanaCHADEMA walioko bungeni.
2. Alihudhuria sherehe iliyoandaliwa na CCM ya kufungua bunnge kinyume na matarajio ya wana CHADEMA
3. Katika tukio la mauaji ya ARUSHA ameonyesha wazi kuwa upande wa CCM
4. Amewahi kukunjiana ngumi na mbunge mwenzie toka MWanza amabe ni mwana CHADEMA halisi bwana Ezekiel Wenje
Haya yote na mengine yanaonyesha kuwa CANCER SHIBUDA haifai kuwepo CHADEMA na ikiachwa kama CCM ilipotoka kupendwa na zaidi ya asilia 90 ya watanzania na sasa kuchukiwa, CHADEMA itafika huko si muda mrefu.
NAWASHAURI VIONGOZI WA CHADEMA KUFANYA KIUME NA KUMVUA UANACHAMA CANCER SHIBUDA. Nafahamu mbunge mmoja atapungua ila nina uhakika hiko kiti kinaweza kurudi CHADEMA maana watu wameichoka CCM.
Pili chaguzi ni nzuri kwa upinzani maana zinaviweka vyama vya upinzani kwenye macho na masikio ya wapiga kura. LEteni by election na watu wataendelea kuwasikiliza maana kama mnavyoona, PUNGUANI MAKINDA hatawawezesha kuongea bungeni.
Nafahamu kuwa Zitto nae amekuwa ndumilakuwili kama CANCER SHIBUDA ila kwa mawazo yangu, kabla ya mkwere kumpa nafasi katika kamati ya madini, Zitto alikuwa anajitambua. In fact, wakati huo Zitto alikuwa moto kuliko hata Dr. Slaa. Na kwasababu CHADEMA imetoka mbali na Zitto, naamini amekwisha earn respect tofauti na hii CANCER iitwayo SHIBUDA. TAFADHALI CHADEMA msichelewekumuondoa CANCER SHIBUDA manake msipom-discredit mapema, ataendelea kutumiwa na CCM kuisambaza sumu yake CHADEMA na kukiuwa chama. Kolimba alitimuliwa kwa kuwa mkweli bila kuwajibika sembuse hii CANCER ambayo haina faida na CHADEMA? CHADEMA ni wakati wa kuonyesha kuwa hakuna aliye juu ya chama. NAOMBA KUWASILISHA!!