dungune
Member
- Nov 10, 2021
- 70
- 157
Habari Wakuu,
Ninaomba kufahamishwa sheria ya ndoa Tanzania inasemaje ikiwa umezaa na mke wa mtu? nataka kujua kama unaweza endelea kutoa matunzo ya mtoto akiwa kwenye familia nyingine. Na unatakiwa kufata utaratibu gani kumchukua mtoto anapo fikisha umri wa kulelewa na baba.
Hii imenitokea kwa mwanamke ambae nilizaa nae mwaka 2017 kwa kipindi cha miaka minne nimekuwa nikitoa matunzo yote kama mzazi mpaka mwaka jana nilipo pokea simu kwa mtu ambae alijitambulisha kama mume halali wa mama mtoto.
Nilishangaa sababu mwanamke alinitambulisha kuwa yeye ni single mama nilipo muuliza jamaa alikuwa wapi kwa kipindi chote anasema alikuwa safarini. Na mwanamke anakiri kweli ni mume wake na waliishi pamoja ila mwanaume alimtelekeza akaenda kuishi na mwanamke mwingine.
Sasa baada ya malumbano ya muda mwanaume akachukua simu ya mama huyo akaiharibu ili nipoteze mawasiliano na mimi nikaamua kukaa kimya ili kuona nini huyo dada atafanya nini.
Baada ya miezi miwili nikapokea simu kutoka kwa jirani wa mama wa mtoto huyo akinijulisha hali ya mtoto sio nzuri hakuna uangalizi tena maana nyumba imekuwa uwanja wa vita. Nikajiskia vibaya sana mana kweli ni damu yangu ila watuwazima na makosa yetu ndio tunapelekea watoto kuwa na mazingira magumu.
Lengo la kuja hapa ni kutaka kujua uhalali wangu kwa mtoto huyo na si mwanamke ili tu mtoto apate haki yake ya malezi.