Sheria ya kumhudumia mwanamke ifutwe, kwa sasa ajira zinatolewa kwa wote bila upendeleo!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Sheria ya Mwanaume kumhudumia Mwanamke ifutwe. Sheria ya mke kuchukua mkopo kwa Jina la mumewe nayo ifutwe. Ni sheria zilizopitwa na wakati na zisizoendana na ulimwengu wa sasa.

Ni sheria kandamizi, zinazomkandamiza Mwanaume. Kwa zamani zilikuwa sheria nzuri lakini sio sasa. Zilikuwa nzuri kwa sababu wanaume walipewa fursa zaidi kuliko wanawake. Wanaume walipewa fursa ya kumiliki Mali huku wanawake walikatazwa.

Wanaume walipewa fursa ya kusoma na kutafuta elimu huku wanawake wakiachwa nyuma. Wanaume walipewa fursa ya kutafuta kazi na kufanya shughuli za uzalishaji huku wanawake wakibaguliwa.

Ndio maana sheria ya kumhudumia mwanamke ilikuwa ya maana na tunaweza kuiita sheria ya haki kama Watibeli tupendavyo Haki, lakini siku hizi kila mtu anahaki. Haki sawa baina ya jinsia zimeboreshwa na kulinganishwa. Ikiwa ni hivyo basi na wajibu lazima uboreshwe.

Isiwe wajibu kwa mwanaume kumhudumia mwanamke katika ulimwengu wa haki sawa. Vijana, sio wajibu wako kumhudumia Mwanamke katika ulimwengu huu wa haki sawa. Ndio maana dunia ya sasa imetoa usawa wa kifursa.

Mwanamke afanye kazi na wewe ufanye kazi. Wote mlete mezani. Hiyo ni Haki. Mwanamke akifanya kazi alafu anataka kuhudumiwa tuu yaani hela yako anaikodolea macho fukuza. Usiwe mjinga. Huo ni ubinafsi.

Mwanamke ambaye atakuambia pesa ya Mwanamke hailiwi wakati unamuita sijui mpenzi, sijui mkeo, huyo ni tapeli, nyonyaji. Huyo hakufai. Piga chini wala usisite mara mbili mbili.

Ndoa za kitapeli, mahusiano ya kibeberu na kikoloni. Unakuta mwanaume mzima kumbe ni koloni la mtu. Unanyonywa kama mwendawazimu. Halafu miaka 45 hii hapa kisukari, presha, mara Stroke unaacha mke watu tunapiga.

Shauri yako. Usijesema sijakuambia.

Usiendekeza ujinga.
 
Kabisa yaani
Siku hizi hawaangalii kama una afya, una akiki timamu, unatokea dini ipi au ukoo upi! Ukisha kuwa na kastatus ka pesa tu haoo chaap na mikakati ya kuitoa roho inaanza ili mtu arithi au aibe kilichomleta!
Nadhani nikosa kubwa lilifanyika kumruhusu mwanamke kumilikishwa baadhi ya haki za mwanaume!
 
Back
Top Bottom